FATHER OF REALITY
Senior Member
- Nov 3, 2014
- 123
- 100
MUHIMU: Mada hii ni ya kujifunza zaidi na kujifunua juu ya utu wetu, tujifunze kutafakari vyema, usijae upepo, build the capacity of having the inquisitive mind.
Katika uzoefu, pitapita, mabishano, majadiliano na minong'ono, mara nyingi nimesikia wanaume wakilalamika sana juu ya wanawake kuwa watu wenye roho isiyo na utu na wasaliti mno, hata wengine wameenda mbali zaidi wanadai mwanamke ni mkatili zaidi ya mwanaume , wanaonya kwamba si kiumbe wa kumkumbatia ukiamini kwamba kwake kuna ulinzi.
Mimi binafsi nikaamua kukaa chini na kufikiri kwa kina juu ya ukweli wowote kati ya hayo yanayodaiwa kuwa ni sifa hasi za mwanamke, baadaye nikapata mang'amuzi juu ya malalamiko hayo.
1.Utu wa mwanamke hauthaminiwi sawasawa na mwanaume, hivo hubeza na kudharau kila lifanywalo na mwanamke.
2.Vilio vingi vya wanaume dhidi ya wanawake vimejengwa juu ya mwamba wa uhusiano wa mapenzi, ambapo juu ya hilo hupanuliwa hata kuingia katika familia n.k
3.Wanaume hujitengenezea haki wasiyostaili hata mbele ya Mungu na utu wenye usawa.
4.Wanawake wanatendwa kikatili sana katika mapenzi na mahusiano, lakini utamaduni wa mwanamke kuwa kama mtu wa pili ndo humfanya habari zake zisienee sana, si hodari wa kutangaza na hana platform(jukwaa la kuzungumzia na kusikilizwa), la wataambiana wenyewe na kuendelea kulalamika chini kwa chini.
5.Kuhusu ukatili, ni wazi kwamba wanaume ni wakatili mno na ndio watu pekee wanaoweza kufanya dunia isikalike, madhara ya mwanamke huishia kwa mtu mmoja mmoja, kitandani, chumbani, nyumbani katika familia kwa upana wake.
kuna vijisababu vingine vingi lakini hivyo hapo juu vitafungua kichwa.
Sasa wanajamvi naomba nimtoe mwanamke katika yale madai ya ukatili ambayo mengi pia ya kinadhalia yaani kufikirika, hasa yakijikita katika mambo ya kichawi.Naomba niangalie zaidi katika swala mama la uhusiano wa kimapenzi.
Jamii yetu imepotoka sana mbele za Mungu na amri zake, maana katika jamii zetu mtoto wa kiume kumweleza kaka yake kwamba ana girl friend si shida na hiyo si laana wala taabu na haisumbui kichwa, sana sana atasifiwa kuwa aaah, huyo dogo kidume bwana na kuonywa onywa kidogo juu ya kutumia kondom iwapo hamwamini huyo mpenziwe.
Pia baba akijua si iishuuuu, mama pia hatolalama sana. Mtoto wa kike akigundulika kwamba anampenzi au na dada ake, au mamake, atapokea maonyo makali sana, mbaya zaidi kaka afahamu hilo, hiyo ndo itakuwa balaa, hata wengine huchukua hatua ya kuadhibu na mwishowe hupongezwa na wazazi.
Hili lilinifanya nikapitie tena amri ya sita na hata maonyo juu ya uasherati, nikakuta pameandikwa USIZINI, pia juu ya uasherati imeandikwa"muasherati yeyote hatauona ufalme wa Mungu" kumbe wanawake kwa wanaume kwa mujibu wa Mungu twaambiwa uzinzi na auasherati ni dhambi, hivo si halali kwa wote.
Wanaume hufanya mapenzi na wanawake, lakini sisi tunaona ni vyema kwa mwanaume kuwa na wapenzi wengi na ni haramu kwa mwanamke kuwa na mwanaume au kuwa malaya, wanaume ni mafundi wa kujadiliana mabo mbalambali tena kwa akili za juu, yaani katika hili tumefeli vibaya, mfano kuna wanawake A, B, C, D, E na F, kuna wanaume A1, B1, C1 na D1, kisha kila mwanaume ana wapenzi zaidi ya watatu, wahat dou you expect to the side of women.
Na labda nikutafakarishe we mwanaume mwenzangu uliye kimbelembele kuwadharau wanawake na kuuona si waaminifu wakati wewe kule kazini umeshalala na mama lishe, naye sekratari wako pia, kuna msichana ulikutana naye kwenye daladala mpenzio, huku unaiba mke wa mtu, baamedi sita ushalalanao.
Mi nakuambia wewe unayejiita mwanaume hawa wanawake hawa hata hivyo ni watu makini sana, maana wao huitwaitwa manjiani, kusifiwa, kuahidiwa offa mbalimbali, pesa n.k, ungekuwa wewe na hakika ungekuwa kicheche mara mia ya hawa.
Fact nyingine, wanaume tumekuwa wajinga sana utasikia, aah, yule, hana kitu yule nshaamchapa, nanai kakwambia kuchapwa kwake ni maumivu, yaani tunawapa raha, na kwa kuwa sisi ni mabozo wanajua ujunga wetu, wanalia lia pale katika bed naumia naumia, basi na hela tunawapa.
Tusilolijua wanaume
-Wenzetu wanapewa raha na kulipwa pia, nani mjinga, afu hujiulizi kama wewe unamkomoa mbona ana wanaume watatu, wawili wa pesa ukiwemo na wewe anayekuambia wamuumiza, na mmoja hana hela au anayo huyo hupewa huduma tena kwa vishindo kiliko wewe.
-Tuanuishi ujinga wetu na kujifariji
-Mwanamke naye hupata hamu kama upatayo wewe, hvo hutafuta mpenzi.
-Sisi tu tunawahitaji wao, na wao wanatuhitaji sisi tena sana, ila sisi katika mabo hayo tu malimbukeni mno.
-Wewe unavoona wanao, wadogo zako wa kiume ni mashujaa kwa kuwa na wapenzi, ndo kadili hiyo hiyo na wadogo zako wa kike watakuwa na wapenzi wavulana watokao familia nyingine.
-Utaalamu wako wa kutamani na kusifia wanwake na wake za watu kwa uzuri na hata kuwatongoza, ndo hivyo hivyo kwa mkeo na dada zako pia, taauti yao wao hawana kelele, hawazungumzii sana.
-Mwanaume ni mregevu zaidi ya mwanamke maana anaacha mke nyumbani, anamtafuta changudoa, changudoa anastareheshwa, kisha mwanaume, yaani mtoa huduma anamlipa changudoa tena kwa hela aliyoitafuta kwa jasho mnoo, tukubali sisi malimbukeni hasaa.
-Mwanake ana nafuu kubwa mno, kwanza jamaa anampa starehe afu anaahidi kumpa ofa mbalambali kama pesa, gari nyumba nk. anafanya jambo ambalo kidunia lina faida mara mbili, mnasema huyu mjinga, hebu fikirini vizuri wandugu.
-Wanaume wengi wanasaliti ndoa zao tena kwa kugharamikia, wanawake husaliti ndoa kwa kugharamiwa, nani alistahili viboko kati yao, mmmmhhmm.
Baada ya hapo nikajua kama ushenzi basi binadamu ni mshenzi kila mtu kwa nafasi yake, ukitaka mshenzi aliyezid, hakika ni mwanaume maana, yeye anashiriki vitu vyote, mwuuaji mkubwa, mvuruga amani, malaya, gaidi, jambazi, mbaya zaidi ni shoga n.k.
Binadamu ni mkengeufu na ameharibika kimaadili.
MUHIMU: Mada hii ni ya kujifunza zaidi na kujifunua juu ya utu wetu, tujifunze kutafakari vyema, usijae upepo, build the capacity of having the inquisitive mind.:nod::nod: