Mwanamke mwolewaji huyu hapa!

stanslausk

New Member
Feb 9, 2012
4
7
Nionavyo mimi mwanamke mwolewaji anasifa zifuatazo. (zingatia: mapenzi hayana formula only use this as a rough guide).

  1. Huruhusu mapenzi yawe wazi.hivyo mara nyingi atakutambulisha kwa ngudu na marafiki zake.
  2. Hapendi kukuingiza gharama. Daima atakushauri kuhusu matumizi mazuri ya pesa. Si mpenda makuu na mara nyingi kabla hajakutolea shida inayohitaji fedha nyingi, kwanza atazingatia umuhimu/ulazima wa hiyo shida sambamba na uwezo wako.
  3. Ni mkweli na muwazi. Akipata matatizo au changamoto mbalimbali atapenda kukushirikisha ili umsaidie hata kimawazo. Atakueleza mambo mengi kuhusu familia yake. Atakueleza hata mambo yake binafsi ambayo ni siri na labda hajawahi kumweleleza mtu mwingine.
  4. Ni mshauri mzuri. Atapenda kukushauri ufanye nini ili ufanikiwe. Yuko tayari kuishi kwa kujibana ili kuku-support utekeleze mambo Fulani ya kimaendeleo.
  5. Ni msaidizi. Yuko tayari kujitoa hata kifedha kukusaidia. Ni kama anakipato atapenda kuchangia gharama ktk mambo mbalimbali kwa mfano mnapoenda viwanja kuspend
  6. Ni mwaminifu na mwenye upendo wa kweli.
  7. Atakuheshimu na kukuthamini. Mapungufu yako hatayatangaza kwa watu
  8. Atawapenda na kuwaheshimu ndugu zako.
  9. Atapenda kuwa karibu na wewe.atawasiliana nawe mara kwa mara hasa mnapokuwa mbali.
  10. Ni msikivu.yu tayari kukosolewa. Huwa tayari kubadilika ili muendane.mathalani, ataepuka kurudia kufanya mambo ambayo huyapendi. Yoku makini katika kauli zake. Kwa mfano wanawake wasio serious na mahusiano pindi mnapolumbana haraka hurukia kauli eg: kama vipi tuachane: unaweza ku-quit kama unaona sikufai.
  11. Hupenda suluhu pale mnapotofautiana. Mwepesi wa kukiri kosa na kuomba msamaha pale anapokukosea.
  12. Mvumilivu. Atakuvumilia pamoja na mapungufu uliyonayo.
  13. Anaweza kuanza ku”assume responsibilities” za mke hata wakati bado hamjaoana (chonde simaanishi tendo la ndoa).Mfano anapokutembelea kwako anaweza kukupikia,kukufulia,kukuchagulia nguo za kuvaa n.k
 
good guideline; but hapo kwenye namba 2 ndiyo palipo na changamoto ya kikwelikweli
 
good guideline; but hapo kwenye namba 2 ndiyo palipo na changamoto ya kikwelikweli

Hahaha,

Kuna wengine anakutangazia kabisa kwamba "mimi ni high maintenance" akitaja hivyo kama sifa, kabla hujajitutumua ujue kabisa, usije kuyavulia nguo maji halafu kujisikia baridi mwenyewe.
 
Itanibidi nimpatie jamaa yangu asome maana huyo gf wake kwa mizinga hajambo halafu akienda kwa jamaa hafanyi chochote anamwambia bado hujamuoa.
 
Ngoja niongezee No. 14
Hawezi kutoa penzi kwa mwanaume mwingine!
 
mh hiyo na. 13 unawezajikuta mmepangwa ka nyanya leo anakuja kufua asha, kesho anakujapiga pasi eliza keshokutwa anakujakupika hadija. kha mwenzenu huwa namtaftia house girl wa muda kufanya vyote hvo. cha kujichosha nin mwisho wa cku unajikuta kaolewa anna pamoja na kufanya yote hayo!
 
Itanibidi nimpatie jamaa yangu asome maana huyo gf wake kwa mizinga hajambo halafu akienda kwa jamaa hafanyi chochote anamwambia bado hujamuoa.

usikute huyu gf analeta swaga wakati kuna vidume vingine pembeni vinakula bure tu
 
mkuu uliyoyasema ni kweli kabisa, nimezipenda zaidi namba 10 na 11.

ila pia tahadhari ichukuliwe kama :
namba 1: unaweza tambuliashwa kila mahali.....wakakuchekea na kukuita shemeji kumbe wanakuchora......

Namba 3: hii inawezekana kama wewe si buzi, maana wengine hukueleza matatizo yao ili kukuvuna....

Namba 6:hapa ndo penye shughuli kwenye mahusiano mengi.....jinsi gani utaprove uaminifu wake kwako.....

Namba 7: mmmmmmh maybe....

Namba 13: Be careful....hutumika kuwaingiza king wanaume wengi.....kumbuka baadhi ya wanawake wasanii...

Hivyo nadhani pamoja na kuwa mwongozo wako ni mzuri sana.....(nitaucopy nimpe mtu mmoja hivi) ni vyema kuwa na tahadhari hapa na pale....maswala ya moyo haya ni tata...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom