Mwanamke mwenye uhitaji wa ndoa huwa sio king'ang'anizi

IMG-20170605-WA0003.jpg
 
Ukisoma Biblia takatifu ,utakuta neno ndoa limezungumzwa mara 38 katika vifungu 38 ,na ukisoma kitabu cha Methali[ 31:10-31] Mke mwema kweli, apatikana wapi?

''Huyo ana thamani kuliko johari! Mumewe humwamini kwa moyo, kwake atapata faida daima. Kamwe hamtendei mumewe mabaya, bali humtendea mema maisha yake yote.'''

Kizazi hiki wanawake wanahitaji harusi ,na wanaume wanahitaji ndoa,ndio maana katika katika harakati za kufunga harusi wanaume wengi hukonda na wanawake wengi hunenepa sababu ,mmoja anahitaji harusi na mwingine anahitaji ndoa.

Baada ya harusi na safari ya ndoa inapoanza ,mwanamke hukonda na mwanaume hunenepa sababu ,Harusi ni sherehe ya siku moja wakati ndoa ni agano la milele,wanawake wanakamia sana harusi kuliko kukamia ndoa zao.


Mwanamke mwenye uhitaji wa ndoa huwa sio king'ang'anizi wa harusi hata siku moja ,yeye hutizama agano takatifu la ndoa ambayo inaweza kufungwa bila ya harusi wala gharama kubwa .Wanawake wa aina hii kwa kizazi hiki hawapo na wanapatikana kwa kufunga na kusali pekee.

Mwanamke anayehitaji ndoa baada ya kufika katika kilele cha mafanikio ya maendeleo ya ndoa na furaha ya ndoa yake ,hupendekeza kwa mume wake wabariki ndoa ndipo mume wake hupokea shauri la mke wake sababu ya hekima na busara ya mke wake na kuibariki ndoa.

Wanawake ,msilazimishe kufunga harusi wakati uwezo wa
wanaume wenu mdogo,harusi ni sherehe ya siku moja na ndoa ni agano la milele,tuwekekeza fikra za kutengeneza ndoa nzuri na bora na sio kuwa na hamasa ya kutengeneza harusi bora na tamu.

Dear brothers maisha ya sasa yanahitaji mwanamke mwenye akili na sio mwanamke mzuri ,sababu unaweza pata mke mzuri asiye na akili na ukapata mwanamke mwenye akili asiye mrembo-uzuri wa mwanamke huwa haudumu milele ila akili ya mwanamke hudumu milele.To be married by the person you love the most is the greatest blessing God can give.

b32099cf591a5805e94ced66cdf0a3fc.jpg
umesema ukweli mtupu mim nimempata mwanamke wa ndoa kwa kuwa alinishauri tuachane na sherehe tupange maisha na familia yetu itakavyokuwa
 
Acha porojo na upoyoyo

Unafikilia, Babu na bibi zetu wote walikuwa na hizo ndoa za vitabu vya wazungu na Waarabu!?

Ndoa ni mke na mke waishi pamoja, ikitokea wakaza watoto poa.

Vinginevyo ni kuleta vikwazo vya watu kuishi kwa amani.


Mfano, dini nyingi za kilokole zimeharibu mabinti na vijana kwa vigezo uchwara Kama hizo za kufunga ndoa mara sherehe za kabla ya harusi za kipoyoyo na mwisho wake wamejikuta kwenye ndoa za kutojitakia .

Kwa sababu, ya kufanya utaratibu wa kuoa kuwa kama kujiunga na jeshi la marekani.

siku zote usipende kualalisha jambo kwa kupitia makosa ila jifunze kupitia makosa.
 
Haha, love this!...:)

Kibao kimegeuka, ni kazi sana kumridhisha mwanaume kwa kweli..
mnakinai sana nyie cjui kwanini..yaanii hata ukate mauno vip lazima itafika point mtu umekinai unaanza ktafuta mwingne aisee mungu atuhurumie tu
 
Kila siku wanawake wanawake tu wakati wanaoongoza kushindwa ndoa wanaume,,nenda angalau mtaani kwako kaangalie wanawake wanaolea watoto peke yao baada ya mijanaume kukimbia kwa kisingizio cha maisha magumu..
Maisha magumu au wanawake majeuri wanaume wanakimbia usumbufu........maana wanaume hao hao wanahonga malaki huko nje sasa iweje akimbie mwanamke ambaye kila asubuhi anamuachia elfu tano au elfu kumi mezani!
 
Back
Top Bottom