Mwanamke mwenye kichanga kupata ujauzito

Mwanamke mwenye kichanga kupata ujauzito

Charliemic

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2019
Posts
604
Reaction score
977
Ndugu wanajamvi, huyu mwanamke ni jirani yangu! Ana kichanga cha miezi tisa (9)!

Alinieleza njia ya uzazi aliyokuwa anaitumia ni ya kalenda! Sasa kuna kulingana na mabadiliko ya mazaringira kumbe siku zikavurugika! Pasipo kutarajia akanasa ujauzito! Je nini madhara yake!?

Je, atoe mimba au ailee haitakuwa na madhara makubwa ya kiafya badaye?
 
Alee tu hiyo mimba maana mtoto anaweza kuhudumiwa vyema na akakua. Kuna jamaa alikuwa na watoto wake wamefunga mwaka mmoja halafu twins alilea vyote, sasa hivi naona yupo poa na raha kweli.

Yupo na twin wake wa miaka miwili na kidogo na yule wa tatu alikuwa wa kiume na twins wote walikuwa wa kike. Maisha yanaenda sawa hadi sasa. Mwambie alee japo huenda ni wewe mwenyewe au mkeo
 
Ndugu yangu alipata ujauzito wakati mtoto wake anamiezi mitatu tu! Alitumia mitishamba ili mtoto asidhurike na maziwa yake na alinyonyesha mpaka mtoto alipofikisha miezi Tisa na ujauzito ukiwa na miezi sita. Wakati mtoto akiwa amebakiza wiki 2 kufunga mwaka akazaliwa mwingine now analea wote.

Asitoe mimba

Mimba asiitoe

Asitoe mimba

Mimba asiitoe
 
Ndugu wanajamvi, huyu mwanamke ni jirani yangu! Ana kichanga cha miezi tisa (9)!
Alinieleza njia ya uzazi aliyokuwa anaitumia ni ya kalenda! Sasa kuna kulingana na mabadiliko ya mazaringira kumbe siku zikavurugika! Pasipo kutarajia akanasa ujauzito! Je nini madhara yake!?

Je atoe mimba au ailee haitakuwa na madhara makubwa ya kiafya badaye??
Miezi tisa ni mingi sana. Mtoto anaanza kulishwa vitu laini laini kuanzia umri wa miezi sita ingawa, pamoja na hilo, inashauriwa mtoto aendelee kunyonyeshwa hadi miaka miwili au hata na zaidi. Sikiliza mkasa unaofuata wa jirani yangu.

Msichana wa miaka 21, binti wa jirani yangu, alizaa mara mbili ndani ya mwaka mmoja. Katikati ya Januari alijifungua mtoto wake wa kwanza. Wiki ya kutangulia Krismas ya mwaka huo huo nilimkuta kwenye baa ya jirani mida ya saa moja jioni akinywa soda. Tumbo lilikuwa likionekana dhahiri kwamba ana mimba. Aliondoka hapo kwenye saa mbili usiku. Kesho yake kwenye saa 11 jioni alikuja tena hapo kwenye baa kununua soda akiwa amebeba kitu fulani ambacho baadaye alitufunulia na kumwona mtoto aliyejifungua usiku. Kumbe jana yake alipoondoka hapo kwenye baa, alirudu nyumbani kulala. Usiku wa manane akaanza kuona uchungu; wakampeleka hospitali saa tisa alfajiri. Saa 11 akajifungua kawaida tu na saa tatu asubuhi akaruhusiwa kutoka hospitali kwa kuwa hakukuwa na matatizo yo yote. Watoto wote wawili bado wako hai na hawana hitilafu yo yote ya afya. Wanatunzwa na bibi yao, mama mzaa mama. Msichana hajaolewa. Ana Boyfriend tu ambaye ndiye baba wa watoto wote wawili. Huyo Boyfriend anatambulika hapo nyumbani kwa binti na huwa anakwenda anakaribishwa kabisa kuwaona watoto.

Watoto wawili wasiokuwa mapacha wamezaliwa na mama mmoja mwaka mmoja.
 
Alee tu hiyo mimba maana mtoto anaweza kuhudumiwa vyema na akakua. Kuna jamaa alikuwa na watoto wake wamefunga mwaka mmoja halafu twins alilea vyote, sasa hivi naona yupo poa na raha kweli.

Yupo na twin wake wa miaka miwili na kidogo na yule wa tatu alikuwa wa kiume na twins wote walikuwa wa kike. Maisha yanaenda sawa hadi sasa. Mwambie alee japo huenda ni wewe mwenyewe au mkeo

saikolojia yake inaonesha
kuw n yeye
 
Nilisema atoeeeeeee... Atoeeeee... Mtoto amuuee!!

Akasema sitoi.. Sitoi.. Atakuja kua nani sijui...,

Mama yako jasiriii, ngoja nikupe story....,

Dah.. 20 Percent Fundi wa mziki.

Turudi kwenye Mada!;
Mkuu, watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, ndio kitu pekee Mimi binafsi najivuniaga hapa duniani, kumbuka wengine wanaenda kwa waganga wapate japo hata mtoto wa dawa. Usiogope kulea, jiwe alisema tufafyatue tu elimu bure.

Then next time mambo ya kalenda msitumie, tumieni njia ingine.
 
Ndugu wanajamvi, huyu mwanamke ni jirani yangu! Ana kichanga cha miezi tisa (9)!

Alinieleza njia ya uzazi aliyokuwa anaitumia ni ya kalenda! Sasa kuna kulingana na mabadiliko ya mazaringira kumbe siku zikavurugika! Pasipo kutarajia akanasa ujauzito! Je nini madhara yake!?

Je, atoe mimba au ailee haitakuwa na madhara makubwa ya kiafya badaye?
Mimi nimezaliwa kwa style hio
Ailee tu

Alienitangulia akiwa na miezi 7 mimi nakua conceived

cant imagine wazazi wangu wangenikatisha maisha
 
Back
Top Bottom