Mwanamke mmoja Mwanza katupa kichanga cha siku 3 ndani ya Ziwa Victoria

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Evelyne John mkazi wa Butuja mkoani Mwanza, anashikiliwa na polisi kwa kutupa kichanga cha siku 3 ndani ya Ziwa Victoria na kusababisha kifo cha kichanga hicho.

Watu wana roho mbaya sana. Hajali hata mateso ya miezi tisa.
 
yaan wanawake sisi jaman wakati wengine tunatafuta watoto asubuh mchana na jion wengine wanatupa watoto inasikitisha sana
 
huyu mwnamke anaroho ngumu sana.. japo kisaikolojia wanasema mwanamke anapotoka kujifungua huwa na hali fulani ya ukichaa na akikosa support ya jamii au mwenzi wake ni rahisi kuweuka.. ushauri wangu kwa watia mimba embu jaribu kuwa nasi karibu hata miezi miwili ukichaa wetu upungue ndiyo muendelee a mambo mengine.. najua wengi mtamlaumu huyo mama na kuweka mbali jamii inayomzunguka na mtia mimba.
 
Tukisema kina mama wakatili huwa mnajawa povu.....mie sijawahi sikia mwanaume katupa mtoto.
 
....mie sijawahi sikia mwanaume katupa mtoto.

Wanaume hawatupagi watoto, wao huwa wanakataa mimba, wanakwepa bin kukimbia kuitunza mimba wakiwa wamejaa hofu (ujasiri mbuzi) kuwa yawezekana mimba si yake, pia wanaume wanakimbia kulea familia hata pale mtoto akizaliwa kafanana nae hadi ulimi na kuwaachia akina mama peke yao wajue watoto watakula nini, watavaa nini, watasoma au watakuwa machokoraa au watakuwa manamba kwenye mashamba ya watu, mama ndo ajue watoto watalala wapi halafu ikitokea mama kavuka yote hayo mtoto amefanikiwa ndo baba huyo anajileta utasikia dume langu hili nilizaa miaka hiyo watoto wamefata akili za baba yao au utasikia binti yangu huyu ni mtangazaji mashuhuri nilizaa wakati wa ujanani amefata akili za baba yake hapo mipua imemtanuka mwanaume kwa misifa wakati ukimuiliza huyo mtoto wako alizaliwa tarehe ngapi hajui, kasoma shule gani hajui.........

Siwatetei wamama wanaotupa watoto nachojua wanakuwa na matatizo ya kisaikolojia. Wakipatiwa maneno ya busara wakati wa ujauzito wala hawatatupa hao watoto.
 
Akichapwa bakora huyo mwanamke

Watu watashikilia bendera huku povu zikiwatoka kuwa udhalilishaji na kaonewa
 
Katika mambo yanayotia simanzi mno.. Yaani umelea mimba miezi 9 umejifungua salama mungu amekusaidia halafu unakuja kutupa mtoto ziwani..!?

Ni wakati sasa Serikali ikaweka adhabu kali sana, tunachoka kwa matukio haya kujirudia..
 
huyu mwnamke anaroho ngumu sana.. japo kisaikolojia wanasema mwanamke anapotoka kujifungua huwa na hali fulani ya ukichaa na akikosa support ya jamii au mwenzi wake ni rahisi kuweuka.. ushauri wangu kwa watia mimba embu jaribu kuwa nasi karibu hata miezi miwili ukichaa wetu upungue ndiyo muendelee a mambo mengine.. najua wengi mtamlaumu huyo mama na kuweka mbali jamii inayomzunguka na mtia mimba.

Watia mimba wanatokwa povu tu hapa kana kwamba wao hawahusiki. Wa kwanza kuhukumu na kusema wanawake wauaji na mashetani.
 
kabisa na wanakosea sana.. sababu huyo mwanamke mtia mimba kamakataa au hamtunzi anaenda kujifungua haupo karibu naye kisaikolojia lazim aathirike na hata kuchukia kiumbe au kujichukia yeye... wanaume hawawezi kukwepa kulaumiwa
 
Katika mambo yanayotia simanzi mno.. Yaani umelea mimba miezi 9 umejifungua salama mungu amekusaidia halafu unakuja kutupa mtoto ziwani..!?

Ni wakati sasa Serikali ikaweka adhabu kali sana, tunachoka kwa matukio haya kujirudia..
kwa mtia mimba na mbeba mimba
 
Wanaume hawatupagi watoto, wao huwa wanakataa mimba, wanakwepa bin kukimbia kuitunza mimba wakiwa wamejaa hofu (ujasiri mbuzi) kuwa yawezekana mimba si yake, pia wanaume wanakimbia kulea familia hata pale mtoto akizaliwa kafanana nae hadi ulimi na kuwaachia akina mama peke yao wajue watoto watakula nini, watavaa nini, watasoma au watakuwa machokoraa au watakuwa manamba kwenye mashamba ya watu, mama ndo ajue watoto watalala wapi halafu ikitokea mama kavuka yote hayo mtoto amefanikiwa ndo baba huyo anajileta utasikia dume langu hili nilizaa miaka hiyo watoto wamefata akili za baba yao au utasikia binti yangu huyu ni mtangazaji mashuhuri nilizaa wakati wa ujanani amefata akili za baba yake hapo mipua imemtanuka mwanaume kwa misifa wakati ukimuiliza huyo mtoto wako alizaliwa tarehe ngapi hajui, kasoma shule gani hajui.........

Siwatetei wamama wanaotupa watoto nachojua wanakuwa na matatizo ya kisaikolojia. Wakipatiwa maneno ya busara wakati wa ujauzito wala hawatatupa hao watoto.
na pia kila binadamu ana upande wa pili unyama (utu kumtoka)
 
Hata kama mtia mimba kakataa ndio umtupe jamani?? Bora umtelekeze hata kwa mtu au mahali ambapo ni salama sio kumuua kabisa
 
Daaaah so sad.....

Hata kama maisha yamekuwa magumu.

Si hivyo

Jina la mwanamke ndo linanifikirisha sana.Evelyn John! yaani john?majina ya kina john sijui yapoje kwani hata john fulani nimjuaye ana moyo mgumu! lkn pia yupo huyu faru alobatizwa jina la John nae anasumbua vichwa vya watu...
 
Back
Top Bottom