Mwanamke jiulize

VPN USED2020OCTOBER28

JF-Expert Member
Oct 27, 2011
1,505
671
Mkeo ni Asali na Mchepuko ni Sukari.

Hebu angalia mkeo alivyo mtamu, na mchepuko alivyo hasara.

1. Asali inatengenezwa kwa Hali ya uasili lakini sukari inatengenezwa kwa akili ya mwanadamu. (Mkeo ni ubavu wako halisi).

2. Asali ina thamani kuliko sukari (1lt ya asali ni 15,000 lakini 1kg ya sukari 2800) {mkeo ana thamani sana kuliko huo mchepuko}

3. Asali huponya Magonjwa lakini sukari huongeza Magonjwa {Mkeo ndiye tabibu halisi wa maumivu ya moyoni mwako}

4. Asali si nyepesi kuisha wakati wa kuilamba lakini sukari unawezaibugia kwa mkupuo {Mkeo huduma zake hazichoshwi kwa uwepo wako}

5. Asali ina radha kamili na msisimko wa kutosha lakini sukari unaweza ilamba huku unapiga story. {Mkeo ubora wake si sawa na ule wa mchepuko upatiakanao kwa kukimbizwa ili kuwakwepa wanaokuja kutaka huduma kwake}

Mkeo ni asali hebu faidi asali yako achana na sukari ya viwandani.
Ifunike Asali yako ili usivutiwe na sukari zilizokosa uhifadhi mzuri.... Naamini watu wazima wenye Ndoa zenu mumenielewa.

Na ambao bado liweke akilini.
Mwanamke uliyeisoma hii post jiulize
Wewe ni ASALI au SUKARI? 😂
 
Kwahiyo wale wanaosema ndoa ndoano ni waongo? Hao michepuko ndo wake za wengine sijui unalijua Hilo?

Hakuna Cha asali wala sukari hili tuliangalie kwa namba wanawake ni wengi kutushinda unafikiri tutawasaidiaje..!!
 
Asali inatengenezwa na wadudu, sukari inatengenezwa na mtu.... nani zaidi..?

Asali yako ni sukari yangu, hili kasema Depal.
 
Back
Top Bottom