Ni yule ambaye afii kimya kimya kwa kuumia na penzi ambalo analo kwa mwanaume anaye mpenda. Mwanamke jasiri ni yule anayejua nini anakitaka, anachukuwa nafasi na ku hit her target.
Dada zangu dunia imebadilika sana na hasa katika mahusiano. Kama unafikiria unampenda mtu fulani kisha unabaki kimya tu, wanawake majasiri wapo wamekuzunguka na uamua kujaribu.
Wanawake walio wise nawependa sana ila wanawake otherwise amsheni akili akili zenu. Kusubiri kutongozwa na mtu ambaye unampenda imepitwa na wakati
Loohh!! Waogopa nini. Mimi sili chips, sili chakula cha mafuta ya korie. Mimi chakula changu lazima kiungwe na karanga.
Hahahaaaaaaaaaaa!
Kijana una maono, lakini kiupeo bado mno
Nimeyakubali yako maono, ila bado mapema mno
Naomba kunyosha mkono, ili nitie japo neno
Wakati si konokono, japo hatua hio bado mno.
Ya ngoswe mtuachie ngoswe!
Kutaka kula kingi, hujukuta umeliwa nyingi.
Katu bf sio kingi, labda mumeo ndo umfanye kingi.
Bf atakutia utumwa mwingi, akivike majukumu mengi
Atakuwekea vingi vigingi, nakukupoteze mda mwingi
Ya ngoswe mtuachie ngoswe.
Tangu lini fisi akakataa nyama, busy unamkabidhi bucha?
Wanaume wengi wanyama, japo hodari wakuficha makucha,
Hata akishiba hakati nyama, tena anaifata mawindoni kucha
kirahisi rahisi umpelekee nyama, atakavoiparamia sipati picha.
Ya ngoswe mtuachie ngoswe.
Mwanaume hatongozwi anatekwa, kama kumvuta kuku bandani
Wamlegezea jicho lege lege kutwa, wamkaribisha kwako ndani
Wamgusagusa kimakosa kutwa, wajielezea wema wako wa ndani
Unamkirimia kama wako mpwa, ilihali mmekutana tu kibandani
Ya ngoswe mtuachie ngoswe.
Kiuno wamplegezea na kalio pia. Mwanamke si gogo la mnazi.
Mkitembea wamuwahi kumtangulia, kalio wamtikisia rahisi si kazi
Ukipika waepuka vitu kuungulia, wamkoleza kwakuti pia nazi
Wamsahaulisha wote waliotangulia, nakujisiti kwa stadha ya mavazi
Ya ngoswe mtuachie ngoswe
naona mzee unahamasisha tutongozwe
Mbona tayari wanatongozanamtaanza kutongozana wanawake kwa wanawake sasa..endeleeni na ujasiri
Loohh!! Utanifanya niwe dhaifu nitoe talaka. Maneno yako yananichimba mpaka ndani ya moyo wangu.
Sasa itakuwa kila unapoguswa na maneno unatoa talaka.... hata mie utanitwanga talaka.
majanga haya sasaUmeona eeeeh!!! loh! ngoja tuanze na yeye mwenyewe.....duh mbona pozi limeniisha? kwa mfano unaanzaje??? huyu atasema na mahari tuwalipie.
Ukweli umebainika kwenye roho yangu kwamba wewe ni No.1 No one like you. Bila shaka wewe utakuwa kigoma mwisho wa reli. Ukweli nimetembea Zanzibar, Tanganyika yote sijawahi kupenda kama nikupendavyo wewe. Naamini wewe ni zawaadi yangu toka juu. Usiogope mpenzi, sitokutenda.
Kama kuwa mwanamke jasiri ni kutongoza basi nitunukiwe cheti cha ujasiri....