Mwanamke hataki maelewano

Mwanamke hataki maelewano

Commander Dalton

Senior Member
Joined
Feb 10, 2018
Posts
198
Reaction score
264
Habari zenu wakuu.

Ni miezi sasa nipo na huyu binti kwenye mahusiano, ikatokea kwenye kurupushani za kwichi kwichi akapata mimba, akaniuliza utailea? Nikasema yes nitailea usitoe, basi nikaanza kuilea kidogo kidogo mpaka sasa ina miezi mitatu.

Kilichonifanya niandike post hii ni kutaka ushauri kwa lifuatalo.

Siku chache zilizopita uchumi wangu haukuwa sawa, kwa hiyo alipohitaji kitu sikuweza kumpa kwa muda huo, hiyo hali ikaendelea hivyo akawa anabadilika akisikia kuwa sina, ilipofika mahali akaniambia ataitoa mimba kwa kuwa siihudumii, hapa alifikia kuniambia kuwa sina tofauti na mtu aliyeikataa mimba( Hapa nilistaajabu kwa kuwa nimekubali na nimemhudumia kwa kipindi fulani). Tulipofika hapo nikamuambia ok itoe tu maana niliona hana shukurani, nikakata mawasiliano.

Baada ya wiki akanitafuta anahitaji mawasiliano na mimi nikamuambia nakusikiliza, akasema anahitaji tuwe kama zamani nikamuuliza mimba umetoa akasema hapana, nikamwambia hakuna shida( hapa nikiri udhaifu wangu kwa kuwa namhitaji mtoto) ikabidi nikubali.

Sasa basi juzi hii ninapiga simu mchana kutwa hapokei na message hajibu kupatikana usiku nikamuuliza ulikuwa wapi akasema nilikuwa kwenye semina ninamtafutia mtoto mahitaji madogo, nikamuuliza yapi? Akasema hawezi kuniambia kwa kuwa sina hela! Kumuuliza zaidi akaanza kuwaka, kuona hivyo nikamuambia usijali sitakusumbua maana naona uko busy sana, akasema sawa! Baada ya muda akanitumia sms akisema nimemkana mtoto nitamtafuta tu kuwa damu ni nzito kuliko maji, wakati kiuhalisia sijaikana mimba wala kuitilia shaka, ila ni kama ananishurutisha niikane.

Sasa anachukulia udhaifu wangu wa kukosa hela kwa kipindi kifupi kunipelekesha kwa kuwa namhitaji mtoto mtarajiwa, ukizingatia kwamba hajui kuomba kitu kwa ustaarabu na kauli zake ninachoka kabisa niamue nini.

Ushauri wenu wakuu.

Samahani kwa gazeti.
 
Braza kwanza inaonyesha bado hamna uzoefu kwenye hizo mambo!!
Huyo mdada anayoyafanya unaweza kukuta ni sababu ya huo ujauzito, mimba inabadilisha tabia za wanawake! Kuna ambao wakiwa wajawazito hawataki kbs kumuona mume wa ndoa, kwa hiyo weka uvumilivu mbele, akishajifungua kisirani chote kitaisha!!
 
Sawa sawa mkuu
 
Pole sana mkuu.
Ndio maana huwa tunashauriwa tuwe makini sana na wanawake tunaotaka kuzaa nao.

Huo ni msalaba wako, beba tu.
 
Hahahah washenzi wa namna hii kumbe wengi Sana... Je alikwambia tu anamimba au mulienda kushuhudia vipimo? Unaweza kuta hana kitu amejua unapenda watoto akakuchezea mchezo.... Hawa viumbe wanaakili Sana...
 
Nilimpima mwenyewe.
 
dizaini na wewe hujielewi..... kuna mahali umesema ulimruhusu kutoa, ukakata mawasiliano, hiyo ndio ilikuwa best option ? japokuwa mwanamke ana kiburi ?
 
Wakati mwingine ni hormones tuu zinampelekesha.Usikate tamaa mkaka,wakati wa ujauzito kuna mabadiliko mengi hutokea.
Wengine huchukia wenzi wao or aina fulan ya chakula or harufu.Kikubwa uvumilivu
 
Nilimpima mwenyewe.
Basi vumilia mkuu labda nihali ya ujauzito kama mwanzo hakuonyesha hiyo tabia kabla ya ujauzito. Jengine nililoliona jitahidi Sana kutafuta PESA umridhishe huyo mwanamke mana yaonyesha kitoto kilicho tumboni kinapenda harufu ya PESA...
 
Inaonesha ni kiasi ilivyokuwa we bado ni mdogo kifikra. Maisha yote tambua kuwa mtoto hagombaniwi, iko siku atakuwa na itaitafut damu yake(baba yake wa kweli) hata kama aliaminishwa mtu mwingine kuwa ndie baba yake.
Tulia fanya mambo yako mengine.
 
Wewe tafuta pesa tu haya yote yataisha
 
dizaini na wewe hujielewi..... kuna mahali umesema ulimruhusu kutoa, ukakata mawasiliano, hiyo ndio ilikuwa best option ? japokuwa mwanamke ana kiburi ?
Kuna muda unaweza kukasirishwa ukaamua kutoa uamuzi ambao hata wewe mwenyewe haukupendezi
 
Inaonesha ni kiasi ilivyokuwa we bado ni mdogo kifikra. Maisha yote tambua kuwa mtoto hagombaniwi, iko siku atakuwa na itaitafut damu yake(baba yake wa kweli) hata kama aliaminishwa mtu mwingine kuwa ndie baba yake.
Tulia fanya mambo yako mengine.
Asante mkuu
 
Pole sana...

Jaribu kumuelewa na kumsikiliza...

Unaweza dhani anafanya kusudi kumbe...

Labda mimba inampelekesha na kumfanya awe hivyo...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom