Mwanamke amuua mwanae ili aolewe

Mwanamke amuua mwanae ili aolewe

ya
Msichana wa miaka 17 mkazi wa Makete mkoani Njombe Vumilia Kyando ambaye ni muhudumu wa baa amemnyonga na kumtumbukiza kwenye mto mtoto wake wa kumzaa John Kyando mwenye miaka miwili baada ya kupata mchumba ambaye si baba wa mtoto huyo aliyetaka kuishi nae lakini akawa hamtaki mtoto huyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Njombe Kamishna Masidizi wa Polisi Podinsiana Protas ameiambia ITV kuwa Vumilia Kyando aliamua kumuua mwanaye wa kumzaa baada ya kumpata mwanaume aliyetaka kuishi nae lakini akawa hamtaki mtoto wa msichana huyo.

Kamanda Podinsiana Protas amesemna kuwa mwanamke huyo anahojiwa na polisi na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani huku wananchi mkoani Njombe wasikitishwa tukio hilo la mama kumuua mtoto wake wa kumzaa.

Katika tukio jingine mtoto wa miezi kumi na mbili Samweli Ahidimiwe ameuawa kwa kukatwa na jembe na Frola Sanga mkazi wa kijiji cha Kisaula wilayani Makete mkoani Njombe katika ugomvi wa kugombea mashamba ambapo Frola Sanga alikuwa akitaka kumkata kwa jembe bibi wa mtoto huyo Tulamba Konga ndipo akamuua kwa jembe mtoto huyo aliyebebwa mgongoni na bibi yake.

Upelelezi utapokamilika mtuhumiwa Frola Sanga atafikishwa mahakamani kwa kesi ya mauaji ya mtoto Ahimidiwe Sanga.
ni hawa wanawake sijui wanapatagwa na nini yan!
 
Vumilia ulivumilia yanini kulea mimba kwa miezi 9 kisha mwana kwa miaka 2, halafu ukaamu kwa muda mfupi kumuua mwanao ambae hujui baadae angekufaa kwa kiasi gani ktk maisha yako? Mwanaume wa maisha yako au ambae anahitaji kujenga familia anaweza kukataa mtoto? Kuua mtoto sio kutoa mimba Vumilia, utavumilia mengi gerezani Vumilia.
 
Nadhani hata shetani hua anashangaa sana manake kuna watu sasa wanamzidi hata yeye uwezo apa apa bongo!
 
Ningekuwa karibu na huyo dada ningempiga vibao,nimeshikwa na hasira sana.
Mwanaume asiyempenda mwanao ni dhahiri hawezi kukupenda na wewe.
Nae alivyo mjinga akamuua mwanae ambaye hakuna mwanamke yeyote chini ya jua angeweza kumtenganisha naye tofauti na huyo mwanaume wa kupita,leo yuko nae kesho akipata mwingine atamuacha.
Basi msamehe mamii,mbona hata wew ni mosaji tu au vipi?makosa unafanya kila dakika.
 
Huyo mwanamme kampenda yeye na si mtt aliezaa na mwanamme mwingine! Anaona ktk maisha yake bado anayo nafas ya kuolewa.
 
Back
Top Bottom