Mwanamke amuua mwanae ili aolewe

Mwanamke amuua mwanae ili aolewe

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,692
Reaction score
59,195
Msichana wa miaka 17 mkazi wa Makete mkoani Njombe Vumilia Kyando ambaye ni muhudumu wa baa amemnyonga na kumtumbukiza kwenye mto mtoto wake wa kumzaa John Kyando mwenye miaka miwili baada ya kupata mchumba ambaye si baba wa mtoto huyo aliyetaka kuishi nae lakini akawa hamtaki mtoto huyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Njombe Kamishna Masidizi wa Polisi Podinsiana Protas ameiambia ITV kuwa Vumilia Kyando aliamua kumuua mwanaye wa kumzaa baada ya kumpata mwanaume aliyetaka kuishi nae lakini akawa hamtaki mtoto wa msichana huyo.

Kamanda Podinsiana Protas amesemna kuwa mwanamke huyo anahojiwa na polisi na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani huku wananchi mkoani Njombe wasikitishwa tukio hilo la mama kumuua mtoto wake wa kumzaa.

Katika tukio jingine mtoto wa miezi kumi na mbili Samweli Ahidimiwe ameuawa kwa kukatwa na jembe na Frola Sanga mkazi wa kijiji cha Kisaula wilayani Makete mkoani Njombe katika ugomvi wa kugombea mashamba ambapo Frola Sanga alikuwa akitaka kumkata kwa jembe bibi wa mtoto huyo Tulamba Konga ndipo akamuua kwa jembe mtoto huyo aliyebebwa mgongoni na bibi yake.

Upelelezi utapokamilika mtuhumiwa Frola Sanga atafikishwa mahakamani kwa kesi ya mauaji ya mtoto Ahimidiwe Sanga.
 
Siku hiz bhana wanawake hakuna , wanawake ilikua ni mama zetu walioolewa na baba zetu. Ila kwa sasa ni upuuz mtupu.. Eri unaua mtoto kisa umepata basha mpya... Kweli tumekua zaid ya wanyama...
Wallah mtu aliefanya kitendo kama hicho hata ukimuoa anawe akakuwekea sumu mana kashakua na roho ya mauti
 
Upuzi mwingine ukakera na kuumiza
Kitoto hakijui lolote
Du!
 
ooooooooooops! watu wanalilia ndoa hadi wanadiriki kufanya dhambi ya mauaji!
 
Si bora angemtelekeza hata kanisani au msikitini watu wamuokote. Hivi kwa nini watu wamekosa hofu ya Mungu?
 
Wanaume wa kuoa wachache binti hakutaka kupoteza fursa hahahaa
 
Huyo mwanaume hakumpenda km angempenda acngempa masharti ya kukataa kuishi na mwanae....huyo mwanaume nae akamatwe ahojiwe...!!
 
aisee duniani kuna mammbo na watu wanamhitaji Mungu unatoa kiumbe cha Mungu kisa ndoa ambayo hujui kama itakuwapo au itadumu nawe
 
Huyo ataweyuka kwa nafsi ya mwanae asiekuwa na hatia kwani nafsi itamsuta kila wakati time will tell, ooh poor soul
 
Hivi hawa wanawake wanapata wapi roho mbaya kiasi kiasi hiki?R.I.P mtoto usie na hatia
 
Huyo ni mgonjwa wa akili. Yani mtoto umemkuza mpaka amefika miaka miwili Afu unamuua kisa ndoa
 
Ningekuwa karibu na huyo dada ningempiga vibao,nimeshikwa na hasira sana.
Mwanaume asiyempenda mwanao ni dhahiri hawezi kukupenda na wewe.
Nae alivyo mjinga akamuua mwanae ambaye hakuna mwanamke yeyote chini ya jua angeweza kumtenganisha naye tofauti na huyo mwanaume wa kupita,leo yuko nae kesho akipata mwingine atamuacha.
 
wanawake ni viumbe dhaifu sana nimeamini
so akizalishwa na kuachwa na huyu mpya aliyempata kisha akapata mtu mwingine ataua tena,hizi roho mbaya za wanawake hata shetani anawashangaa
 
Back
Top Bottom