Mwanamke amenisaliti

Mwanamke amenisaliti

Kweli anatunga story anashindwa kuweka mtiririko kuficha uongo wake.
stori yako inatia mashaka, manake mtu mwenye mumewe umeishi nae kipindi chote hicho mpaka anajifungua huyo mumewe alikuwa wapi? au walikuwa wametengana? na kwa maelezo yako wakati mnaanzi mahusiano hiyo 2013 wewe ulikuwa na miaka 22 sasa yeye atakuwa na miaka mingapi? na pia umesema mwaka 2014 ndo alipata ujauzito, sasa nikipiga mahesabu huu ndo kwanza mwenzi wa 9 sasa wewe unasema mtoto alishazaliwa na ana miezi 4, kwa kweli nimeshindwa kukupata
 
endelea na maisha yako mtoto akikua atamfata baba.... ila kama mama akimwambia....
 
Habari wapendwa
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 23.
Mnamo mwaka 2013 mwezi wa 9 nilianza mahusiano ya mapenzi na msichana wa kikwere mixer na mlugulu; Ilipofika mwaka 2014 aliniambia kuwa ana ujauzito wangu.
Nilikataa akasema lengo langu ni kuzaa na wewe? Nilikataa kutokana na hali yangu ya maisha sio nzuri.

Akaniambia" usijali mimi nitajihudumia mwenyewe, niliamini hivyo kutokana na hali nzuri ya maisha aliyokuwa nayo.
Tukaendelea hivyo siku zote nikampeleka kwetu wazazi wangu wakamfahamu.

Tuliishi wote wakati wote mpaka akajifungua mtoto wa kike nilifurahi sana kwa mara ya kwanza kuitwa baba. Tukawa wote mpaka mtoto alipofikisha miezi minne.

"Mnamo siku ya jumamosi akaniaga anakwenda kwao kuna ngoma nilimruhusu kiroho safi ( kumbe sikujua ) ndio ikawa hivi?

Nikiwa natambua kuwa mwenzangu yuko kwao kwenye ngoma siku moja usiku nilipiga simu ikapokelewa na mwanaume ambaye alijitambulisha kama mume wake.

Sikuweza amini mpendwa nilikata simu kwa hasira.

Nikampigia simu tena akaniambia" mimi huyu ni mke wangu nimemuoa kwa ndoa nikamwambia mimi ni mzazi mwenzangu.

Mume wake akamwambia" aongee na mimi lakini yeye akakataa ila mume wake akaniambia" tuweke kikao juu ya hili.

Kikao kilitishwa yule mwanamke akauliza" mtoto ni wa nani? Akajibu mtoto niwa mume wake (unfaithful for me ) mimi niliondoka kwa sababu alikuwa tayari ameshanikana kumbe yule mwanamke alikuwa ameolewa tangu mwaka 2009 hakubahatika kupata mtoto.

Baada kikao kuisha akanipigia simu na kuniambia kuwa yule mtoto ni mwanangu nilikataa na nikamwambia"asinipigie simu tena mpaka sasa ananisumbua.

Ndugu zangu wapendwa nifanye nini?

Naombeni ushauri wenu

pole sana mkuu ndo ukubwa wenyew, japokua mwiba wa kujichoma hauna pole.
 
I'm sorry best for prove me wrong▶▶
Mnamo mwaka 2013 alipata ujauzito mwezi wa tisa

na huyo mume mwenzio alikuwa wapi kipindi choooote mlichokuwa na huyo dada? na ana umri gani?
 
Endelea na maisha yako usijiumize kichwa
 
Yaani uikatae mimba halafu ujifariji kuwa mwanamke anakupenda?????

Alikuwa anakulia timing tu akuumize kama ulivyomuumiza

Halafu umario mbaya ujue

Cha muhimu songa mbele
 
stori yako inatia mashaka, manake mtu mwenye mumewe umeishi nae kipindi chote hicho mpaka anajifungua huyo mumewe alikuwa wapi? au walikuwa wametengana? na kwa maelezo yako wakati mnaanzi mahusiano hiyo 2013 wewe ulikuwa na miaka 22 sasa yeye atakuwa na miaka mingapi? na pia umesema mwaka 2014 ndo alipata ujauzito, sasa nikipiga mahesabu huu ndo kwanza mwenzi wa 9 sasa wewe unasema mtoto alishazaliwa na ana miezi 4, kwa kweli nimeshindwa kukupata

c wewe tu mm ndo kabisaa hadith haieleweki hii
 
stori yako inatia mashaka, manake mtu mwenye mumewe umeishi nae kipindi chote hicho mpaka anajifungua huyo mumewe alikuwa wapi? au walikuwa wametengana? na kwa maelezo yako wakati mnaanzi mahusiano hiyo 2013 wewe ulikuwa na miaka 22 sasa yeye atakuwa na miaka mingapi? na pia umesema mwaka 2014 ndo alipata ujauzito, sasa nikipiga mahesabu huu ndo kwanza mwenzi wa 9 sasa wewe unasema mtoto alishazaliwa na ana miezi 4, kwa kweli nimeshindwa kukupata

Anatuzinguwa mtoaa madaa
 
Back
Top Bottom