Mwanamke alivyotaka kuharibu maisha yangu

Mwanamke alivyotaka kuharibu maisha yangu

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,793
Reaction score
5,053
Mapenzi yana raha yake pia yana karaha. Mapenzi ni asali pia ni sumu.

Mwaka 2017 nilikutana na mwanamke fulani shuleni, Nilimtongoza mwana dada huyo kwa bahati nzuri akakubali ombi langu.

Mapenzi yetu yakawa ya furaha saana mimi na huyo mwanamke nilimpenda saana na yeye akanipenda saana tukaamua kuwa sote tuache shule ili tutafute pesa za kuandaa harusi yetu na mambo mengine baada ya kuoana maana tulikuwa tunasomea tu lugha.

Yeye akapata kazi kwenye campany moja ya nyama hivi na mimi nikapata kazi kwenye campany ya kutengeneza biscuit. Huko kwenye campany ambayo huyo mwanamke alipata kazi rafiki yangu wa damu alikuwa anafanya kazi huko kwa hiyo nikampa kazi ya kumuangalia huyo shemeji yake mtarajiwa.

Baada ya siku kadhaa tabia ya mwanamke ikaanza kubadilika nikimpigia simu mara anadai anachoka saana akawa mtu wa sababu nyingi sana.

Siku moja niko zangu nyumbani nimetulia zangu, rafiki yangu mwingine akafika home kunipa habari kuwa alimuona yule demu wangu walikuwa restaurant fulani, Mimi nilichukulia poa nikajisemea moyoni mwangu ni mtu na shemeji yake.

Sasa kuna siku nilikuwa nakwenda zangu job nilivyoingia ndani ya bus nikamuona yule demu wangu na yule rafiki yangu wanapigana kiss. Hizi nchi za wenzetu kiss unaweza piga popote tu.

Mimi niliwaona wao hawakuniona
Maana walikuwa bize nikashindwa kwenda kazini niliamua kushuka ndani ya bus na kurudi nyumbani huku maswali ya kiwa mengi kichwani mwangu kwanini huyu ndugu yangu ananifanyia hivi!

Nilipata hasira saana nikamfuata jamaa nyumbani kwake jioni kufika kule tukaanza kubishana mimi katika kubishana kwetu nilichukua kiti nikampiga kichwani akazimia, sasa alivyokaba sauti yake majirani walisikia wakapigia polisi simu na polisi walifika ndani ya nyumba na kukuta nalia maana nilifikiri nimemua kwa sababu ya mapenzi kumbe alikuwa amezimia tu polisi walinibeba na kuniweka ndani
Na mimi niliona ni haki yangu kunyongwa tu.

Huyo rafiki yangu alipopona alikuja kunitetea kwa kusema kuwa sikukusudia ilikuwa bahati mbaya.

Kwa bahati nzuri walimsikiliza na kunitoa jamaa aliniomba msamaha kwa kunifanyia usaliti na mimi nilimuomba msamaha.

Kuweni makini na wanawake sio watu wa kuwamini sana wanaweza kukugombanisha na familia yako na kukutenganisha na ndugu na marafiki zako.
 
Siti ya kwanza maana naona wachangiaji wa hapo huu wotee wamesimaaaaa dede.

Nauliza tu mpooo nchi gani na huyo mpenzio
 
Hivi vitu huwaga havisound poa kama hujakumbana navyo. Waliopitia haya wanajua jinsi inavouma. We move lakini💪
 
Nilipata hasira saana nikamfuata jamaa nyumbani kwake jioni kufika kule tukaanza kubishana mimi katika kubishana kwetu nilichukua kiti nikampiga kichwani akazimia, sasa alivyokaba sauti yake majirani walisikia wakapigia polisi simu na polisi walifika ndani ya nyumba na kukuta nalia maana nilifikiri nimemua kwa sababu ya mapenzi kumbe alikuwa amezimia tu polisi walinibeba na kuniweka ndani
We2e ni mwanaume dhaifu sana. Anayetusaliti ni demu wako wswe badala uzunhumze naye unamuogopa unaend akumpiga kiti mwanaume mwenzio ambaye naye kamtongoza kama ylivyofanya wewe.

Kama mke wako anakusaliti then ukaenda kugombana na bwana wake mpya ina maana wewe ni Boya.
 
.
JamiiForums-629024192.gif
 
Mapenzi yana raha yake pia yana karaha. Mapenzi ni asali pia ni sumu.

Mwaka 2017 nilikutana na mwanamke fulani shuleni, Nilimtongoza mwana dada huyo kwa bahati nzuri akakubali ombi langu.

Mapenzi yetu yakawa ya furaha saana mimi na huyo mwanamke nilimpenda saana na yeye akanipenda saana tukaamua
Rudi Tanzania
 
Mapenzi yana raha yake pia yana karaha. Mapenzi ni asali pia ni sumu.

Mwaka 2017 nilikutana na mwanamke fulani shuleni, Nilimtongoza mwana dada huyo kwa bahati nzuri akakubali ombi langu.

Wewe ndo ulitaka kujiharibia maisha kwa kugombana na ndugu yako sababu ya mwanamke. Usimsingizie.
 
Back
Top Bottom