Mwanamke akipenda anapenda kweli!

Mwanamke akipenda anapenda kweli!

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,681
Mwanamke akikupenda anakuwa na furaha, anakuwa anajivunia kuwa na wewe, na hujihisi furaha kuongea na wewe.
Hupenda awe rafiki wa rafiki zako na ndugu zako, uvipendavyo na yeye atavipenda, atabadilisha mtindo wake wa maisha kuendana na mtindo wako.
Haitajalisha ni kiasi gani utamuudhi, atakusamehe hata kabla hujamuomba msamaha, atachokifanya ni kusubiri tu umuombe msamaha kuthibitisha kama kweli umejutia kosa lako.
Atajaribu kuwa na wivu na atakulinda kwani atahitaji uwe wake, wake peke yake na sio ku share. Atawakataa wengine wote wanaomtongoza kwa sababu ameona kesho yake ipo mikononi mwako.
Haitajalisha ni kiasi gani uko mbali na yeye, atajilinda kwa ajili yako. Atalike na ku comment kila kitu unachoweka facebook hata kama ni cha kipuuzi (hahaahaa).
Atakujibu kwa wakati text zako either watsapp, za kawaida au inbox ya fb. Hatajali kama unampa pesa au laa, kama ni tajiri au laa kwa sababu lengo lake ni kujenga maisha na wewe na sio kupass time ameona potentials kwako.
Atakuonyesha marafiki zake na ndugu zake, kwa sababu anajivunia kuwa mpenzi wako.
Tafadhali sana, muangalie mwanamke huyo, moyo wake umejawa na mapenzi, anastahili kutunzwa na kupendwa kama almasi.
Lakini tatizo kubwa la hawa "wavulana" (baadhi yao) baada ya kumfanya akupende zaidi, baada ya kupoteza muda wake juu yako, baada ya kuwakataa wanaume wengine ambapo kimsingi wengine walikuwa tayari kumuoa, baada ya kumuacha akutambulishe kwa ndugu zake na marafiki sasa unamuacha, unamkataa kwa mbwembwe nyingi, unamuacha akiwa na maumivu na aibu kubwa kwamba atawaambia nini wazazi wake, ndugu na marafiki, atatambulisha wangapi?
Na akiulizwa yuko wapi yule uliyetutambulisha? Awajibu nini!? Ofcoz atakachofanya ni kuinamisha kichwa huku ameshika mashavu! Hana jibu ni aibu na maumivu makubwa kwa kuwa alikupenda kwa dhati.
Mbona mnawaweka katika wakati mgumu wanawake waliopewa moyo wa kupenda?
Brothers, usimfanye mwanamke wako ajute kwanini alipenda, usifanye wengine wamcheke na kumdhihaki. Timiza ahadi yako, kama amekukosea na kukuomba msamaha jaribu kumpa nafasi ya pili. Kila mtu anahitaji nafasi ya pili ili aweze kurekebisha pale alipokosea.
Samehe
 
vp akipoteza na hyo nafasi ya pili na ya tatu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda kama unazungumzia wanawake aina ya Mrs.Jiwe lakini sio tubinti twa siku hizi za mwisho! Hutu ukiona amekupenda kweli ujue na wewe una hela kweli!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesema kweli.. ila hawa wa leo!! sijui wa keshokutwa watakuwaje tu
 
Back
Top Bottom