kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,784
- 20,155
Jeshi la utawala wa Kizayuni limemfukuza mwanajeshi mmoja aliyekataa kumpiga risasi binti wa Kipalestina aliye na umri wa miaka 16 kwa jina la Nauf Infiat.
Katika tukio hilo ambalo lilijiri mwanzoni mwa mwezi huu katika lango la kuingilia katika kitongoji cha Wazayuni kwa jina la Mevou Dotan huko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, mwanajeshi huyo wa Kizayuni aliyefukuzwa jeshini hakuwa tayari kummiminia risasi binti huyo wa Kipalestina, ambapo mwanajeshi mwingine alimpiga risasi binti huyo na kumjeruhi vikali na hatimaye binti huyo kuaga dunia siku moja baadaye.
Baada ya kumchunguza mwanajeshi huyo aliyekataa kumpiga risasi binti wa Kipalestina, jeshi la Israel lilisema kuwa mwanajeshi huyo hakuonyesha radiamali inayofaa mkabala na binti huyo wa Kipalestina. Jeshi hilo limedai kuwa, binti huyo wa Kipalestina alikuwa na lengo la kumshambulia mwanajeshi Mzayuni katika lango la kuingilia katika kitongoji cha walowezi wa Kiyahudi cha Mevo Dotan. Hadi kufikia sasa, Wapalestina zaidi ya 300 wameuawa shahidi na wengine wengi wametiwa mbaroni na wanajeshi wa Israel tangu kuanza Intifadha ya Quds mwezi Oktoba mwaka 2015.
Parstoday.com