Mwanahabari Manyerere Jackton akiri kwa mchakato wa maoni CCM uligubikwa na rushwa

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
889
Reaction score
2,863
Wakuu

Akizungumza alipokuwa katika mahojiano kwenye kipindi cha Medani Kuu na Edwin Odemba alisema:

“Nilishindwa Uchaguzi ndani ya CCM kwenye kura za maoni 2025 katika Jimbo la Butiama kwa kuwa sikutoa Pesa wenzangu walitoa"

Hiki alichokisema Comred Manyerere, nami nilikutana nacho ile 2020, na nikapigwa chini, na nikaeleza kitu humu GE2020 - Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!
P
 
dear friends, ladies and gentlemen,
elections are very expensive processes in nature, tumejifunza haya masomoni jamani,

yaan kweli unaenda kushiriki mchakato wa uchaguzi bila kujiandaa na kujiimarisha kiuchumi?:pedroP:

niliwahi kushiriki uchaguzi nikiwa na laki5 pekee, nikajifunza mengi sana na nikapata uzoefu mkubwa mno ulionifanya kujipanga vizuri sana chaguzi zilizofuata na hatimae hakuna stress tena.

halafu,
kuanza na kujitumbukiza kichwakichwa kwenye siasa at age of 50, is dangerous to your health and life at large.
 
Hiki alichokisema Comred Manyerere, nami nilikutana nacho ile 2020, na nikapigwa chini, na nikaeleza kitu humu GE2020 - Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!
P
Mwalimu Paskali,
kura 1 muhimu sana uloipata kwenye uchaguzi ule,
ilifaa uigeuze na kua fursa muhimu sana ya kujifunza, kujisahihisha, kujiimarisha, kujipanga upya ili hatimae kupata kura nyingi zaidi kwenye chaguzi nyingine zilizofuata.
 
Ni kweli, kitu cha kwanza nilichofanya ni kushukuru kwa hicho kidogo nilichopata.

Kitu cha pili ni kukubali matokeo, kuwa japo CCM ni chama cha siasa, na chama cha siasa ni mali ya wanachama, hao wanachama hawafani, kuna wanachama ambao ni wanachama tuu, kuna wanachama ambao ni wakuja tuu, na kuna wanachama ambao wao ndio wenyewe wenye chama chao na kujifunza ili mtu ushinde kura za maoni CCM, ni lazima uwaone hao wenyewe wenye chama chao!, mimi sikumuona mtu yoyote na matokeo yake ndio ile kura moja

Hivyo nilipaswa kujipanga upya, ili uchaguzi unaofuata, nitupe tena karata yangu nikiwa nimejipanga nikiwa kamili gado.

Kwa vile ni wale CCM wa Nyerere type, hatuko tayari kufanya hizo mambo, hivyo nikakubali matokeo na kujikalia pembeni kwa kuendelea kulitumikia taifa katika maeneo mengine.

P.
 
naweza kuelewa mtazamo wako na kukubaliana nawe kwa kiasi,
lakini hapo ulipoeleza kwamba ili ushinde kura za maoni CCM ni lazima uwaone wenyewe hao wenye chama chao, nao sio sahihi. mimi sikua na chochote na sina chochote cha kuwaoffer wajumbe ispokua utumishi na uongozi uliotukuka. kata zaidi ya 25, wajumbe zaidi ya 1000 ni vigumu mno kuwin sapoti yao wote. ni kuchagua sapoti ya kundi moja au mawili miongoni mwao.

binafsi wakati naomba ridhaa ya wana ccm katika nafasi ya ubunge kwa mara ya kwanza, nilikua simfahamu kiongozi yoyote wa ccm, hata mwenyekiti wa ccm kwenye tawi langu tu kule kijijini, japo nilikua nayafahamu karibu matawi yote jimboni kwangu baada ya kutamani kuomba nafasi hiyo.

Na sikua mjumbe wala kiongozi wa ngazi yoyote wa ccm kote nchini nilipokua naishi, na kwahivyo sikua nawafahamu hao unaodai ndio wenye chama chao. Mimi nimethibitisha mwenyewe pasina shaka yoyote kwamba, mwanachama yeyote wa ccm anaethubutu kwa chochote ndani ya CCM, anaweza kupata fursa anayoitaka bila mbambamba za ambao wanatisha wengine kwa dhana hiyo ya kwamba chama kina wenyewe.
Chama ni cha kwetu sote.

Leo hii mathalani,
napigiwa cm na kupata messages kutoka kwa wanachama na viongozi mpaka nacheka mwenyewe, nakujiuliza hivi kulikoni? kwamba hawa watu mbona wakati natia nia mara ya kwanza na hata ya pili hawakunifahamu hivi, kulikoni leo? sikukata tamaa na sintakata tamaa hata iweje:pedroP:

Kura yako 1 ilipaswa kua utambulisho wako muhimu sana mwalimu Paskali,
kwasababu ungerudi mara ya pili ungewauliza wajumbe ni nani asiekujua? na kwa majigambo zaidi hata kujitambulisha kwako kulifaa kua mimi ndie yule wa kura moja kura za maoni za ubunge2020.

Nashauri ikiwa utaona inafaa kwamba,
Kuna uchaguzi wa ndani ya chama mwaka ujao,
tafadhali,
ikikupendeza,
usiache kuomba nafasi yoyote ya uongozi uipendayo kwenye chama chako,
hata kua mjumbe tu wa kamati ya siasa ya tawi tu. Nina hakika utapata mwanga na fursa zaidi ya kuona namna bora ya kupenyeza mawazo, mapendekezo na maoni yako ambayo daima huwa ni mazuri tu, lakini pia kupata fursa ya kushauri namna bora ya kuimarisha demokrasia ndani ya ccm.

hakuna sababu ya kujiweka pembeni bali kupambana na kuhakikisha kwamba fursa zilizopo ndani ya vyama vya siasa zinapambaniwa kwa usawa, uwazi na haki, lakini dhana za kua eti chama fulani kina wenyewe zinafutika kwenye fikra za wanachama wa chama husika.
vyama vya siasa ni mali ya umma na wanachama wake wote.
 
Mkuu asante sana kwa ushauri huu, na siku ukilisikia jina langu nimejaribu kutia nia popote,ujue ni wewe ndio umenitia moyo,mimi niliisha jikatia tamaa zamani, unenihamasisha sana na kunitia moyo, hivyo 2027 narejea.
Asante sana kwa ushauri wako,kiukweli kuna watu ndani ya CCM,kazi yao ni kutisha wengine, kumbe vingine ni vitisho tuu!.
P
 
Ni kweli, kitu cha kwanza nilichofanya ni kushukuru kwa hicho kidogo nilichopata.

Kitu cha pili ni kukubali matokeo, kuwa japo CCM ni chama cha siasa, na chama cha siasa ni mali ya wanachama, hao wanachama hawafani, kuna wanachama ambao ni wanachama tuu, kuna wanachama ambao ni wakuja tuu, na kuna wanachama ambao wao ndio wenyewe wenye chama chao na kujifunza ili mtu ushinde kura za maoni CCM, ni lazima uwaone hao wenyewe wenye chama chao!, mimi sikumuona mtu yoyote na matokeo yake ndio ile kura moja

Hivyo nilipaswa kujipanga upya, ili uchaguzi unaofuata, nitupe tena karata yangu nikiwa nimejipanga nikiwa kamili gado.

Kwa vile ni wale CCM wa Nyerere type, hatuko tayari kufanya hizo mambo, hivyo nikakubali matokeo na kujikalia pembeni kwa kuendelea kulitumikia taifa katika maeneo mengine.

P.
Ina maana ulipata kura yako tu
 
Mkuu asante sana kwa ushauri huu, na siku ukilisikia jina langu nimejaribu kutia nia popote,ujue ni wewe ndio umenitia moyo,mimi niliisha jikatia tamaa zamani, unenihamasisha sana na kunitia moyo, hivyo 2027 narejea.
Asante sana kwa ushauri wako,kiukweli kuna watu ndani ya CCM,kazi yao ni kutisha wengine, kumbe vingine ni vitisho tuu!.
P
Mimi nakuhakikishia hutopita mpaka uwaone wenye Chama Chao usisikilize maneno ya motivational speaker ukajitia moyo mwisho wa siku utajitia kitanzi solution ni mbili tu either uwaone wenye Chama Chao uzuzngumze nao vizuri Au andaa pesa ya kutosha CCM ni Chama cha wala rushwa
Mambo ya kiswahili kukaa tunadanganyana hapa na hali yakua ukweli tunaujua yameshapitwa na wakati

Naomba nikuvunje moyo tena HUTOPITA Mpaka uwaone wazee na uende na hela kama una masikio umeniskia
 
Back
Top Bottom