Mwanafunzi wa IFM apigwa risasi 4 na mtu anayesadikiwa kuwa ni askari

Kwanini aliitiwa mwizi na kupigiwa kelele. ...Kwanini hakujisalimisha?
Uwe unasoma habari yote kwa makini sio kuuliza maswali ya kijinga hivo kwenye blog makini kama JF. Kama hujui kusoma kauze ubuyu mitaani. Unauliza swali wakati jibu lipo ndani ya habari!
 
Sasa sinza kafata nini tabata? Nyie ndo majambaz tunao watafta..hata wanafunz pia n majambazi tu
Wewe nawe una akili ya kuazimwa, umeambiwa katoka kwenye sherehe ya birthday, sasa ajabu iko wapi hapo!
 
Watu wengi wanaochangia mada hawajasoma hata habari yenyewe manake wanaongea vitu tofauti na habari yenyewe.
Aisee watz wengi wana akili kwenye makalio mkui, yaani comments nyingi watu hawajui undani wa mada kabisa
 
Uwe unasoma habari yote kwa makini sio kuuliza maswali ya kijinga hivo kwenye blog makini kama JF. Kama hujui kusoma kauze ubuyu mitaani. Unauliza swali wakati jibu lipo ndani ya habari!
Ngekuwepo mm ngemtia midoleee kwenye matundu ya hzo risasi..... tunataka komesha ujambaz dsm kabsaaa
 
Tuwaachie polisi wafanye uchunguzi wao. Tusihukumu kwamba yeye sio jambazi wala aliemuua ni polisi. Chanzo halisi cha kupigwa risasi hujakieleza
Watu wanaonywa wasijichukulie sheria mikononi hata hawasikii jamani. Binadamu wanafanya dunia hii iwe mbaya!
 
Hivi bado kuna watu wana muda kabisa wa kuhudhuria hizo tafrija za ubatizo na kuzaliwa. Tena mwanaume kabisa unafunga na safari.
Kweli safari bado ndefu, tena na Tanzania hii ya Viwanja
Zaidi nimpe pole kwa kugongwa risasi.
Unajua uhusiano wake na huyo mwenye Birthday? Aidha kuna ubaya gani kuhudhuria hizo sherehe? Hao waliojichukulia sheria mkononi ndio wa kushikwa. Tena washikwe wote pamoja na mlinzi na hao watu wasiojua hata kutumia psycholojia kidogo! mtu kajisalimisha unampiga tu ha[pata say no to mob justice as it is un-justice!
 
Tanzania kila kitu HEWA tu hata wezi hewa wapo, wanafunzi hewa nao wapo. IFM nao hewa. Alitokapi usiku huo peke yake tena kwa miguu. Tabata hadi Sinza kwa miguuu! Dah! Kazi ipo
Familia yake nyingine ipo tabata, na sehemu aliyokulia
 
Unajua uhusiano wake na huyo mwenye Birthday? Aidha kuna ubaya gani kuhudhuria hizo sherehe? Hao waliojichukulia sheria mkononi ndio wa kushikwa. Tena washikwe wote pamoja na mlinzi na hao watu wasiojua hata kutumia psycholojia kidogo! mtu kajisalimisha unampiga tu ha[pata say no to mob justice as it is un-justice!
Kama alikua na uhusiano naye alishindwa nini hakulala kwake, aamue kuondoka usiku wa manane? Kutoka Tabata kuitafuta Sinza tena kwa miguu, inaingia akilini hii?
 
Namfahamu huyu kijana, sio jambazi wala mwizi ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu kozi ya Information Technology na sio wa pili kama mleta uzi alivyosema tena ni mtiifu na ni kiongozi hapo IFM, ana shughuli za kijasiriamali zinazohusiana na IT na pia anaimba muziki wa hiphop anatumia jina la Cyclonic, Nyumbani kwao ni tabata na pia ndipo alipokulia maisha yake yote, ila kwa kipindi cha karibuni amekua akiishi na dada yake maeneo ya sinza
Huyo askari ambaye hajulikani ni wa Jeshi gani kamrudisha nyuma sana kijana kwa maana ana mtihani wa kurudia tarehe 16 September ili aweze kumaliza chuo mwishoni mwa mwaka huu
 
Kwa mujibu comments za baadhi wachangiaji wa mada hii humu nimegundua watanzania wengi wana akili za mwendo Kasi. Wanaongeaongea tu hata hawajui sheria na haki za binadamu zikoje. Kama IQ za watu wengi ziko low hivi, basi hili taifa ni jipu.
 
mwizi anauwawa afrika kwasababu usipomuua kesho atakuja kuiba tena na ukimpeleka polisi wanamuachia

Sio enough reason ya kuua, na unavyo~support unaprove point yangu. Kesho atakuja kuiba tena kasema nani? We ulishuhudia mwizi yupi kakamatwa kua kaiba akaenda akaachiwa kesho yake? Mi nilioona wote wanafungwa, hakuna sababu hata moja ya kumuua binadamu mwenzako tena kwa kumshambulia na mawe, wengine wanachoma moto kabisa, ndiyo matatizo kama haya yanajitokeza, unakuta mtu alikua hana hatia lakini wajinga kutokuuliza wanaanza tu kupiga, hii sio mara ya kwanza tunasikia mtu kauliwa ki-bahati mbaya, na mwanza waliua mtu ambaye alisakiziwa na mwenzake mwenye chuki binafsi. Watanzania wengine naona bado iq zinafukuzana na za nyani. Nje kila siku watu wanatuambia nchi za Afrika hazina amani tunajifanya kutetea, ila ukweli uko palepale, nchi kama Tanzania ni ya hatari mno.
 
Kama Wenzie walimuitia Kelele za Mwizi hata kama ni utani hakusimama kuashiria ni utani Polisi alitumia Weledi kumpiga risasi za Miguuni na walipogundua sio pia wakawahi kumpeleka hospitali.

Matumizi ya silaha kwa askari yanamasharti yake. Kama huyu mtu alikuwa hakimbii na wala hajaresist arrest huwezi kumpiga risasi. Kwa maelezo hapo juu mlinzi alikuwa anampiga maana yake alishadhibitiwa hakuna ground ya mupiga risasi kwa kuwa hakuwa tishio kwa askari wala watu waliokuwepo.
 
Acha uchunguzi ufanyike.,maana kama kuna chumvi fulani za jazba.
Maana kuwa mwanafunzi sio kigezo.
Achatusubirie taarifa kamili,maana kama alikuwa amethibitiwa na watu wote hao,halafu from no wea mtu aje tu amimine risasi,basi naamini hata wale waliomtia mikononi mwanzo wangeona jamaa ni chizi.Kuna sababu hapo kwenye tukio zima.
Maana alieibuka usiku na kuita mwizi labda alikuwa anaota.
 
Matumizi ya silaha kwa askari yanamasharti yake. Kama huyu mtu alikuwa hakimbii na wala hajaresist arrest huwezi kumpiga risasi. Kwa maelezo hapo juu mlinzi alikuwa anampiga maana yake alishadhibitiwa hakuna ground ya mupiga risasi kwa kuwa hakuwa tishio kwa askari wala watu waliokuwepo.
kaka hawa jamaa wanaoshabikia matumizi haya ya nguvu kuzidi kiasi kamwe hawawezi kukuelewa katika issue kama hii nzito
 
Back
Top Bottom