Mwanafunzi wa DRC auawa India

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Masunda Kitada Oliver alipigwa hadi kufariki na kundi moja la wanaume wa Kihindi Ijumaa iliopita baada ya majibizano mjini Delhi. Watu wawili wamekamatwa kufuatia kisa hicho

160525120633_drc_student_kiliing_512x288_bbc_nocredit.jpg

Wanafunzi kutoka Afrika wakifanya maandamano nchini India

Balozi hizo zimesema kuwa hazitaki kushiriki katika kuadhimisha siku ya Afrika siku ya Alhamisi kufuatia misururu ya mashambulizi dhidi ya wanafunzi kutoka Afrika.

''Hii ni kwa sababu jamii ya Kiafrika nchini india ,wakiwemo wanafunzi wanaendelea kuomboleza kuwaenzi wanafunzi wa Afrika waliouawa akiwemo bwana Oliver,alisema Alem Tsehage Woldremariam'',kiongozi wa mabalozi wa Afrika nchini India.

Mnamo mwezi Februari,mwanafunzi mmoja wa Tanzania alipigwa na kuvuliwa nguo na kundi moja katika mji wa Kusini wa Bangalore.

Chanzo: BBC
 
Hivi hawa waliopo huku wanajua wenzao humo nyumbani wanavyo watenda ndugu zetu?
 
Back
Top Bottom