Mwanafunzi wa chuo cha St Joseph akamatwa na bastola, risasi 13

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,411
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Lazaro Mbise (23) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kukutwa na bastola pamoja na risasi 13 ambayo alimwibia baba yake.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema mwanafunzi huyo alipokamatwa alikiri kuiba bastola hiyo pamoja na fedha kiasi cha Sh800, 000.

“Bastola hiyo ni LUGER cz100 mtuhumiwa alikiri aliiba pamoja na risasi kutoka kwa baba yake,” amesema Sirro.

Kamishna Sirro ameagiza mzazi wa mtuhumiwa kukamatwa ili afikishwe mahakamani kwa kosa la kutohifadhi bastola yake vizuri.

Chanzo: Mwananchi
 
Bashite na wabaya wa Nape mpaka leo hajaagiza.
 
Hyo bastola ni ndogo sana hata haiui yakuwindia tuu

Sema hajawindia mtu ndo bora
 
Achunguzwe vizuri asije kuwa miongoni mwa wale wa wale wa Kibiti na Mkuranga.
 
Ukiisha rasimishwa kuwa na bastola ni sawa na kuvalishwa hirizi! Na kama ukitaka kuiacha basi uwe na kabati la chuma. Ni utumwa wa namna fulani hivi.
 
Back
Top Bottom