Mwanafunzi wa kidato cha tatu ktk shule ya sekondari ya Tongoni mkoani Tanga amekutwa amekufa ndani ya nyumba ya kulala wageni iliyoko barabara ya 21, alikopelekwa kutolewa mimba bila mafanikio.
Muhudumu wa nyumba hiyo ya wageni alisema kuwa mwanafunzi huyo aliingia saa 4:00 asubuhi siku ya tukio akiwa ameambatana na kijana mmoja wakakodi chumba na baadaye alikuja mwanaume mmoja wa makamo ambaye aliulizia, na kuambiwa kuwa ndiyo wamefika, na baada ya kuonyeshwa chumba walichoingia naye akakodi chumba jirani, ndipo baadaye wote wakaingia kwenye chumba kimoja, alisema muhudumu. Na baada ya muda wa saa moja yule kijana na mmwaume wakaaga na kusema kwamba msichana amebaki chumbani akiwa amepumzika.
Akithibitisha ahabari hizi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga' Constantine Massawe, alisema taarifa ya tukio hilo itolewa na muhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni katika Kituo cha Polisi cha Chumbageni jijini Tanga. Kamanda Massawe alisema kuwa wahudumu hawakuwapa daftari ili waorodheshe majina yao, hivyo inakuwa vigumu kuwafahamu, kamanda Massawe alifafanua kuwa alifariki akitolewa mimba ya mwezi mmoja, na kusema mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa na kwamba Polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na kifo hicho.
Source by Mwananchi 26, Desemba 2012
ndio wanayataka hayo wanawake...sii umfunge miguu yenu hiyo mpaka molewe jamani!!