Mwanafunzi afia gesti akitolewa mimba

Mwanafunzi afia gesti akitolewa mimba

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
Mwanafunzi wa kidato cha tatu ktk shule ya sekondari ya Tongoni mkoani Tanga amekutwa amekufa ndani ya nyumba ya kulala wageni iliyoko barabara ya 21, alikopelekwa kutolewa mimba bila mafanikio.
Muhudumu wa nyumba hiyo ya wageni alisema kuwa mwanafunzi huyo aliingia saa 4:00 asubuhi siku ya tukio akiwa ameambatana na kijana mmoja wakakodi chumba na baadaye alikuja mwanaume mmoja wa makamo ambaye aliulizia, na kuambiwa kuwa ndiyo wamefika, na baada ya kuonyeshwa chumba walichoingia naye akakodi chumba jirani, ndipo baadaye wote wakaingia kwenye chumba kimoja, alisema muhudumu. Na baada ya muda wa saa moja yule kijana na mmwaume wakaaga na kusema kwamba msichana amebaki chumbani akiwa amepumzika.

Akithibitisha ahabari hizi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga' Constantine Massawe, alisema taarifa ya tukio hilo itolewa na muhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni katika Kituo cha Polisi cha Chumbageni jijini Tanga. Kamanda Massawe alisema kuwa wahudumu hawakuwapa daftari ili waorodheshe majina yao, hivyo inakuwa vigumu kuwafahamu, kamanda Massawe alifafanua kuwa alifariki akitolewa mimba ya mwezi mmoja, na kusema mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa na kwamba Polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na kifo hicho.

Source by Mwananchi 26, Desemba 2012
 
hiyo gesti ya voda fasta nini? maana inaonekana hawana utaratibu wa kuregester wateja
 
Yan kwa hali hii, mtu muuaji anaweza kuuwa hata watu mia moja bila kukamatwa. Hii kila siku nasikia uchunguzi unaendelea ndiyo tatizo. Ila nafikiri wa kwanza kukamwata anatakiwa Boy friend wake, (tatizo dada zetu wanaweza kuwa na BF zaidi ya mmoja) ila rafiki zake wa kike wanaweza kuwataja maBF wake wote coz huwa wanapeana taarifa. Hii ni uchunguzi rahisi sana kumkamata huyo kijana na dokta uchwara, ila police wa bongo, mtu akishakufa ndo mwisho.
 
Do hii hatari wakati mwingine watoto waliokua wanahitaji kuolewa sisi tunalazimisha shule tusilize sometime ideals za watoto hasa wanakuwa form 3 or 4
 
Sasa mimba zinatolewa gesti hausi na sio hospitali tena?
 
hapo doctor na boyfriend kwa mawasiliano ya simu washakamatwa. labda waamue kuzizima na kuzitupa na kupotea mazima. ila kwa polisi wetu walivyo, watambana doctor awape mlungura wa kutosha siku ziende.
 
Dah! Kale katoto ka 4m 3 nakapiga chini effectively 4m now!
 
Nawapa pole sana wazazi wa mtoto.
Pamoja na hayo lakini sisi wazazi inabidi tuwe makini sana na mienendo ya watoto wetu kwa kila wanachofanya kwani itasaidia kupunguza matatizo kama haya
 
Mwanafunzi wa kidato cha tatu ktk shule ya sekondari ya Tongoni mkoani Tanga amekutwa amekufa ndani ya nyumba ya kulala wageni iliyoko barabara ya 21, alikopelekwa kutolewa mimba bila mafanikio.
Muhudumu wa nyumba hiyo ya wageni alisema kuwa mwanafunzi huyo aliingia saa 4:00 asubuhi siku ya tukio akiwa ameambatana na kijana mmoja wakakodi chumba na baadaye alikuja mwanaume mmoja wa makamo ambaye aliulizia, na kuambiwa kuwa ndiyo wamefika, na baada ya kuonyeshwa chumba walichoingia naye akakodi chumba jirani, ndipo baadaye wote wakaingia kwenye chumba kimoja, alisema muhudumu. Na baada ya muda wa saa moja yule kijana na mmwaume wakaaga na kusema kwamba msichana amebaki chumbani akiwa amepumzika.

Akithibitisha ahabari hizi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga' Constantine Massawe, alisema taarifa ya tukio hilo itolewa na muhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni katika Kituo cha Polisi cha Chumbageni jijini Tanga. Kamanda Massawe alisema kuwa wahudumu hawakuwapa daftari ili waorodheshe majina yao, hivyo inakuwa vigumu kuwafahamu, kamanda Massawe alifafanua kuwa alifariki akitolewa mimba ya mwezi mmoja, na kusema mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa na kwamba Polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na kifo hicho.

Source by Mwananchi 26, Desemba 2012

Hili ni tatizo kubwa zaidi...nafikiri ni tatizo la kisera...Sera ya Afya(Health Policy) iruhusu utoaji mimba ili suala hili lifanyike kwa uwazi na katika mazingira salama zaidi... vinginevyo tutaendelea kupoteza ndugu zetu

Msimamo wa kupinga utoaji mimba(Abortion) ni msimamo uliopitwa na wakati...TUTAFAKARI

Nimeamini watoto wa kike wanaogopa sana mimba kuliko ukosefu wa kinga mwilini.
 
Hapo unaanza kukamata boyfriends wake wote,kama huyo mwanafunzi alikuwa na simu basi itakuwa rahisi kwa polisi kufatilia mazungumzo yao.
 
hiyo gesti ya voda fasta nini? maana inaonekana hawana utaratibu wa kuregester wateja

Kwani hata hizi zilizojazana hapa Jijini (nyingine za hadhi ya juu tuu) huwa wanahakiki hizo documents za mchukua chumba basi?

Ukweli ni kuwa nyumba nyingi za kulala wageni suala la ulazima wa kujirejista katika kitabu cha wageni halipo na, pale wanapojitahidi bado hakuna uhakiki wa vitambulisho! Nyumba hizi ni moja ya chochoro kubwa tuu la uhalifu hapa nchini!
 
Back
Top Bottom