Great Thinkers
Lets
assume Katika New cabinet ya JK anakuambia chagua decision making Position utakayotaka atakupa.
Sasa tuelezane
- Post au position gani ungependa kupewa na kwa nini?
- Ungefanya nini na ungekuwa na vision gani? Challenge kubwa kwenye position hiyo ni nini
- ungewaambia wananchi watathimi utendaji wako kwa vitu gani baada ya miaka mitatu?
- Kitu gani kiongozi wa position uliyochagua aliyepita alifanya sahihi na kitu gani hukubaliani na alicofanya?
Kama great thinkers tunaweza kuwapa mawazo chanya waheshimiwa watarajiwa
Nawasilisha.
Nitachagua kuwa nafasi ya Umwenyekiti wa tume ya uchaguzi.
Maamuzi, ni kufuta uchaguzi wote wa mwaka huu na kuuahirisha kwa miaka miwili wakati tukirekebisha katiba. Kulifanyia marekebisho daftari la wapiga kura na kuondoa majina hewa kama 8,000,000 yaliyopo kwa sasa na kuacha wapiga kura halali 12,000,000 tu. kuhakikisha kuwa wakuu wa mikoa/wilaya na wakurugenzi hawahusiki kwa aina yoyote ile katika uchaguzi. Mtu yeyote ambaye ni president appointee ni marufuku kuwa na uhusiano na NEC.
Kuhakikisha kuwa kura zote zinabandikwa vituoni na kutangazwa kwenye vyombo vya habari as they come. Na NEC inakuwa na database ya majina na vituo online. Kuhakikisha kuwa majina ya wapiga kura yanabandikwa mara tu uandikishaji unapoisha na kuwapa wananchi muda wa kuyahakiki na kujua ni wapi watapigia kura badala ya kusubiri siku tatu kabla ya kupiga kura.
Kuhakikisha kuwa matokeo ya vituoni ni ya mwisho kama wakala akitia saini kituoni na kubandikwa basi hakuna wa kuyabadili isipokuwa amri ya mahakama tu katika kesi.
Kuhakikisha kuwa kura zinatangazwa ndani ya masaa sita tangu kufungwa vituo vya kupigia kura na majimbo yanafanya hivyo ndani ya masaa 8 tangu kufungwa vituo vya kupigia kura.
Tume ikimtangaza mshindi awe wa rais ama ubunge na ikatokea kesi ikafunguliwa basi mtu huyo atakuwa amepotezasifa za kuapishwa mpaka shauri lake liamuliwe na mahakama ya rufaa kama litafika huko.
.............................................