Mwana diplomasia dr. Kikwete. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwana diplomasia dr. Kikwete.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kasimba G, Mar 9, 2012.

 1. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,569
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kwa nchi kama Marekani, huwa hawaruhusu mwanadiplomasia kuwa Rais. Huwa wanafanya hivyo kwa maksudi maalum kuwa, mwanadiplomasia hawezi kuwa na maamuzi magumu,hoja zake huwa zinapunguzwa ukali, majibu ya mwanadiplomasia huwa siyo makali/magumu hata maamuzi yake pia ni hivyohivyo.

  Kwa mwanadiplomasia hawezi kusema nduguyangu hujapendeza atasema ingekuwa vizuri kama ungevaa au ungejitengeneza vingine, huwa, kwa mtu mzito hawezi kuelewa ujumbe wa kidiplomasia. Watendaji wengi ni wazito na ujumbe wa kidiplomasia hawawezi kuuelewa, mfano, posho za wabunge, Mwanadiplomasia mheshimiwa Rais alitoa changamoto kuwa walitafakali! Watendaji wakaona hapa ulaji!!! Ni kwamba huwa hawawezi kuelewa ujumbe wa kidiplomasia.

  Watanzania na waafrika wengi huwa wanapochagua kiongozi hawazingatii historia au kazi alizowahi kufanya mtu anaye omba kuchaguliwa kuwa kiongozi ,ambapo, ni kosa kubwa saana. Rais wa nchi huwa ni amirijeshi mkuu, Huwa hatakiwi awe mwanadiplomasia kama wamarekani wanavyofanya, kwa kuwa mwanadiplomasia maamuzi yake ya kidiplomasia hayako moja kwa moja, maamuzi huwa “yanajifichaficha,” ajenda haiko wazi!

  Kwa Mh. Dr. Kikwete kweli anadhihirisha uanadiplomasia wake kwa maamuzi yake ambayo huwa yanazingatia pande mbili, yaani hayataki kuumiza upande wowote, mkosa/mtuhumiwa na mwenyehaki, mfano, kesi za EPA n.k. Hapo diplomasia ilizingatiwa!
  Je kwa vigezo hivyo Watanzania walifanya kosa kumchagua amiri jeshi mwanadiplomasia? na je wanatambua kosa walilifanya ili wasije kurudia teana na ikiwezekana wafanye kama wamarekani au iwemo katika katiba kabisa kuwa mwanadiplomasia asiwe Rais wa nchi kamwe?

  Nawasilisha.
   
 2. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mwana diplomasia anatakiwa awe na sifa hizi Subtly skillful handling of a situation,Wisdom in the management of public affairs.Ila hata haya yameshinda anachekacheka tu wakati nchi inateketea, angeweza kukaa na pande zote mbili madaktari na serekali ila amepuuza madai ya upande mmoja na kujiweka bado unamuita mwanadiplomasia, hana sifa ya kutatua mgogoro bila kuonyesha interest ya upande mmoja kama anavyofanya sasa kuwa chafua madaktari.Futa hiyo sifa ya kumuita mwana diplomasia
   
Loading...