Rugby Union
JF-Expert Member
- Nov 21, 2012
- 402
- 257
Basi la Azam likiwa uwanjani, wakati timu hiyo ilipokuwa ikifanya mazoezi mkoani Mbeya chini ya ulinzi wa polisi.
Azam inajivunia rekodi ya kuwa timu pekee iliyofanikiwa kuifunga Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine tangu timu hiyo ilipopanda daraja na kucheza ligi msimu uliopita, iliifunga mabao 2-1 kwenye mechi ya mzunguko wa pili wa ligi msimu huo.
Mwambusi alisema wanatambua kuwa Azam ndiyo timu iliyowawekea doa kwenye rekodi yao ya mechi za nyumbani, hivyo hawatakubali hilo liwatokee tena msimu huu kwani wamejipanga kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa Jumamosi.
"Azam haitabebwa na rekodi kwenye mechi ya Jumamosi, tumejipanga vizuri na tutahakikisha tunaibuka na ushindi kwenye mchezo huo.
"Natambua kuwa haitakuwa kazi rahisi kwani Azam ni timu nzuri lakini tutapambana kuhakikisha tunafanya vizuri, pointi tatu ndiyo muhimu zaidi kwetu," alisema Mwambusi ambaye alitwaa tuzo ya kocha bora msimu uliopita.
Mbeya City inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa imeshinda mechi moja na kutoka sare mbili, mpaka sasa haijafungwa bao hata moja kwenye mechi hizo. Azam inashika nafasi ya pili kwenye msimamo huo ikiwa na pointi saba.
MwanaSpoti