kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,428
- 13,936
Kazi na jambo kubwa gumu kwa wanadamu kulifanya ni uwezo wao wa kuamini. Kiwango chako cha kuamini kinalingana na kiwango chako cha kufanikiwa katika jambo hilo; imani yako itakuwezesha kutembea juu ya maji, imani yako inakausha maji ya bahari na kutembea kama nchi kavu; "imani yako ndio iliyokuponya".
Wewe uliyeamini usilalamike na wewe kama mpagani bali mwambie Mungu kila jambo ambalo unaamini kwa dhati yako kuwa halikufai wewe. Mungu bila kuchelewa ataliondosha jambo hilo mara moja bila kuchelewa.
Namna mtakavyokuwa wengi mnaoamini kuwa jambo au mtu fulani hakufaeni inakuwa rahisi zaidi kuondoshwa hilo tena mara moja, maana vitu, watu, na matukio yote ni yake mungu na yanatoka kwake ila yanakupata yote kwa mapenzi yake na kwasababu yake fulani kwako.
Kama utadhani maombi yako/yenu yatachelewa kujibiwa basi yachanganye pamoja na kufunga au kutoa sadaka ili mungu akubadilishie chakula chako halali ulichokiacha kukila ama kitu chako halali ulichokitoa sadaka na kitu unachokiomba upatiwe.
Anaekuendea kinyume mshitaki kwa baba yako wa mbinguni, usilalamike ovyo barabarani ukashitakiwa bure, yeye Mungu anatosha sana kugeuza hiki kuwa kile na kile kuwa hiki.
Semeni wote AMEEN.