Mbunge wa CCM: Mafisadi wamemwaga 60m/- jimboni
Na Thobias Mwanakatwe
28th December 2009
Asema lengo ni kutaka kumng`oa 2010
Mbunge wa Lupa CCM wilayani Chunya, Victor Mwambalaswa
Mbunge wa Lupa CCM wilayani Chunya, Victor Mwambalaswa, ameibuka na hoja nzito na kudai kuwa mtandao wa mafisadi umejipenyeza jimboni mwake kwa kusambaza fedha chafu zaidi ya Sh. milioni 60 kwa lengo la kutaka kumng'oa Uchaguzi Mkuu mwakani.
Mbunge huyo alitoa madai hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, kuelezea mambo aliyokutana nayo wakati yupo kwenye ziara ya kutembelea wapiga kura wake jimboni.
Mwambalaswa alisema katika ziara yake alibaini kuwa zaidi ya Sh. milioni 60 zimesambazwa katika vijiji vya jimbo la Lupa kwa lengo la kushawishi wananchi wasimchague mwakani.
Kwa mujibu wa Mwambalaswa, fedha hizo ambazo ana imani zimetolewa na mtandao wa mafisadi, zinasambazwa na mawakala wa mafisadi, wakiwemo watu wanaotaka kugombea ubunge jimboni humo mwakani.
Mwambalaswa alisema kutokana na fedha hizo kugawiwa ovyo vijijini, wananchi wameingiwa na hofu kubwa na kuhoji kama watu hao wanaozisambaza wana lengo zuri kwenye jimbo hilo kwani iwapo watakosa ubunge nini hatma kwa wananchi watakaokuwa wamepewa mamilioni hayo.
Mbunge huyo ambaye hakutaka kuweka wazi katika suala hilo, alisema fedha hizo chafu zimeletwa katika jimbo la Lupa kutoka kampuni moja ya ujenzi iliyopo mkoani Mwanza na kwamba uthibitisho wa kusambazwa kwa mamilioni hayo ameupata kutoka kwa wananchi ambao wamegawiwa.
Mwambalaswa alisema hata hivyo, anashangaa mafisadi kusambaza fedha hizo wakati yeye (Mwambalaswa) hajawahi kuwashambulia mafisadi hata siku moja.
''Mimi sijawahi kuwashambulia mafisadi lakini inashangaza nimekuta jimboni mwangu wamesambaza mamilioni,' 'alisema.
Alisema hata hivyo, hatishiki na mafisadi kumwaga fedha hizo na kuwataka wananchi kukaa mkao wa kula mamilioni hayo ila wajiulize wanaotoa fedha hizo wanania gani na je, wasipochaguliwa hatma yao itakuwaje.
''Kama umeikosea jamii kwa bahati mbaya kwa matendo yako nenda kwa padre au kwa sheikh ukatubu lakini si kumshughulikia mwenzako kwa fedha,'' alisema.
Kwa mwenye uwezo wa kutumikia wananchi wake.. na kama kweli anapendwa....... tumieni chochote hatang'olewa. Lakini ukishaona mtu anaanza kuhaha kwa maneno........ ujuwe ni debe tupu haliachi kelele.Mheshimiwa naona naye pressure imeanza kupanda na kushuka. Ukiona mbunge anakuja na madai mazito kama hayo bila kutaja majina jua ni yale yale ya kukalia kuti kavu, anataka kutumia neno ufisadi kudanganya wananchi ili kujiokoa. Kama ana ushahidi si aende polisi au mahakamani kuwataja hao wanaomwaga hizo pesa.
Mheshimiwa Mwambalaswa, kama una uhakika na madai yako, si wataje wanaosambaza pesa? Vinginevyo na wewe wapelekee wananchi zile pesa za posho mbili wakafaidi maana CCM wote mnafanana tu.
Mwanakatwe naye, hiyo ni hoja nzito au tuhuma (madai) nzito? Hawa waandishi wetu wa kwenye miembe balaa tupu.
Kwa mwenye uwezo wa kutumikia wananchi wake.. na kama kweli anapendwa....... tumieni chochote hatang'olewa. Lakini ukishaona mtu anaanza kuhaha kwa maneno........ ujuwe ni debe tupu haliachi kelele.
Tutasikia mengi sana mwaka huu. Hata wale waliokuwa wanashinda Dar badala ya majimboni kwao, dakika ya mejeruhi ndio wanaamkia majimboni na kuja na kelele za mafisadi.
Ukiwa mchapa kazi, hata mafisadi waje na pesa kiasi gani, naamini wananchi hawatakutema. Utaratibu wa sasa wa wanachama wote CCM kupiga kura, una walinda wabunge wachapa kazi maana sio rahisi fisadi kuhonga wananchi wote.
Wana JF nawashauri muwe mnafanya research kabla ya kutoa comments zenu. Inaonyesha wengi mnachangia mada kwa kukurupuka. Majibu yenu hayajaniridhisha kabisa.
Hawa watu wananitibua kweli; kama wameshindwa kufanya mambo ya maendeleo kwenye majimbo yao wanafikiri watachaguliwa kwa sababu wanalia lia na mafisadi? Nani aliwaambia kuwa wana hati miliki ya majimbo?
Mwenyewe anasema yeye hajawahi "kuwashambulia" mafisadi sasa iweje wanamfuata fuata?. Kwa maneno mengine yeye hana tatizo watu kuliibia taifa muradi tu yeye abaki kuwa Mbunge!
Kazi kweli kweli...
Unamaanisha alikwenda kwa Yahaya Hussein au Bruno kanyungu?Kama sikosei huyo bwana alitumia all means...I mean all means....kumng'oa Mzee wa G55 Njelu Kasaka...sasa analialia nini?