Mheshimiwa naona naye pressure imeanza kupanda na kushuka. Ukiona mbunge anakuja na madai mazito kama hayo bila kutaja majina jua ni yale yale ya kukalia kuti kavu, anataka kutumia neno ufisadi kudanganya wananchi ili kujiokoa. Kama ana ushahidi si aende polisi au mahakamani kuwataja hao wanaomwaga hizo pesa.
Mheshimiwa Mwambalaswa, kama una uhakika na madai yako, si wataje wanaosambaza pesa? Vinginevyo na wewe wapelekee wananchi zile pesa za posho mbili wakafaidi maana CCM wote mnafanana tu.
Mwanakatwe naye, hiyo ni hoja nzito au tuhuma (madai) nzito? Hawa waandishi wetu wa kwenye miembe balaa tupu.
Mheshimiwa Mwambalaswa, kama una uhakika na madai yako, si wataje wanaosambaza pesa? Vinginevyo na wewe wapelekee wananchi zile pesa za posho mbili wakafaidi maana CCM wote mnafanana tu.
Mwanakatwe naye, hiyo ni hoja nzito au tuhuma (madai) nzito? Hawa waandishi wetu wa kwenye miembe balaa tupu.
Mbunge wa CCM: Mafisadi wamemwaga 60m/- jimboni
Na Thobias Mwanakatwe
28th December 2009
Asema lengo ni kutaka kumng`oa 2010
Mbunge wa Lupa CCM wilayani Chunya, Victor Mwambalaswa
Mbunge wa Lupa CCM wilayani Chunya, Victor Mwambalaswa, ameibuka na hoja nzito na kudai kuwa mtandao wa mafisadi umejipenyeza jimboni mwake kwa kusambaza fedha chafu zaidi ya Sh. milioni 60 kwa lengo la kutaka kumng'oa Uchaguzi Mkuu mwakani.
Mbunge huyo alitoa madai hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, kuelezea mambo aliyokutana nayo wakati yupo kwenye ziara ya kutembelea wapiga kura wake jimboni.
Mwambalaswa alisema katika ziara yake alibaini kuwa zaidi ya Sh. milioni 60 zimesambazwa katika vijiji vya jimbo la Lupa kwa lengo la kushawishi wananchi wasimchague mwakani.
Kwa mujibu wa Mwambalaswa, fedha hizo ambazo ana imani zimetolewa na mtandao wa mafisadi, zinasambazwa na mawakala wa mafisadi, wakiwemo watu wanaotaka kugombea ubunge jimboni humo mwakani.
Mwambalaswa alisema kutokana na fedha hizo kugawiwa ovyo vijijini, wananchi wameingiwa na hofu kubwa na kuhoji kama watu hao wanaozisambaza wana lengo zuri kwenye jimbo hilo kwani iwapo watakosa ubunge nini hatma kwa wananchi watakaokuwa wamepewa mamilioni hayo.
Mbunge huyo ambaye hakutaka kuweka wazi katika suala hilo, alisema fedha hizo chafu zimeletwa katika jimbo la Lupa kutoka kampuni moja ya ujenzi iliyopo mkoani Mwanza na kwamba uthibitisho wa kusambazwa kwa mamilioni hayo ameupata kutoka kwa wananchi ambao wamegawiwa.
Mwambalaswa alisema hata hivyo, anashangaa mafisadi kusambaza fedha hizo wakati yeye (Mwambalaswa) hajawahi kuwashambulia mafisadi hata siku moja.
''Mimi sijawahi kuwashambulia mafisadi lakini inashangaza nimekuta jimboni mwangu wamesambaza mamilioni,' 'alisema.
Alisema hata hivyo, hatishiki na mafisadi kumwaga fedha hizo na kuwataka wananchi kukaa mkao wa kula mamilioni hayo ila wajiulize wanaotoa fedha hizo wanania gani na je, wasipochaguliwa hatma yao itakuwaje.
''Kama umeikosea jamii kwa bahati mbaya kwa matendo yako nenda kwa padre au kwa sheikh ukatubu lakini si kumshughulikia mwenzako kwa fedha,'' alisema.