mwalimu wa primary kubadilisha nae

Escoba

Member
Joined
Jan 10, 2013
Posts
75
Reaction score
18
natafuta mwalimu wa shule ya msingi wa kubadlisha nae ye aje Tarime me nije sehemu yoyote ya tanga, morogoro, kibaha, arusha , kilimanjaro au dsm
 
sio lazima uwe ww hata ukiwa na rafiki ako au mwalimu yeyote ambaye yupo interested kwenda tarime contact 0655906828
 
Huko sizani kama utapata mtu nani hayapeendi maisha yake na kichwa chake ?kukatwa kicha si mchezo
 
mmmh rolya?!!!!!. ni balaa we komaa2 mkuu hapafai huko full kuchomana visu daaa
 
Kasi ya mauaji Musoma yaongezeka T Details
Imechapishwa Ijumaa, 08 Februari
2013 22:03
Imeandikwa na Erasto Mkumbange,
Butiama
Imesomwa mara: 55 KIJANA mmoja aliyetambulika kwa jina la Magere Masatu Mkazi wa Mtaa wa Nyakato, Wilaya ya Musoma ameuawa kisha kutupwa mtoni. Katika tukio hilo wanajeshi waliingilia kati na kufanikiwa kudhibiti maafa zaidi baada ya nyumba moja ya mtuhumiwa wa mauaji hayo kuchomwa moto. Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo la Februari 4 mwaka huu katika kijiji cha Etaro wilayani humo, walisema kuwa siku ya tukio marehemu aligongana na pikipiki ambapo marehemu aliamua kumlipa fedha aliyegongana naye lakini balozi wa eneo la tukio alipelekewa pikipiki ya marehemu kwa ajili ya kuihifadhi. “Baada ya tukio kweli pikipiki ilichukuliwa na kupelekwa kwa balozi wakati wanakwenda kuna vijana wawili walikuwa wakifuatilia kwa nyuma, na baada ya hapo marehemu hakuonekana tena hadi jana alipoonekana amekufa na yupo ndani ya mto,”alisema shuhuda aliyekataa kutaja jina lake. Baada ya waendesha pikipiki wa Wilaya ya Musoma kupata taarifa kwa kuuawa kwa mwenzao walikwenda na kuvamia kijiji hicho kwa kuwapiga baadhi ya wananchi na balozi ambaye alikuwa amehifadhi pikipiki hiyo kisha kumtaja mmoja wa wauaji hao kuwa ni Koti Magee mkazi wa kijiji hicho. Waendesha pikipiki hao walikwenda hadi kwa mtuhumiwa huyo na walimkuta lakini alifanikiwa kuwatoroka kisha kukimbilia ziwani na kujitosa kwenye maji kuogelea ikiwa ndio pona yake. Baada ya kumkosa vijana hao walirudi nyumbani anapoishi kijana huyo ambaye anaishi na baba yake mzazi aliyejulikana kwa jina la Magee Saganda kisha kuitia moto nyumba moja na kuteketea kabisa. Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania waliwahi kufika katika eneo la tukio na kuzuia uchomaji moto wa nyumba zingine. Jeshi la polisi baada ya kufika lilichukua mwili wa marehemu na Balozi wa eneo hilo Peter Mabojano na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho kwa ajili ya mahojiano zaidi. Mwili wa marehemu umepelekwa katika Hospitali ya Mkoa huo na umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa ajili ya taratibu za mazishi. Tukio hili ni la tano kutokea katika wilaya ya Butiama kuanzia Novemba mwaka jana hadi Februari mwaka huu. Matukio hayo ni pamoja na la Desemba 21, mwaka huu saa 5:30 usiku Tabu Makanya (68) Mkazi wa Kijiji cha Kwikuba alichinjwa lakini watuhumiwa wakiwa katika harakati ya kuondoka na kichwa chake waliwahiwa na wananchi kisha kukitupa. Tukio lingine lilitokea Desemba 2, Blandina Peru alichinjwa na kuchukuliwa damu yake tu na Sabina Mkireri wa kijiji cha Kabegi, alichinjwa na kuondoka na kichwa chake. Aidha kijana aliyetambuliwa kwa jina la Thomas Majengo (23-28) Mkazi wa Kiara, Musoma Mjini alichinjwa na kunyang'anywa pikipiki.
 
mkuu musoma,mar,tarime.rorya.. Huko mnnhhhhh!!!?? escober
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…