mwalimu wa hisabati darasa la sita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mwalimu wa hisabati darasa la sita

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Mar 15, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  SHULE ya Msingi Bunge ya jijini Dar es salam, imeingia kwenye kashfa baada ya mwalimu mmoja shuleni hapo kuwaadhibu wanafunzi kwa waya wa transfoma.
  Taarifa kutoka shuleni hapo ilisema kuwa mwalimu anayefahamika kwa jina la Preygod Isaya [26] ameiingiza shule hiyo kwenye kashfa hiyo.

  Mwalimu Isaya mwalimu wa hisabati darasa la sita amewapa wanafunzi wake adhabu ya kuwachapa na waya wa umeme baada ya kuona wanafunzi hao hawasikii.

  Hata hivyo mwalimu huyo alifafanua kuwa aliamua kuwachapa na waya huo kwa kuona fimbo haiwatoshelezi kuwapigia wanafunzi hao kutokana na kosa lao.

  Pia shule hiyo imekuwa na tuhuma ya kuwapa adhabu ya kuwarudisha wanafunzi nyumbani kutokana na kuchelewa kufika shuleni hapo.

  Na zoezi hilo limedaiwa kubarikiwa na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Hadija Telela.

  WAZO:serikali imezuia uchapaji wa viboko mashuleni sasa mbadala wake kwa wanafunzi wanaokusa waalimu watoe adhabu gani kwao??maana kwa mwanafunzi wa kibongo akiachwa tu sidhani kama tutafika maana wanafunzi walio wengi hawapendi shule kutokana na mawazo ya utoto hasa hawa wanaosoma katika shule za serikali na ambao wanatoka katika familia duni kimaisha!!!sijui tutashauli vipi juu ya hili wanajamii au wanajamvi au tunamtazamo gani juu ya hili?ukizingatia tupo kusini mwa jangwa la sahara!
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Unasemaje?!, lazima watoto wetu wachalazwe kwa nyaya za umeme?!, uliona yaliyotokea buguruni- mwalimu kanyofoa kope za mwanafunzi kisa kasahau daftari nyumbani: wewe unabaliki hili?! CRAP.
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hujanielewa mkuu bado ninachosema kwamba mnafikiri baada ya kuzuia adhabu ya viboko tufanyi nini ambacho kiwe mkabala wa viboko yaani kwamba ili kudhibiti nidhamu ya mwanafunzi kifanyike nini?mie siungi mkono hayo ya kunyofolewa kope!nimekua nikisikia kwa muda mrefu sana viboko vizuiwe mashuleni bila kusikia mapendekezo ya kukabili nidhamu!
   
 4. Revolution

  Revolution JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 567
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 60
  Watoto wapelekwe na school bus shuleni, wapewe chai ya maziwa, bites, chocolate, juice, wafundishwe kwa upendo, wacheze michezo mbalimbali, wakifika nyumbani wasipewe kazi nzito, wasaidiwe homework na wazazi na sio mabeki tatu, wanunuliwe nguo mpya za shule na mabegi mapya mara kwa mara, wafundishwe tabia njema tangu utotoni, wasikilizwe, waheshimiwe, wapendwe, na mambo mengine mbalimbali halafu uone kama kuna mtoto atachukia shule au atatega shule....watoto huwa ni wajanja sana kugundua hapa ndipo au sipo mapema kabisa........
   
 5. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  usiangalie kwa familia zenye kipato kuna familia zipo vijijini ambako hakuna yote hayo uliyoyataja pia kila mtoto wa serikali kuna uwezekano kweli akapelekwa shule kwa school bus na hali hii ya maisha ilivyo ngumu
   
 6. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2011
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Tehe.. We umenifurahisha sana. Ila sidhani kama ume consider hali ya watanzania walio wengi waishio vijijini.
   
 7. M

  MZAWATA JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  viboko muhimu sana, cc tumelelewa na viboko dats y tuko hapa, watoto wa siku hz weng wao wanafel kwa kukosa motivation hii, lakin kuwaadhibu kwa waya hapa mwalimu amekosea tena sana tu, angetafuta njia mbadala lakin co waya
   
 8. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kwa waya nakubali kabisa kakosea ila ukweli utabaki viboko muhimu nakuunga mkono man cha muhimu kuwe na idadi ya viboko na kulingana na afya ya mwanafunzi maana kuna wengine kiboko kimoja tu kadondoka na nasikitika shule za miaka hii hazina gwaride wala mchakamchaka!
   
 9. TATE

  TATE Member

  #9
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaani hii habari imenigusa, hapo Bunge kuna historia ya walimu wakatili hakuna mfano, utafikiri hawana watoto au hawatazaa, yaani ndo chanzo kimojawapo cha utoro mashuleni.
   
 10. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  shule ipo ikulu
   
 11. m

  muzachai Member

  #11
  Mar 15, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ualimu ni kazi ngumu lakini at the end of the year unatakiwa ufaurishe wanafunzi wote. hivyo strategy ya kwanza ni kuanza kuwa groom standard six kuwa kama LAST YEAR(LY). Wakifika ly wanakuwa wamekomaa kabisa. hivyo basi shule ya bunge huwa inafaurisha watoto wote darasa la saba. ikitokea bahati mbaya wafeli wawili au mmoja. kwa kudhibitisha hilo kupata nafasi ya standard one lazima ndugu yako awe either mwalimu au kigogo wa serikali kuu. wanafunzi wa standard one wanafanyiwa interview ya kusoma na kuandika kama hawezi nafasi hakuna. Jamani nani kwa umri wetu huu hajui utamu wa viboko na matunda yake. ukitaka kujua zaidi waulize wanafunzi wa tabora boys viboko vya jeshi vilivyosaidia kutengeneza one. sasa hivi hakuna viboko ziro za kumwaga. viboko oyeee .
   
 12. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Waalimu wengi wa shule za msingi ni wavuta bange. Sasa unategemea nini kutoka kwa mvuta bange?
   
 13. k

  kisukari JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,042
  Trophy Points: 280
  hii shule jamani mbona ilikuwa nzuri miaka ya nyuma?mm nilisoma hapo hapo.watoto wengi wa wakubwa{mimi sio mmoja wapo}wengi walisoma hapo
   
 14. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  tatizo wanasema sio watoto ni waalimu wanawachapa kwa waya ila sina hakika kama ina watoto wakorofi pia
   
 15. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  viboko virudi tu shuleni
   
Loading...