The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,708
Mpendwa Julius Kambarage Nyerere,
Pamoja na madhaifu yako kama kututengenezea huu mfumo mbovu na hatari, bado tunakukumbuka. Nakukumbuka kwa majonzi na vilio. Je, hali ikoje?
Kwanza, kuna jamaa mmoja mbabe alipenya akaukwaa urais na kuwageuza watu wako wanyonge ili awanyonge.
Jamaa alianzisha utekaji ambao hadi sasa aliyemrithi ameuzidisha. Tunatekwa, tunapotezwa, kuteswa na kuuawa na hakuna anayejali wala kutoa maelezo hata ya uongo.
Wapigaji wanapiga kama hawana akili nzuri. Yule jamaa uliyemkataa mwaka 1995, pamoja na kutawala na kuiba kwa miaka kumi, bado anaendesha nchi. Nchi imegeuka chaka la wezi. Ikulu wamejaa wezi na wafanyabiashara wenye kutia shaka. Mitandao uliyopinga na kudhoofisha sasa hivi imeshika kani.
Uchaguzi wa ndani ya chama ulitindinganywa na mama akajipenyeza na 'kugombea' bila kuteuliwa na chama kufanya hivyo.
Siku hizi tumewekwa rehani. Waarabu na wachina wako wanahondomola.
Sera ya kujigegemea imezikwa. Badala yake kuna uchawa na ukunguni.
Tanzania iliyosifika kwa haki na umoja na usawa imegawanyika. Inaongozwa kifamilia. Wakubwa wanateua watoto wao, washikaji zao, wakwe zao na mashoga yao. Kila kitu ni vururuvururu na meli inaenda mrama.
Kusifiana uzwazwa nayo ni sera namba mbili. Kukopa na kutumia hovyo ndo usiseme.
Leo niachie hapa kwa sababu machozi na majonzi yamenizidi.
RIP mwana wa Burito JK Nyerere.
Ni baba yako The Father of All you included.