Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,561
- 19,056
'It has been confirmed that, One of Africa's greatest sons, champion of Africa liberation, dear friend of Uganda, former President of United Republic of Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere has died' Baada ya tangazo hilo lililotolewa bungeni na aliekua Makamu wa Rais wa Uganda wakati huo Eliya Kategeya bunge zima lilipiga kimya kwa sekunde kadhaa kama limemwagiwa maji na ikaanza minong'ono na zogo la fadhaa kwa taarifa hizo za kifo cha Mwalimu. shughuli za bunge la Uganda kwa siku hiyo zika ahirishwa!
Mtakumbuka hivi karibuni Rais Museveni alipokua kwenye ufunguzi wa jengo la forodha kama sikosei, Mtukula Mkoani Kagera alifichua kwamba alikua akipita sana hapo border miaka ya nyuma kwa 'kuvunja sheria'. Alikua anapitisha silaha! Halikadhalika kwenye mazishi ya Nelson Mandela Rais Kikwete alieleza mlolongo wa viongozi na matukio ya kimkakati ambayo wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini walipitia wakiwa Tanzania, japo watu wengine walikosoa hotuba ile kama ya kuwasimanga watu baada ya kuwasaidia, kwamba angekua Nyerere asingeweza kutoa siri hizo kama ambavyo amekufa na siri nyingi za namna hiyo.
Huyo ndio Mwalimu Nyerere anaekumbukwa kwa kutengeneza 'mifumo' ndani na nje ya nchi yake. Kwa nje ya nchi ni mtu aliyekua na weledi wa hali ya juu kabisa wa diplomasia,siasa na sheria za kimataifa. Alitengeneza viongozi wengi wa kanda yetu ya Afrika mashariki kama hao kina Museveni, Kagame na hata Raila alishawahi kufichua hadharani kwamba wakati serikali ya Moi ilipomnyima Passport ya kusafiria kwenda Ujerumani kusoma miaka hiyo Nyerere alimpatia kama raia wa Tanzania!
Aliwajua watu kwa historia, hulka na tabia zao na akizitumia kama advantage ya kumsaidia kufikia malengo yake. Ukizungumza na Waganda watakwambia hata majina ya baadhi ya wapiganaji wa jeshi la 'kuikomboa' Uganda toka utawala Idd Amin Dadaa aliyatoa yeye. Hayo ni kama ya kina Salim Salehe ambae ni ndugu wa mama mmoja na Museveni na wengine wengi ambao Mwalimu alishauri watumie majina ya kiislamu ili kuchota fikra za baadhi ya Waganda ambao walikua wanadhani Amini anaungwa mkono na waislam!
Kambi na Oparations za wapigania Uhuru wa Msumbiji, Zimbabwe na Afrika ya Kusini zilikua na ukubwa ambao usingeweza kudhania kama ulikua unaendelea Tanzania. Mambo mengi yaliratibiwa kwa siri na ustadi mkubwa na kwa uongozi na maelekezo ya moja kwa moja ya Mwalimu Nyerere.
Kwa siasa za ndani bado hajatokea bingwa wa kuweza kuzicheza kama Mwalimu. Nyerere alilijua vyema taifa lake, aliwajua watu wake na aliwajua aliokua akifanya nao kazi nguvu na udhaifu wao. Aliiunda taasisi ya intelijensia yenye weledi wa hali ya juu kwa majukumu ya ndani na nje ya nchi.
Sehemu zote kuanzia mitaani, viwandani, mashuleni na kwenye taasisi za elimu pamoja na taasisi za dini(Hasa zile kubwa kama TEC,CCT na BAKWATA) waliwekwa watu wa system ambao kazi yao ni tofauti na polisi. Taarifa kuhusu hali ya nchi na hasa usalama zilikua zinaratibiwa very systematically na usiri mkubwa ulikuwepo, tofauti na siku hizi ambapo hata Mkurugenzi na naibu Mkurugenzi wa TISS sio tu wanajulikana kwa majina bali kwa kuonekana kwenye runinga mara kwa mara. Ilikua inawezekana kwa taasisi za kidini kuwa na kiongozi asiekua wa dhehebu hilo na hakuna aliyejua!
Nyerere alipowashauri CCM waingie katika mfumo wa vyama vingi alisema inabidi CCM iratibu hiyo transition vinginevyoi mabadiliko yakitoka nje itakua tabu. Matokeo yake vikaundwa vyama ambavyo wengi ya viongozi wake na wanachama waandamizi ni watumishi wa System. Nikiwaona baadhi ya wanaodhaniwa ni viongozi imara na wafia mabadiliko wa vyama vya upinzani wanavyochota na kuchochea watu hua nachekea tumboni tu. Mwalimu Nyerere mwenyewe akitamani sana CCM imeguke vipatikane vyama viwili ambavyo hakika vingekuana na mfumo kama wa chama dola hivi, lakini vinavyodhibitiwa na dola yenyewe.
Hata mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 fundi mkuu ambaye mkono wake wa chuma haukuonekana alikua Mwalimu Nyerere(pitia kitabu cha kwaheri ukoloni kwaheri uhuru), na viongozi wengine wanaodhaniawa ni wapigania demokrasia kiuhalisia ni watu wanaochukua maagizo kutoka katika 'Mfumo" ambao Mwalimu aliuasisi
Hali hivi sasa inaanza kugeuka kwa system kufanya kazi kama ya kipolisi kitu ambacho nadhani mwasisi wake kama angekua hai leo asingelishauri hivo. Najiuliza ni weledi umepungua au uoga umezidi au mchasnganyiko wa vyote viwili? Vyovyote itakavyokua kitendo chochote cha kuimarisha nchi na tunu zake ni kitendo cha kuungwa mkono na kinyume chake kilaaniwe