Mwalimu na mwanafunzi wake

Nukta5

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2014
Posts
1,192
Reaction score
1,315
Mtoto: Mwalimu mimi nataka nisome darasa la nne kwani hili la3 halinifai.

Mwalimu: Kwa nini unasema hivo?

Mtoto: Nina akili...

Basi mwalimu kamueleza mkuu wa shule na mkuu kaitisha interview kwa dogo.
Maswali ni haya....

Mwalimu: Kwenye ndege kuna matofali 20 tukitoa moja tukalidondosha chini
yatabaki mangapi?

Dogo: Yatabaki 19.

Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka tembo kwenye friji.

Dogo: Unafungua friji unamuweka tembo kisha unafunga.
Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka nyani kwenye friji.

Dogo: Unafungua friji unamtoa tembo ulemuweka kisha unafunga friji.

Mwalimu: Kuna sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa simba, wanyama wote wameenda kasoro mmoja. Ni nani na kwa nini?

Dogo: Ni nyani kwa sababu tumemuweka kwenye friji.

Mwalimu: Bibi kizee amevuka mto unaokuwaga na mamba na viboko wakali aliwezaje?

Dogo: Aliweza kwani mamba na viboko nao walienda kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa simba.

Mwalimu: Ingawa bibi kizee alivuka mto baadae alikufa. Unadhani kwa nini?

Dogo: Alidondokewa na lile tofali lililotoka
kwenye ndege na kutupa chini.

Mwalimu mkuu: Huyu dogo akasome chuo kikuu....
 
​Sawa hii imetuburudisha, sasa tuambie vipi kuhusu jina lako?
 
Hahahahahahahahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…