Mwalimu mzoefu nahitaji kazi ya kudumu sasa

Mwalimu mzoefu nahitaji kazi ya kudumu sasa

KURA ZA SIRI

Member
Joined
Oct 3, 2014
Posts
18
Reaction score
3
Wadau wa jf
Mimi ni mwalimu mwenye uzoefu wa miaka sita katika kufundisha shule za binafsi kwa upande wa sekondari na primary...Nina stashahada ya elimu lakini pia na shahada ya elimu..
Baada ya kutoka stashahada nilifundisha sekondari na baada ya miaka miwili nilienda kusoma shahada na baada ya kutoka huko nilifundisha katika shule mojawapo maarufu sana na yenye matokeo mazuri hapa Dar Es salaam na ipo maeneo ya Tabata ambapo katika shule hyo nilifundisha upande wa sekondari ila kwa sasa nipo shule nyingine ya hapa hapa jijini Dar iliyopo Upanga ila nafundisha upande wa primary...
Kwa bandiko hili nikiwa najua kwa sasa walimu ni wengi sana hasa wa masomo ya sanaa lakini mimi najivunia uzoefu wangu na uwezo wangu katika kufundisha na kuendana na mifumo na utaratibu wa shule za binafsi..
Kwa sasa nimejenga kibanda changu huku Kibaha na ninaishi huku kwahyo inakuwa mzigo kwangu kutoka huku na kwenda kazini Upanga kila siku...Naomba kama kuna mwenye shule iwe ya sekondari au primary katika maeneo ya Kibaha....Kibamba....Mbezi...Kimara na maeneo ya karibu anayehitaji mwalimu wa kufanya kazi muda mrefu iwapo tutakubaliana masharti anipe kazi ili niwe karibu na kwangu na nifanye kazi kwa ufanisi ..
Kwa primary naweza kufundisha masomo ya Civics....History....Geography(social studies)....na English Language ...
Kwa sekondari nafundisha masomo ya history na civics/general studies
Ahsanteni
 
Shahada yangu ni ya Elimu katika elimu ya watu wazima na maendeleo ya jamii...kwahiyo hata vyuo au taasisi ambazo zinafundisha watu wazima ambao tayri wapo nje ya mfumo wa kawaida wa shule naweza kufanya kazi
 
Back
Top Bottom