Mwalimu mpya majanga!

unajua mashuleni kuna waalimu wanafiki kila wanachofanya wenzao wanapeleka kwa mkuu wa shule au mwl.mkuu. sasa mleta mada uko type hiyo. hujaombwa hela ya pombe achana naye... unataka avute kwa kujificha......huo ni unafiki...
what to do mpatieni chumba chake mwenyewe....mtu mzima haulizwi umetoka wapi.
 
Jamii tunayoishi imejaa kila aina ya mambo sio kila jambo liletwe ktk forums.Ina maana siku mkeo akipika maharage yasipoiva utaleta huku tukushauri nini?
ndugu yangu labda nikwambie kitu kimoja, nimesema kuwa huyu mwalimu ni mgeni katika kazi na isitoshe kazi yetu ya ualimu ina miiko yake. hebu turudi kwenye point lengo la mimi kuja hapa kuomba ushauri ni kutaka kupata njia sahihi za kumfanya huyu mwalimu awe kwenye utaratibu unaoeleka wala sikua na maana ya kumdharirisha mwalimu mwenzangu.
 
Jitahidi kumshauri,ndivyo tulivyo. Hata wataalam wa masuala ya tabia wanasema watu wote hatuwezi kuwa na tabia za aina moja (we cannot act on the same manner,otherwise dunia itakuwa very bored) hivyo ht hizo deviant behaviour unazozichukia bado zina mchango mkubwa sn kwa jamii. Therefore you can't force a person to behave the way you want, cha muhimu hapo ni kuvumiliana tu na siajabu nae akawa kuna mambo hayampendezei toka kwako/kwenu ndio maana anafanya hivyom
 

Mwalimu tena wa shule ya msingi bado una safari ndefu ya kupanga maisha yako tumia muda huu hata kujiendeleza kielimu kuliko kupiga majungu au umeridhika na hapo ulipo?
TAFAKARI
 
kwani hafundishi????????????..........................mwache mwenzio ale ujana maisha yenyewe yapo wapi
 
Lol bora pombe kuliko madem...asije ngoma bure.
 
ndani ya wiki moja mmefanya yote juu yake vikao, ushauri nk du nyie noma.
 

Acha ukiranja wewe,ukiranja unaishia shuleni,hiyo ni kaz kama kaz zingine,acha unoko wewe
 
Tafuteni mzee mmoja wa kimakonde, mpeni mkanda wote na elfu kumi hivi, then endeleeni na kazi zenu tu kwani kila akichelewa atakutana na simba mwisho wa siku ataacha kabisa pombe. Au unajifanya hujui sayansi mwitu a.k.a bluetooth za kiafrika?
 
Nakula ujana...yani ndio umenileta kunishitak jf?leo nakuvutia bangi ili unitambue vizuri
 
Mfanyieni mpango achonge funguo yake
 
Duh! fanya yako mwalimu, maisha mduara...
 

Umenikumbusha ile kauli ya Jesus Christ, kwa wale jamaa waliotaka kumponda mawe yule mwanamana ambaye walidai ni mzinzi, alipowaambia yeyote kati yao ambaye hajawahi kutenda dhambi yoyote maishani mwake, awe wa kwanza kumrushia jiwe yule mama, ghafla wale jamaa, mmoja baada ya mwingine waliondoka eneo hilo kimya kimya bila ya hata kuaga!
 
Wewe kama mlezi. 1 mshauri,2 mtahadharishe, 3 mpe muda kabla hujasambaza matatizo yake kihivi,waliokuteua wamekuamini.
 

Kiongozi,
1 Kwani Una mtoto kwenye darasa analofundisha jamaa?

2 Vipi akishatumia mmea na pombe huwa anakutembezea kichapo?

3 Jamaa huwa anakutengemea kifedha ili akidhi mahitaji yake au wewe unamtegemea yeye?

4 Hakuna uwezekano wa kutengana mahali pa kulala/nyumba?

Kama huwezi kubadili mienendo yake,badili mienendo yako wewe!
 
Kama ni mkurya achana nae fanya yako
 
Una mihemko ya kishoga shoga sana we dogo. Waarabu wamekuharibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…