Mwalimu Mkuu atuhumiwa kudhalilisha wanafunzi

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Mkuu wa Shule ya Sekondari Sale wilayani Ngorongoro, Ngunai Gidore ameingia katika uchunguzi kutokana na tuhuma zilizoelekezwa kwake akidaiwa kuwadhalilisha wanafunzi wake wa kike.

Taarifa kutoka katika shule hiyo ambazo hata hivyo zimekanushwa na Mwalimu Gidore akisema wanaozitoa wanamuonea wivu, zinadai kuwa kwa nyakati tofauti amekuwa akiwaita baadhi ya wanafunzi nyakati za usiku na kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji.

Hata hivyo, Kamishna wa Elimu nchini, Dk Lyabwene Mtahabwa alipotafutwa jana alisema ofisi yake haina taarifa ya suala hilo lakini itafuatilia kuanzia kwa Mdhibiti Ubora wa Elimu Kanda ya Kaskazini ili kama lipo, hatua ziweze kuchukuliwa.

Vitendo anavyodaiwa kufanywa na mwalimu hiyo ni pamoja na na kuwashurutisha kufanya nao ngono, kuwaingizia vidole sehemu za siri, kuchezea matiti, kuwatongoza na kutaka kuwakagua kama ni bikira.

Chanzo: Mwananchi
 
Huyo mkuu wa shule ana umri gani? Anajishughulisha na siasa? Ana miradi ya kumuingizia pesa nje na ajira yake ya ualimu? Ana ugomvi na yeyote awaye? Duh! Mwalimu kwa ujumla ana maadili ya ualimu na anajua kujihusisha kimapenzi na wanafunzi wake ni hatari kwa ajira yake na pia ni fedheha kwa kushusha heshima yake. Hiyo mikasa huwa ipo na huandiliwa kiufundi na maadui zake kama anao na anasigana nao katika mambo fulani kuanzia shuleni hadi nje ya shule. Haingii akilini baba mtu mzima afanyie wanafunzi wake vitendo hivyo labda awe amechanganyikiwa/kalogwa,/kapigwa kimbola. Maadui hupenda sana kupakazia kushikwa matiti, matako, nyeti kuingiziwa vidole wanajua hivyo vitu ni very sensitive kwa mwanaume mzima. Isije ikawa wanafunzi hao ndio wanamdhalilisha mwalimu wao. Tulio mashuleni tunajua jinsi mikasa hii inavyowakumba walimu. By the way hao wanafunzi kimakuzi ni watu wazima wanajitambua si rahisi kuvuliwa nguo na kuanza kufanyiwa vitendo hivyo wabaki wametulia tu
 
Mkuu wa Shule ya Sekondari Sale wilayani Ngorongoro, Ngunai Gidore ameingia katika uchunguzi kutokana na tuhuma zilizoelekezwa kwake akidaiwa kuwadhalilisha wanafunzi wake wa kike.

Taarifa kutoka katika shule hiyo ambazo hata hivyo zimekanushwa na Mwalimu Gidore akisema wanaozitoa wanamuonea wivu, zinadai kuwa kwa nyakati tofauti amekuwa akiwaita baadhi ya wanafunzi nyakati za usiku na kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji.

Hata hivyo, Kamishna wa Elimu nchini, Dk Lyabwene Mtahabwa alipotafutwa jana alisema ofisi yake haina taarifa ya suala hilo lakini itafuatilia kuanzia kwa Mdhibiti Ubora wa Elimu Kanda ya Kaskazini ili kama lipo, hatua ziweze kuchukuliwa.

Vitendo anavyodaiwa kufanywa na mwalimu hiyo ni pamoja na na kuwashurutisha kufanya nao ngono, kuwaingizia vidole sehemu za siri, kuchezea matiti, kuwatongoza na kutaka kuwakagua kama ni bikira.

Chanzo: Mwananchi
walimu wanafanya sana hivi vitendo kote nchini shida ipo kwenye kuwafukuza kazi tu wana vyombo 100 kidogo vinawalinda
 
Tamaa mbaya sana,unawezaje kumtamani mtoto mdogo? Halafu utasikia wanasema shetani alinipitia.
 
Back
Top Bottom