Mwalimu Mkuu ashushwa cheo kwa kushindwa kudhibiti walimu kuwaagiza wazazi kuku

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,720
55,858
jogoo.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Amani Mwenegoha amemvua wadhifa wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Silamila, Mashaka Lusotola na kumrudisha kuwa mwalimu wa kawaida.

Hatua hiyo ilikuja baada Mwenegoha kubaini kuwa walimu wa shule hiyo wamekuwa na tabia ya kuwaagiza kuku, wazazi wanaowaandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza.

Mwenegoha alichukua maamuzi hayo, baada ya kuthibitisha kuwa mwalimu huyo mkuu, ameshindwa kudhiti tabia hiyo ya walimu walio chini yake.

Akizungumzia kusimamishwa kwake, Mwalimu Lusotola alisema amefurahi na kufananisha adhabu hiyo na kumpiga teke chura.

Tayari mwalimu huyo amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupamaba na Rushwa (Takukuru), leo anatarajia kwenda kuandikisha maelezo, huku akisisitiza kuwa hajaomba kitu chochote kwa wazazi.
 
Dah hii nchi hatari sana yaani Head teacher alikuwa anakula kuku kutoka kwa wazazi.
Sijui ndio ya kila mbuzi kula kwa urefu wa kamba yake
 
Kuna haja ya Serikali kufuatilia kwa kina taarifa wanazopelekewa kabla ya kuchukua hatua.Kimsingi taarifa hii imepotoshwa kuliko ukweli wenyewe.

Kimsingi sakata hili ambalo linaonekana kama walimu waliomba rushwa ya kuku ili wawapokee watoto waliokuwa wanaandikishwa Darasa la kwanza si la kweli.

Kama vilivyo vijiji vingi,Silamila ni kijiji kilichopo Wilayani Bukombe Mkoa wa Geita,Kipo umbali wa takribani kilomita sita toka zilipo ofisi za Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kandokando ya barabara iendayo Katoro-Geita-Mwanza kupitia Lulembela.

Pamoja na kuwa karibu na mji wa Ushirombo-Bukombe,lakini wakazi wa kijiji hicho ni masikini na wanajishughulisha zaidi na Kilimo pamoja na kuponda mawe ya dhahabu katika machimbo madogo ya Ushirombo yajulikanayo kwa jina la NAMBA MOJA.

Chanzo cha tukio hili ni zoezi la uandikishaji wa watoto wa darasa la kwanza,katika kuitikia Sera ya "Elimu bure"wakazi wa eneo hilo walikuwa wanawapeleka watoto wao shuleni wakiwa wamewavalisha nguo zenye viraka zilizochoka na kuchanika.Ni watoto wachache sana walioripoti shuleni wakiwa na sare rasmi ya Shule.

Kutokana na hali hiyo ya watoto kuletwa wakiwa wamevalishwa nguo zilizochanika,ndipo walimu walipoanza kuwahoji kwa nini wameshindwa kuwanunulia watoto wao sare za Shule,wakati waraka wa Elimu bure umetoa ufafanuzi wa majukumu ya mzazi/mlezi kwa mwanae kuwa ni kumnunulia mwanae sare za Shule na madaftari,pamoja na kughalamia mlo wa mwanae awapo shuleni.

Wazazi walipopewa ufafanuzi huo,walijitetea kuwa wao ni mafukara na hawana uwezo wa kuwanunulia watoto wao sare za Shule wala madaftari.Kupata hela hadi wauze mazao na kipindi hiki hawana mazao kwa vile bado wapo kwenye Kilimo.

Waliendelea kusema kuwa njia pekee ya wao kupata hela ni kwa wao kuuza mifugo yao ikiwemo kuku na mbuzi,lakini hata hivyo wanunuzi wanawapunja kwa kununua mifugo yao kwa bei ya chini.

Kutokana na maelezo yao,Walimu wakawaambia sare za Shule na madaftari ya mwanafunzi wa darasa la kwanza vyote kwa pamoja havighalimu zaidi ya sh.5000/,wakawashauri wazazi kabla ya kuwapeleka Shule watoto wakiwa wamewavisha " masulupwete",wauze walau kuku mmoja ili waweze kuwanunulia watoto wao sare na daftatri.

Kumbuka walimu waliwashauri wakauze walau kuku mmoja wapate hela za kuwanunulia watoto wao sare na daftari na si kupeleka kuku shuleni ili watoto wao waandikishwe darasa la kwanza.

Kutokana na uelewa duni wa wakazi hao,waliuchukulia ushauri wa walimu kama kikwazo cha watoto wao kwenda Shule,ndipo baadhi yao walipeleka taarifa wilayani kuwa wamezuiwa kupeleka watoto wao Shule mpaka wapeleke kuku,jambo ambalo si la kweli na sicho walichoshauriwa na walimu.

Kutokana na Maelezo hayo ya upande mmoja,Mkuu wa Wilaya akamshusha cheo Mwl.mkuu.Huu ni mwendelezo wa kutoa maamuzi ya kukurupuka chini ya serikali ya wakurupukaji wakidhani wanawakomoa walimu kumbe mwisho wa siku jamii ndiyo itakayoumia kwa kukosa ushirikiano na walimu ambao ni viungo muhimu katika malezi na makuzi ya jamii husika.
 
sasa ilikuwaje mkuu wa wilaya akachukua maamuzi hata kabla ya mamlaka husika kuthibitisha kwamba huyu mtu anahusika na hayo maswala halafu inaonyesha kwamba kasikiliza upande mmoja bila kuwa na uthibisho. kwa hali hii basi wafanyakazi wa umma watakuwa wapo hatarini sana na hawa wanasiasa.
 
Well said serekali ya ccm inajenga mazingira magum sana kwa walim ,ila wasubiri ujira wataupata,walimu sio mbumbu
 
Huyo mwalimu alikuwa hajui sheria zinafanya kazi kwa maskini pekee!
View attachment 321796
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Amani Mwenegoha amemvua wadhifa wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Silamila, Mashaka Lusotola na kumrudisha kuwa mwalimu wa kawaida.

Hatua hiyo ilikuja baada Mwenegoha kubaini kuwa walimu wa shule hiyo wamekuwa na tabia ya kuwaagiza kuku, wazazi wanaowaandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza.

Mwenegoha alichukua maamuzi hayo, baada ya kuthibitisha kuwa mwalimu huyo mkuu, ameshindwa kudhiti tabia hiyo ya walimu walio chini yake.

Akizungumzia kusimamishwa kwake, Mwalimu Lusotola alisema amefurahi na kufananisha adhabu hiyo na kumpiga teke chura.

Tayari mwalimu huyo amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupamaba na Rushwa (Takukuru), leo anatarajia kwenda kuandikisha maelezo, huku akisisitiza kuwa hajaomba kitu chochote kwa wazazi.

Hakuna vyeo tangu nikiwa darasa la tano mpaka sasa navipuuza na sijawahi kuvisimamia ipasavyo kama vyeo vya kuteuliwa. unafanya kazi kama msukule. ukifanya tofauti na aliyekuteua tayari inakua shida. Nilikua sijui pia ya kuwa wakuu wa shule wanateuliwa na wakuu wa wilaya.

Haya yote yangemalizwa kwenye ile rasimu ya pili ya Tume ya Mabadiliko ya katiba ya Jaji Warioba. Sasa kilichotokea ni Mungu tu ndiye anayejua.
 
Back
Top Bottom