Mwalimu jela miaka 30 kwa kubaka mwanafunzi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela na kuchapwa viboko 24 Abed Rajab Mbuba (54), ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Shinji iliyopo Kijiji cha Shinji, kata ya Mbebe kwa kosa la kumbaka mwanafunzi.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Shughuli Mwampashi, alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Julai, 2019 katika maeneo ya kijiji Cha shinji kwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Shinji, huku akijua kufanya hivyo ni kosa na ni kinyume cha kifungu cha sheria namba 130 kifungu kidogo cha kwanza na pili E na kifungu cha 131.

Mwampashi alisema mahakama hiyo baada ya kusikiliza pande zote mbili, imeridhika na ushahidi upande wa mashitaka, na kumhukumu mtuhumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela na kucharazwa viboko 30 ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.

Awali Mwendesha Mashitaka, Peter Mrisho, aliomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa kwani vitendo vya ubakaji vimekithiri wilaya ya Ileje, ambapo husababisha kukatisha ndoto za wanafunzi kwa kuwapa mimba.

Akitoa utetezi wake, mshitakiwa alidai ana familia inayomtegemea, hivyo akihukumiwa familia itakosa mwelekeo, na kuiomba mahakama impunguzie adhabu.

Hata hivyo, Hakimu Mwampashi alitupilia mbali ombi hilo, na kuamuaru akatumikie kifungo cha miaka 30 jela na kuchapwa viboko 24.

NIPASHE
 
Mtoto wa darasa la sita wa Sasa unabaka wapi jmn? Yaani kabisa unapata hisia kwa mtoto wa darasa la 6.

Basi mboo itakuwa na akili kubwa ya ushawishi kuliko vichwa vyetu vya kawaida. Duuh!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom