Mwalimu jela miaka 3 kisa ufisadi

Mwalimu jela miaka 3 kisa ufisadi

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,247
Reaction score
25,191
Hukumu hiyo, ilitolewa na hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Hassan Momba, baada ya mwalimu huyo kukiri makosa ya ufujaji, ubadhirifu na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu akiwa mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.


Mwalimu huyo alifikishwa mahakamani Julai 28 mwaka huu na baada ya kusomewa mashtaka hayo mawili alikana, Ijumaa shauri hilo, lilipoitishwa kwa ajili ya usikilizwaji wa awali bila kushurutishwa, alikiri kutenda makosa hayo.


Hakimu Momba alitoa uamzi wa shauri hilo, kuwa kwa vile mshtakiwa ni mkosaji wa mara ya kwanza na anajutia kosa hilo, mahakama inamhukumu kwenda jela miaka mitatu ama kulipa faini ya Sh. milioni moja.


Awali upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Edson Mapalala, uliiambia mahakama kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo kati ya Agosti 2014 hadi Machi 2015 alipokuwa akikaimu nafasi ya mtendaji wa kijiji cha Itebulanda.


Mapalala alidai katika kipindi hicho, mshtakiwa akiwa ni mwajiriwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kama mwalimu mkuu na kaimu ofisa mtendaji wa kijiji cha Itebulanda alifuja Sh. 1,701,000, mali ya mwajiri wake.


Mapalala aliongeza kudai mwalimu huyo, alitenda kosa la ufujaji wa kiasi hicho cha fedha kwa kuwa zilikuwa chini ya umiliki wake.

Chanzo: Nipashe
 
vp alilipa faini au alienda jela? adhabu kama hizi ziliwafaa akina chenge na wenzake ingawa ni ndogo ila na wao wapate dispilin.
 
Back
Top Bottom