Mwalimu jela kwa wizi wa unga

Mwalimu jela kwa wizi wa unga

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,322


MAHAKAMA ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma imemhukumu kifungo cha mwaka moja gerezani mwalimu wa Shule ya Msingi Mtamba iliyopo katika Kata ya Rudi, Stephano Kuchera kwa makosa ya wizi wa vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kilo kumi za unga.

Kesi hiyo iliyokuwa ya rufaa kutoka katika Mahakama ya Mwanzo, Chipogolo ilitolewa hukumu juzi na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa, Pascal Mayumba. Mshitakiwa huyo ambaye alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi Mtamba alishitakiwa kwa kosa la kuvunja na kuiba mali kadhaa za Zena Hosea, ikiwemo redio moja, pasi ya mkaa na unga kilo 10.

Hakimu Mayumba alisema mshtakiwa huyo alifanya kosa hilo kinyume na kifungu cha Sheria Namba 273 C ya Kanuni ya Adhabu Sura Namba 16. “Kwa mujibu wa kifungu hicho cha sheria ambacho kinatamka wazi kuwa kama mtu aliyepatikana na hatia na kuvunja na kuiba adhabu yake ni kifungo cha gerezani, miaka 14 kosa la kuvunja na miaka saba na kosa la kuiba miaka saba,” alisema Hakimu Mayumba.

Alipotakiwa kujitetea, mwalimu huyo aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ana majukumu ya serikali pia na familia yake ikiwemo wazazi wake na watoto wa ndugu zake ambao anawasomesha na wanamtegemea pia ni kosa lake la kwanza.

Hakimu Mayumba alisema kutokana na mwenendo wa kesi mahakama inamhukumu kutumikia kifungo cha mwaka moja gerezani. Alisema kwa ambaye hataridhika na maamuzi ya mahakama anaweza kuipinga adhabu hiyo ndani ya siku 30.

Chanzo: Habari Leo
 
Afadhali wamempa huo mwaka mmoja, anatia huruma.... Walimu mjiongeze na nyie kweni na mambo ya ziada ya kuwaingizia kipato.
 
Habari kama hizi sizonje ndo anafurahi kweli...mana watumishi wa uma wakiteseka kama hivi kwa maisha duni kutokana na mishahara midogo ye ndo raha kwake....furahi mungu wa tanzania
 
Huyo inawezekana alikuwa mchepuko na walikorofishana so wanaonyeshana ubabe, kwa hali ya kawaida haiwezekani pasi ya mkaa,unga kilo kumi na radio vimfanye huyo bwana afungwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu watajiongeza wapi wakati mda wote maafisa elimu wanawabana wanataka wawaone shuleni..hii kazi ni bora ukishapata mtaji uachane nayo tu


Tatizo na sisi wa tz waoga mno na maisha,, tunaamini tusipoajiriwa hatujaishi bado. Kazi ya ualimu na ujira wake yataka moyo kwa kweli. Binafsi hujanishawishi.
 
Hapo hoja ni stephano kuchera kuiba unga kg 10, na sio kutake attention ya ualimu!
 
Huyo inawezekana alikuwa mchepuko na walikorofishana so wanaonyeshana ubabe, kwa hali ya kawaida haiwezekani pasi ya mkaa,unga kilo kumi na radio vimfanye huyo bwana afungwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mm naliona kwambalii huko ni kukomeshana hakuna kitu kibaya kumwambia mwanamke mm na ww bhash wakati yy anakuhitaji atakutafutia coz za kutokukuona tena au chuki yake anajua mungu hapo bibi zena ameshindwa ficha hisia zake akimuona mwl mhhh
 
Tatizo na sisi wa tz waoga mno na maisha,, tunaamini tusipoajiriwa hatujaishi bado. Kazi ya ualimu na ujira wake yataka moyo kwa kweli. Binafsi hujanishawishi.
Walimu wenyewe walivyowaoga sasa..utafikiri bila ualimu huwezi ishi
 
Back
Top Bottom