Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,443
- 40,537
Kuna dhana isiyo sahihi inajengwa miongoni mwa watanzania kwamba Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa Maskini kwa ivo ndiyo maana alikuwa muadilifu. Kwanza kwa wasiojua pamoja na Mwalimu kuwa Mtanganyika wa kwanza kusoma kwenye Chuo Kikuu Edinburgh cha nchini Uingereza, lakini pia alitoka kwenye koo ya kichifu.
Kwa viwango vyovyote vile vya watu wa Tanganyika wa zama hizo Mwalimu hakuwa ni miongoni mwa watu unaoweza kuwaita maskini. Mwalimu baadaye miaka ya sitini alijenga nyumba yake ya Msasani kwa Mkopo na alimjengea mama yake nyumba kutokana na fedha alizopata alipoacha kufundisha Pugu ili akafanye kazi za TANU. Mtu aliyeweza kulipa mkopo baada ya kuukopa huwezi kumwita maskini!
Mtu aliyekuwa analipwa shilingi mia tano (500) kwa mwezi zama hizo za miaka ya hamsini huwezi kusema kwamba alikuwa ni maskini na eti umaskini wake huo ndiyo uliomfanya awe muadilifu. Mwalimu hakupenda kutumia madaraka yake kujitajirisha lakini si kwa hoja kwamba kuwa alikuwa maskini bali uadilifu kwake ilikuwa ni sehemu ya imani yake!