Mwalimu apigwa risasi huko Tabora kwa kosa la kukojoa kwenye gari la mtu

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,734

POLISI wilayani Igunga mkoani Tabora inamshikilia mfanyabiashara kwa tuhuma za kumjeruhi kwa bastola aliyekuwa mwalimu wa Shule ya Msingi Saint Leo Ndugu Teophano Mvula.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamisi Selemani alisema tukio hilo ni la usiku wa Januari 15 mwaka huu katika baa ya Kibo iliyoko barabara ya Mwanzugi mjini Igunga.

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Igunga, Abdallah Ombeni amethibitisha kumpokea Mwalimu Theophano Mvula akiwa na jeraha kichwani ambapo alitibiwa kwa kushonwa nyuzi tatu na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Kamanda Selemani alimtaja mwalimu aliyepigwa risasi kuwa ni Teophano Mvula mkazi wa mtaa wa Nkokoto kata ya Igunga.

Aidha kamanda huyo alisema chanzo cha kupigwa risasi mwalimu huyo ni kujisaidia haja ndogo jirani na gari la mfanyabiashara huyo, Felix Peter Mselel (42) mkazi wa Nzega.

Alibainisha kuwa baada ya kumuona mwalimu katika gari yake, aliamua kumfuata na baadaye yalitokea mabishano, hali iliyofanya mfanyabiashara kuchomoa bastola na kupiga risasi hewani huku risasi ya pili akimlenga kichwani mwalimu huyo.

Alisema baada ya kupigwa risasi mwalimu alianguka chini ambapo wasamaria walimchukua na kumkimbiza katika hospitali ya wilaya ya Igunga.

Hata hivyo, Kamanda Selemani alisema tayari mshitakiwa amekamatwa pamoja na bastola yake ikiwa na risasi 10 ambapo anategemewa kufikishwa mahakamani wakati wowote ili kujibu tuhuma inayomkabili.

Aidha Kamanda Selemani ametoa mwito kwa kamati zinazojadili na kupitisha majina ya watu wanaoomba kumiliki silaha kuwa makini, kwani bila kufanya hivyo inasababisha kupewa silaha watu wasiokuwa na sifa za kumiliki silaha jambo ambalo ni hatari.

Mwalimu Teophano Mvula akizungumza kutoka hospitali hapo, aliomba serikali kuwa makini na utoaji wa silaha kwa baadhi ya raia.
 
Anacheza na na jasho la pesa,pole Mwalimu wangu ungekuwa unazo kama yeye ata ungekunya poa tuu
 
Pole mwalimu siku ilikuwa bado na umilikishwaji wa silaha uwe na umakin sana vinginevyo tutaumia hata tusio na hatia
 
Hyo kuna jamaa tulimpiga akajinyea na tukamng'oa jino!!yan alimkanyaga mshkaj afu jamaa akamuliza mbona umenikanyaga na uombi hata samahanj,mshkaj akamtukana afu akatutolea mkwasa!!na ukamanda wetu tukatulia tuli!!akatukana sanaa tumeuchuna tu!!kuna mwenzetu alikua kaenda toilet anarud analiona like picha bhas akamtime akadaka,tukainuka tukamvaa tukampokonya!!daaah tulichomfanya hasahau na kwa unaa tunapiga mbili hewan kuonesha alitaka kutuua!!pisto kanyang'anywa na mtaan alihama!!
 
Pole mwalimu siku ilikuwa bado na umilikishwaji wa silaha uwe na umakin sana vinginevyo tutaumia hata tusio na hatia
Huyu mwalimu ana makosa, sema aliyempiga risasi amejichukulia hatua mikononi mwake kwa kosa ambalo halikustahili kutumia bastola
 
Marehemu nyokaa aliteka mishkaki mitano kwa bastola alafu baada ya dakika kama kumi hivi akarudisha kwa muuzaji zile stick zilizokuwa zimechomekwa kwenye ile mishkaki.

Conrad alimshoot jamaa bar akamuua kisa ugomvi wa wanawake bar wakiwa wamelewa.

Bwana War bus aliteka kwa bastola daladala nzima ikiwa na abiria kwenye route kondakta ameambiwa akusanye simu za abiria wote na hela zote huku gari inaenda.

Haya matukio meengi kuliko yanayoripotiwa.
 
Kuna haja ya kuangalia namna vibali vya kumiliki silaha zinavyotolewa
 
Kwa nyie msio kunywa mnamuona ticha kama kituko. lkn kwa si wanywaji kukojoa karibu na gari wala sio issue kanisa, yaani unamshoot mlevi mwenzio kisa kakojoa karibu na gari yako kweli?, pumbufu kabisa Huyo jamaa akitoka jela tunamnyang'anya leseni ya unywaji na kumiliki bastola
 
Back
Top Bottom