Mwalimu amdunga mimba mwanafunzi wa miaka 13. RC ang'aka


Hivi punde

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Messages
1,865
Likes
4,507
Points
280
Hivi punde

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2017
1,865 4,507 280
Ofisa elimu mkoa wa Mara, Emmanuel Kisongo ametakiwa kumchukulia hatua mwalimu wa shule ya msingi Namubi wilayani Bunda kwa madai ya kumpa mimba mwanafunzi (13) ambaye amejifungua watoto pacha.


Mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima alitoa agizo hilo mbele ya kikao cha watumishi wa Serikali wa wilaya zote sita mkoani humo.


Kikao hicho kilichowahusisha wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, makatibu tawala, wakuu wa idara na taasisi za Serikali kilifanyika wilayani hapa lengo kilikiwa ni kuwakumbusha watumishi wajibu wao na kutatua matatizo ya wananchi.


“Mwalimu mpaka sasa hajawajibishwa, badala yake akasingiziwa mwanafunzi kuwa ndiyo kambebesha mimba tena mtoto yatima asiye na baba wala mama. Kiongozi anayeona kukaa Mara ni adhabu ahame matukio ya ukatili yanatokea lakini viongozi hamchukui hatua,” alisema Malima.


Mkuu wa wilaya ya Bunda, Lyidia Bupilipili alisema uongozi wa wilaya umeshachukua hatua kwa mwalimu huyo (jina linahifadhiwa) kwa kumfikisha katika vyombo vya dola ili hatua za kisheria zichukuliwe.


Ofisa elimu, Kisongo alisema mwanafunzi huyo alipewa mimba na mwalimu wake kisha akasingiziwa mwanafunzi wa darasa la saba (jina linahifadhiwa) kuwa ndiye aliyehusika kumpa ujauzito huo.


Kisongo alisema Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), William Kanon alisema mwanafunzi huyo tayari amejifungua watoto pacha.
Alisema tukio lingine limetokea Shule ya Msingi Nyamongo ambako mwanafunzi wa darasa la pili (8) alibakwa na mtu ambaye hajafahamika jina.


Kisongo alisema kuwa mama wa mtoto huyo (jina linahifadhiwa) aligundua mwanaye kubakwa Machi 22, 2017 na alikwenda kuripoti kituo cha polisi lakini hadi sasa anazungushwa bila kupata msaada wowote na hivyo taarifa kumfikia mkuu wa mkoa wa Mara.
 
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
18,033
Likes
53,034
Points
280
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
18,033 53,034 280
Haya mambo ya walimu na wanafunzi kuduu hayatakaa yaje yaishe
 
Evelyn Salt

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Messages
48,184
Likes
39,537
Points
280
Evelyn Salt

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2012
48,184 39,537 280
Ahamishwe kituo, amuoe, walee watoto....
Teachers na hizi teaching allowance duh hadi kwa vitoto!!! Sio sawa
 
Ugangaaa

Ugangaaa

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2017
Messages
287
Likes
345
Points
80
Ugangaaa

Ugangaaa

JF-Expert Member
Joined Nov 5, 2017
287 345 80
Mtoa mafa hili tukio limetikea zaid ya miez 6 nyuma kabla ya RC malima hajateuliwa kuongoza mkoa wa Mara na hatua zilisha chukuliwa ila kilichofanyika juzi ni kujitakatisha kisiasa kwa jambo ambalo lisha tolewa uamuzi.
 
Ugangaaa

Ugangaaa

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2017
Messages
287
Likes
345
Points
80
Ugangaaa

Ugangaaa

JF-Expert Member
Joined Nov 5, 2017
287 345 80
Pia ni rahisi sn kumponda na kumzungumzia mwl ww ukiwa siyo mwl.
 
cmases

cmases

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2015
Messages
968
Likes
560
Points
180
cmases

cmases

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2015
968 560 180
Mtoa mafa hili tukio limetikea zaid ya miez 6 nyuma kabla ya RC malima hajateuliwa kuongoza mkoa wa Mara na hatua zilisha chukuliwa ila kilichofanyika juzi ni kujitakatisha kisiasa kwa jambo ambalo lisha tolewa uamuzi.
Maana yake ni kwamba zilipendwa.
 

Forum statistics

Threads 1,250,458
Members 481,354
Posts 29,733,803