Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
MWILI wa mwalimu wa shule ya msingi Sirari, tarafa ya Inchugu, wilayani Tarime, mkoani Mara, Rose Gulinjwa umekutwa ukiwa ndani ya gari lake ukiwa umefungwa kwa vitambaa usoni, mikono, miguu na mdomo na mtoto wa miaka sita Jonathan Burugu akiwa hai.
Hata hivyo mtoto huyo alikutwa akiwa na alama za kamba shingoni ndani ya gari hilo ambalo linaonekana kutelekezwa maeneo ya mpakani ya Isebania nchini.
Chifu wa Isebania nchini Kenya Marwa Marioba alisema kuwa mwili wa mwalimu huyo uligundulika jana alfajiri na wananchi waliokuwa wakipita katika njia isiyo rasmi inayotoka Tanzania na kuingia nchini Kenya maeneo ya Mali ngumu ambapo waligundua mwili wa mwanamke ukiwa ndani ya gari lenye namba za usali T 733DNT ukiwa umefungwa mikono, miguu,uso na mdomo na pembeni kukiwa na mtoto wa kiume na kutoa taarifa kituo cha polisi Isebania.
Wananchi hao pia walitoa taarifu kwa wakazi wa mji wa Sirari akiwemo diwani wa kata ya Sirari Nyangoko Paulo na Mtendaji wa kata ya Sirari Mirumbe Wakuru ambao walifika na kuutambua mwili wa mwalimu huyo na wananchi.
Diwani wa kata ya Sirari Nyangoko Paulo alisema wamesikitika kumpoteza mwalimu huyo .
Ofisa Mtendaji wa kata ya Sirari Mirumbe Wakuru amesema kuwa wenyeviti wa vitongoji na vijiji katika mji huo wa Sirari wameshapewa maelekezo na serikali kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi katika kila kijiji ili kuimarisha ulinzi.
Kaka wawili wa marehemu Rose waliojitambulisha kwa majina ya Albert Gulinjwa na Elisha Gulijwa waliongozana na polisi wa Isebania kusindikiza mwili wa marehemu kwenda hospitali ya Migori nchini Kenya kufanyiwa uchunguzi.
Habari Leo