Mwalimu akamatwa na viroba vya shilingi milioni 77

Mwalimu akamatwa na viroba vya shilingi milioni 77

Mjamaa masalia

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2012
Posts
373
Reaction score
354
Mwalimu akamatwa na viroba vya shilingi milioni 77

MWALIMU wa shule ya sekondari ya St Margareth wilayani Igunga amekamatwa na boksi za pombe aina ya viroba 825 akiwa amevihifadhi katika duka lake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Hamisi Selemani alimtaja mwalimu aliyekamatwa na maboksi hayo kuwa ni John Pastory (48).

Kamanda Selemani alisema mwalimu huyo alikamatwa Machi 7, majira ya saa 5 asubuhi katika mtaa wa Mwayunge mjini Igunga.

Alisema baada ya jeshi la polisi kufanya upekuzi walifanikiwa kukamata vioroba hivyo vyenye thamani ya sh 77,136,000.

Aidha kamanda Selemani alisema mwalimu huyo ndiye alikuwa msambazaji mkubwa wa pombe aina ya viroba wilaya ya Igunga.

Nae mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mwayunge kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, Abel Shampinga alilipongeza jeshi polisi kwa kuwakamata wauzaji wa pombe za viroba na kuongeza kuwa yeye kama mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mwayunge hayuko tayari kuwatetea watu wanaovunja sheria za nchi
 
mfano wa kuuza viroba vilivyokatazwa??
Nadhani mfano ni kuwa mwl alikuwa mjasilia mali kuliko ilivyo walimu wengi wanategemea mshahara na kutwa wanalalamika mshahara mdogo.
Inamaana hii biashara isingekatazwa mtaji wake ungezidi kukua na kupata faida kubwa zaidi.
 
Waige kuuza viroba?,
Hoja yako imeakisi uwezo wako wa kufikiri,
Kichwa chako ni cha kufugia nywele tu.
 
Walimu ni wajasiriamali asikwambie mtu, ndio kada pekee ya utumishi wa umma kuendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda!
 
Mungu awanusuru wanafunzi Wa St Margreth,,
Maana stock ya hiyo mwalimu ingewahusu pia,,
 
Mm nadhani serikali imefanya haraka sana kufungia hii biashara kama madhara mbona sigara inaendelea kuuzwa wakati hizi ndio zenye madhara zaidi inaanza kwa mvutaji mazingira na ata asievuta anaasirika ila wamefunga viroba basi fungieni na sigara
 
Mwalimu mnjanja huyu, atakuwa alikuwa hali lii mshahara mdogo!
 
Hili katazo la pombe viroba sijalielewa kila siku nasikia na kuona kwenye tv polisi wakitangaza kunasa pombe hizo baada ya maelezo mwisho wake kuna kauli wanatoa kuwa ziendelee kuhifadhiwa kusubiri maelekezo nauliza wote waliohifadhi hizo pombe walizipata kihalali au kwa njia ya panya maana wanashupaliwa kama watuhumiwa wa ujambazi wanavyotangazwa nisaidieni
 
Hili swala lilivyoendeshwa limenifanya nijisikie aibu kuitwa mtanzania. Ovyo kabisa. Na watu wenye stock kubwa ka huyu wamekaa tu wameshindwa la kufanya. Ilitakiwa waidai serikali ilipe. The only reason ya kujificha ni kama alikua hajasajiri biashara au anakwepa kodi.
 
Mm nadhani serikali imefanya haraka sana kufungia hii biashara kama madhara mbona sigara inaendelea kuuzwa wakati hizi ndio zenye madhara zaidi inaanza kwa mvutaji mazingira na ata asievuta anaasirika ila wamefunga viroba basi fungieni na sigara
Kwan wamefungia au wanataka ubadilishaji wa packaging
 
Back
Top Bottom