Mwalimu wa shule ya msingi anusurika kuachwa na mpenzi wake

kibovu

JF-Expert Member
Apr 17, 2017
661
686
Igweeeeeeee

Kuna dada mmoja ni rafiki yangu nimesoma nae masomoni china alikuwa na boy friend wake mwalimu wa shule yamsingi.

Stori iko hivi wadau mwalimu wa shule ya msingi amezaliwa mkoani tabora akiwa mtoto wa kwanza katika familia yao ya watoto wanne,Marehemu baba yake ni mstaafu wa katka kazi ya ualimu na mama yake ni mama wa nyumbani . Baada ya kumaliza masomo yake ya ualimu wa shule ya msingi baba yake alifariki hivo kijana akawa na jukumu lakutunza familia yake .

Kiukweli kijana amepambana sana huku na kule kuhakikisha wadogo zake wanapata elimu na mama yake akiishi maisha mazuri huku yeye mwalimu akiwana maisha ya kawaida saana yaani alikuwa na kitanda na Godoro tu.

Mdogo wake anaemfuata mwalimu alisoma mpaka chuo kikuuu akapata kazi katika taasisi moja ipo chini ya wizara ya madini mshshara mnono kwani alifanya kazi miezi mitatu akanunua ndinga wakati huo mwalimu nae alianza kujiendeleza kusoma diploma.
Mwalimu alijiendeleza masomo yake na huku akiwaendeleza wadogo zake wakichangishana na dada yake aliyeko madini. hatimae nao pia walifika vyuo vikuuu na kumaliza masomo yao .

Mnamo mwaka 2018 Mwalimu alimaliza masomo yake ya shahada ya kwanza. Mwalimu alianza kupambana maisha yake hakuna alichokifanya zaidi ya kusomesha wadogo zake na kumsaidia mama yake kila mwezi pesa isiyopungua elfu 50 kwa ajili ya kujikimu kwa maisha yake yote mwalimu mpaka alipo fika hapo.

Pamoja na yote hayo mwalimu nae ni binadamu kwani alipenda kila weekend kwenda kupata moja mbili tatu bar ambayo iliyo changamka huku akikumbatia viuno vya warembo na akiwa na kitu cha thamani kitanda na Godoro tu pamoja laptop na jiko la gesi na alikuwa akijipenda hivo aliishi chumba cha self.. katika mapito yake yote hayo mwalimu alikuwa akiendelea na mahusiano na huyu dada Tina niliyesoma nae china

Mwalimu katika ukoo wao baba yake mdogo ni mkurugenzi mkuuu tataasisi moja iliyo chini ya wizara ya elimu mwalimu alimuomba msaada sana baba yake huyo ili amtoe kwenye ualimu lakini jitihada za mwalimu ziligonga mwamba ndipo mwalimu alianza kupambana taratibu bila hata mtu yeyote kujua

Mnamo mwaka 2019 mwalimu alipata scholarship ya mafunzo ya muda mfupi uingereza kwa muda wa mwezi mmoja .Mwalimu alienda na liaga ndugu na marafiki na yule baba yake mdogo aliyepo wizarani elimu alishangaa saana mwalimu aliyepo shamba kupata nafasi hiyo pia hata maafisaa wa Halimashauri walishangaa sana .

Mwalimu alienda na kurudi na kupokelewa Airport na mpenzi wake Tina ambae alikuwa kwa wakati huo yupo pia Tanzania walienda hotelini kwa sababu hawana chumba pale mjini Dar es salaam ,Tina anaishi kwao na mwalimu anafanyia kazi Geita.

Tina aliniomba ushauri sana juu ya kuachana na mwalimu kwani alimuona ni mtu asiekuwa na future .Nilimuuliza Tina moyo wako unakuambiaje kuhusu mwalimu .Tina alinijibu moyo unaniambia mwalimu ana kitu kikubwa anahitji mtu wa kumpush kidogo tu atafika mbali.Nilimsihi na kumuambia mtie moyo mwalimu ana nyot mtafika mbali .Tiina alinikumbatia na alilia na kuniambia atafunga na kuomba kwa ajili ya mwalimu .

Mwalimu safari yake ya uingereza alipata posho kama Tsh milioni 3 lakini kutokana na maisha ya mwalimu yalivo alikuwa na madeni makubwa na kumbuka alifikia hotelini na Tina na kuishi hotel siku 10 ,Hivo alilipa madeni na kubakia hana hata mia.

Mwalimu alienda kukopa kwa hawa watu unaacha kadi ya atm na akaanzisha NGO Apo kwa mda wote akiwa hana kitu zaidi ya kitanda ,Godoro ,Jiko la gesi ,Pasi,Begi na Pc.

Na mwalimu alikuwa bize kuandika proposal kuomba msaada kwa ajili ya NGO yake , Kilio cha mwalimu kilisikika alipata ma Donor walimpa Gari tatu pamoja na feza nyingi tu za kuendesha miladi katika ngo yake.

Mwalimu alimuita Tina akamuambia umenivumilia muda mrefu Agost tuna funga ndoa ,Tina kapelekwa shopping na mwalimu last moth ambayo hajawahi mfanyia tangu wameanza mahusiano na kumuachia cash usd 2000 kwa ajili ya mambo yake.

Tina baada ya apo aliniita na kuongea na mimi huku akilia na kunishukuru kwani alitaka kumuacha mwanaume wa ndoto zakeina na watu walimcheka sana kuwa na mahusiano na mwalimu asiekuwa na kitu kazi yeye mwalimu ulikuwa mda wote yeye na laptop .Tina wadau alininunulia suti na viatu kama asante wa kumpa ushauri mzuri.

Mpaka sasa tunavooongea mwalimu ni habari ya mjini kawa mtamu ni bosss ana kila kitu unachokijua kamwe usimzalau mtu anayesimamia ndoto zake
,
 
"kamwe usimdharau mtu anayesimamia ndoto zake". Kumbe mkuu kwa habari za Law of Attraction huu pia ni moja ya mfano wake?.
 
Hii story niliishaisoma Instagram kwny page ya simulizi_tz, na aliyeisimulia ni dada
 
Back
Top Bottom