Mwakyembe: Wizara yangu imefanikiwa kuwatisha mafisadi na wezi wa mali za umma

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
1,808
2,000
WAZIRI wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe, ameeleza jinsi wizara yake ilivyofanikisha kuwatisha mafisadi kuacha wizi wa mali ya umma wa mabilioni.

Aidha, Dk. Mwakyembe amefafanua maboresho ya huduma za mahakama ndani ya mwaka mmoja uliopita wa uongozi wa Rais John Magufuli.

Dk. Mwakyembe, katika mahojiano maalum wiki iliyopita, alisema kuanzishwa kwa Divisheni Maalum ya Makosa ya Rushwa na Ufisadi katika Mahakama Kuu kumewatisha mafisadi.

"Tulipokuwa tunaandaa utaratibu wa kurekebisha Sheria ya Uhujumu Uchumi ili chini yake tuanzishe divisheni hii ya Mahakama Kuu, matukio mengi ya rushwa, wizi, ujangili, ubadhirifu nchini yalikuwa ya mabilioni ya fedha," alisema.

"Kuadimika kwa kesi kubwa toka Makahama hii ianzishwe rasmi mwezi Julai mwaka 2016 kunatoa tafsiri ya mafanikio makubwa ya mabadiliko ya sheria tuliyofanya; kwamba tayari mabadiliko tuliyoyafanya yamewaogopesha wezi wote, wazoefu na wapya.

Naomba nisisitize kuwa haya ni mafanikio," aliongeza Dk. Mwakyembe.

Mwakyembe alizungumzia mafanikio ya wizara yake akijibu moja ya maswali ya Nipashe juu ya utendaji wa Wizara ya Katiba ya Sheria katika mwaka mmoja tangu Magufuli aapishwe kuwa Rais wa Tano, Novemba 5, 2015.

Mbali na kuanzishwa kwa divisheni hiyo maarufu kwa jina la Mahakama ya Mafisadi, Waziri huyo aliyataja mafanikio mengine ya wizara yake kuwa ni kuanza kutengwa kwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa mahakama za mwanzo na za walaya, kutatuliwa kwa changamoto ya mrundikano wa kesi na mapambano dhidi ya rushwa kwa watumishi wa mahakama.

Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano hayo na Dk. Mwakyembe.

Swali: Wizara imekumbana na changamoto zipi tangu uteuliwe kuiongoza na Rais Magufuli?

Jibu: Changamoto ni nyingi, pengine nikutajie chache tu zenye uzito wa pekee: Rushwa katika mfumo mzima wa utoaji haki, huduma ya utoaji haki kuwa mbali na Watanzania walio wengi, mrundikano wa kesi mahakamani, ugoigoi mkubwa katika upelelezi, madai ya ubambikizwaji kesi kwenye vituo vya polisi, ucheleweshaji mkubwa wa nakala za hukumu na mienendo ya mashtaka, upotevu wa mafaili ya kesi kwa miaka mingi, malalamiko mengi ya uonevu kwenye mabaraza ya ardhi na nyumba, faida na hasara za kuendelea kuwa na washauri wa mahakama kwenye mfumo wetu wa utoaji haki.

Swali: Kabla hatujaziangalia kwa kina baadhi ya changamozoto ulizozitaja, zinatatulika kweli changamoto hizi Mheshimiwa Waziri?

Jibu
: Zinatatulika vizuri tu.

Sisi chini ya Jemedari Mkuu, Rais John Pombe Magufuli, tumejipanga kisawasawa na tumedhamiria kuipa sheria sura mpya kabisa ndani ya miaka hii mitano ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Na tayari tumeshaanza kama nilivyotangulia kueleza kuhusu uanzishwaji wa Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi na utungaji sheria kufanikisha mapambano dhidi ya ufisadi.

Swali: Watanzania wengi bado wanaishi mbali na maeneo yenye huduma za utoaji haki, hususan mahakama. Mfupa huo mnaukabili vipi?

Jibu: Katika dhana ya kila mtu kufikiwa na huduma ya utoaji haki (access to justice), kila kata nchini inatakiwa iwe na mahakama yake ya mwanzo. Lakini hali si hivyo.

Tuna kata 3,957 kwa takwimu za Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana. Na kati ya kata hizo 3,957, ni kata 976 tu zenye mahakama za mwanzo, yaani asilimia 24.6 tu ya kata tulizonazo.

Picha hii si nzuri hasa kwa Taifa letu lenye misingi imara ya haki, usawa na umoja. Kukosekana kwa miundombinu ya mahakama katika zaidi ya asilimia 75 ya kata, ni changamoto kubwa ambayo Serikali ya Awamu ya Tano inaitambua na tunaifanyia kazi kwa kuelekeza rasilimali zaidi za nchi katika ujenzi wa miundombinu ya mahakama.

Mathalan katika miaka hii miwili ya fedha yaani 2015/16 na 2016/17, tuna jumla ya Sh.bil 48.3 kujengea mahakama 40, yaani mahakama kuu nne, za mikoa sita, za wilaya 14 na za mwanzo 16. Tunao mkopo toka Benki ya Dunia ambao sehemu yake vilevile itatumika kujengea baadhi ya mahakama zetu mpya.

Vilevile tumeendelea kuhamasisha wadau mbalimbali kuchangia ujenzi wa mahakama bila masharti na kwa kutumia teknolojia ya ujenzi imara lakini wa gharama nafuu uitwao Moladi.

Ilikuwa faraja kubwa sana kwangu Jumatatu Desemba 19, 2016 kukutana na uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam ambao ulikubali kuchangia juhudi za Wizara kwa kujenga mahakama 20 Dar es Salaam ndani ya miaka hii miwili kwa kuzingatia vipimo na michoro rasmi ya Mahakama ya Tanzania.

Kwa mwendo huu, kasi, nguvu na azma tuliyonayo, tutabadilisha kabisa picha ya miundombinu ya mahakama nchini.

Swali: Ujenzi wa miundombinu bora na ya kutosha ya mahakama ni jambo moja, na uendeshaji wa mashauri kwa ufanisi ni jambo jingine. Matizo ya mrundikano wa mashauri mahakamani na uchelewaji mkubwa wa upelelezi wa mashauri, mtayatatua vipi?

Jibu: Matatizo hayo yanasababishana. Ucheleweshaji wa upelelezi huzaa ucheleweshaji wa mashauri mahakamani ambao vilevile husababisha mrundikano wa mashauri mahakamani. Hii ni changamoto kubwa kwani haki iliyocheleweshwa, ni haki iliyokataliwa, yaani 'Justice Delayed is Justice Denied'.​

Ni katika muktadha huo tumeamua kuyatatua matatizo hayo kwa pamoja. Mahakama ikaanzisha mkakati maalum wa kupunguza na hatimaye kuondoa kabisa mrundikano wa kesi "zero case backlog" kwa mahakimu na majaji kujiwekea idadi mahsusi ya kumaliza kesi mbele yao kwa mwaka, yaani: Hakimu Mahakama za Mwanzo kesi 260; Hakimu Mahakama za Wilaya na za Hakimu Mkazi kesi 250; na Majaji wa Mahakama Kuu kesi 220.

Hii zero backlog campaign ya mahakama imesaidia sana kupunguza mrundikano mkubwa uliokuwapo wa mashauri mahakamani kwani miaka mitatu tu iliyopita zaidi ya 60% ya kesi zilizokuwapo mahakamani, zilikuwa kesi za zamani, tofauti na sasa ambapo kesi za zamani ni asilimia 15 tu.

Hadi kufikia mwisho wa mwaka 2016, Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani zilijipangia kumaliza mashauri yote yenye umri zaidi ya miezi 24, Mahakama za Wilaya na za Hakimu Mkazi mashauri yote yenye umri zaidi ya miezi 12 na Mahakama za Mwanzo mashauri yote yenye umri zaidi ya miezi sita.​

Kila Jaji au Hakimu atapimwa kwa idadi ya kesi za muda mrefu alizobaki nazo mwishoni mwa mwaka. Wenye kesi zenye umri zaidi ya ukomo uliowekwa, wana wajibu wa kujieleza, waeleweke.

Kwa upande wa upelelezi, mbali na kuwahimiza Polisi na Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa) kuongeza kasi na weledi kupitia Jukwaa la Haki Jinai linalowakutanisha pamoja viongozi wote wa vyombo vinavyohusika na Haki Jinai, tumewaboreshea wapelelezi mazingira ya ufanyajikazi kwa kutunga sheria ya kulinda watoa taarifa na mashahidi, sheria ambayo muda si mrefu toka sasa itaanza kufanya kazi baada ya kuitungia kanuni.

Swali: Ipo vilevile changamoto ya ucheleweshaji mkubwa wa nakala za hukumu na mwenendo wa mashtaka kutoka mahakamani na hivyo kuwanyima wafungwa haki yao ya kikatiba ya kukata rufani wasiporidhishwa na hukumu zilizowatia hatiani.​

Hili mnalitatuaje?

Jibu
: Ni kweli hali ilikuwa hivyo awali, lakini katika kipindi hiki cha mwaka moja tumeshirikiana vizuri sana na Mahakama kuitafutia dawa.

Nimeshazunguka kwenye magereza zaidi ya 15 kwa nyakati tofauti, suala la ucheleweshaji wa nyaraka za mashauri halijitokezi tena kwa nguvu kama awali na sehemu nyingi, wafungwa na viongozi wa magereza wanakiri kuwa hali ni nzuri zaidi sasa.
 

Majestic wolf

JF-Expert Member
Feb 10, 2015
1,245
2,000
Kuwatisha sio lugha nzuri...ila kama kesi za kifisadi na rushwa zimepungua ni dalili nzuri..thumbs up
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,828
2,000
Nadhani yale madawa ya India bado ni tatizo kichwani! This can not be a statement from a PhD holder, obtained from a renowned University like Dar Es salaam in those days!
 

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,481
2,000
Kwa umri huu naona haya sijui nikijaaliwa miaka mingine 10 itakuwaje!? Tz doctors and PhDs
 

Pakawa

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
6,357
2,000
Hizi PhD zingine hizi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Inashangaza sana hakuna tofauti na yule ambaye hakusoma hata darasa la kwanza. Inatia kinyaa kusikiliza au kusoma waziri anajibu kama nchi ni yake majibu mbofumbofu tu! Tutafika kweli?
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
33,638
2,000
Kuwatisha sio lugha nzuri...ila kama kesi za kifisadi na rushwa zimepungua ni dalili nzuri..thumbs up
Amtishe nani, ukweli ni kuwa hela iliyopo ni chache kiasi haifai kuiba, kumbuka hela iliyokuwa ikifisadiwa sana ni ya wafadhili na sasa hivi wafadhili wamepewa lugha za shombo wametupotezea. Pia hao wachache hawajulikani maana hakuna ruhusa kutangaza mambo hayo. Na hata kama kuna mafisadi serekali itajuaje wakati hili la kupanda kwa umeme likikuwa wazi na bado hawajui?
 

Majestic wolf

JF-Expert Member
Feb 10, 2015
1,245
2,000
Amtishe nani, ukweli ni kuwa hela iliyopo ni chache kiasi haifai kuiba, kumbuka hela iliyokuwa ikifisadiwa sana ni ya wafadhili na sasa hivi wafadhili wamepewa lugha za shombo wametupotezea. Pia hao wachache hawajulikani maana hakuna ruhusa kutangaza mambo hayo. Na hata kama kuna mafisadi serekali itajuaje wakati hili la kupanda kwa umeme likikuwa wazi na bado hawajui?
Kwa hiyo mafisadi sasa hivi hakuna kwa sababu hela hakuna?
 

pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
10,910
2,000
Waziri wangu Mh. Mwakyembe, linda heshima yako;
  1. Wezi wa escraw
  2. wezi wa eppa
  3. wezi wa bandarini
  4. wale wauaji wote wa tembo
  5. wezi wa milioni 7 kwa dakika
  6. wezi wa mishahara ya wafanyakazi hewa
  7. wezi wa lugumi
  8. wezi wa mikataba ya hovyo waliyoingia na leo ni hasara kubwa kwa taifa
Mh. Mwakyembe ukitusaidia hiyo mijitu hapo juu itangulie MAHAKAMA ya MAFISADI tutapiga MAKOFI
 

Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,289
2,000
Huyu jamaa hana maadili km lile liprofesa la cuf. Mwansheria anajivunia kuwatisha masifadi na si kuwashitaki, kuwanyang`anya pesa na kuwasukumiza lupango.Ndio maana huwa nashangaa hizi phd na waafrica
 

Batale

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
1,113
2,000
Kumbe alianzisha mahakama kutisha watu, mi nilifikiri kuwakamata na hatimaye kuwatia hatiani? . Hiki ni kionja kingine.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom