Mwakyembe Wacha unafiki! Uthibitisho ulionao peleka Mahakama ya Mafisadi Lowassa ahukumiwe

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,943
18,665
59e481c6dd8d808fb9a236189ef0de87.jpg

Watanzania tumeishazoea mauongo yenu. mnatuona sisi mafala sana. Mlifungua mahakama ya mafisadi kwa mbwewe mpaka leo hakuna lolote lililofanyika juu ya mafisadi ambao mnashinda nao na kucheka nao.

Watanzania tungekuelewa kama uo uthibitisho ungeupeleka mahakama ya mafisadi.

Bunge unawezaje kulithibitishia kama sio kutupotezea muda kama mlivyofanya 2008? Watanzania mafisadi tunawajua tena na wewe ukiwemo.

Je, Ukishalithibitishia bunge kuwa lowassa ni fisadi, sisi Watanzania tutanufaika na nini? Pesa alizokwiba atarudisha? Bunge litamhukumu?

Acha utoto aseee. Peleka uthibitisho wako Mahakamani. Au mpelekee mtumbua majipu amtumbue kama anaubavu.
 
Kesi ya mafisadi imekosa watuhumiwa hadi hao akina Mwakyembe wakashusha kiwango cha pesa unazotuhumiwa nazo hadi kufikia milioni 400, na bado wamekosekana watuhumiwa!
 
Miongoni mwa PhD holders ambao walirukwa na akili muda mchache baada ya kutunukiwa PhD zao ni huyu. Yaani ni bonge la hasara ambayo haijawahi kutokea hapa nchini kwa PhD holder ambao PhD zao ni halali. Kwa wale ambao PhD zao si halali hawahusiani kabisa na comment yangu. Hivyo sitegemei kuona Noah nyeusi ikinifatafata.
 
Huyo ana laana ya mabebewa hewa.mwakyembe ni shetani,jehanamu hayupo na kuzimu wanamtafuta ! Hivi, elimu gani alifuata huko chuo kikuu? Mbona hakuelimika? Waliofagia chuo kikuu au hata kupalilia Maua tu wameelimika,na wana akili sana kuliko mwakyembe.huyu toeni kabisa mwenye idadi ya wasomi.anajidhalilisha tu kama nape !mnalishwa nini huko ccm Jamani ? Mbona mnapoteza,fahamu za kiutu ?
 
Siku Mwakyembe alipolia kinafiki bungeni kwenye ule msiba wa Samuel Sitta , hata mbumbumbu walimfahamu tabia yake .

Huyu mtu ni msanii wa kiwango cha chini sana !
 
59e481c6dd8d808fb9a236189ef0de87.jpg

Watanzania tumeishazoea mauongo yenu. mnatuona sisi mafala sana. Mlifungua mahakama ya mafisadi kwa mbwewe mpaka leo hakuna lolote lililofanyika juu ya mafisadi ambao mnashinda nao na kucheka nao.

Watanzania tungekuelewa kama uo uthibitisho ungeupeleka mahakama ya mafisadi.

Bunge unawezaje kulithibitishia kama sio kutupotezea muda kama mlivyofanya 2008? Watanzania mafisadi tunawajua tena na wewe ukiwemo.

Je, Ukishalithibitishia bunge kuwa lowassa ni fisadi, sisi Watanzania tutanufaika na nini? Pesa alizokwiba atarudisha? Bunge litamhukumu?

Acha utoto aseee. Peleka uthibitisho wako Mahakamani. Au mpelekee mtumbua majipu amtumbue kama anaubavu.
Uthibitisho Mh. Mwakembe aliutoa bungeni na hukumu ikatolewa ikawa ndio mwisho wa kesi. Kuupeleka mahakamani ingetokea kama Bunge lingeamua kuwa pamoja na kuvuliwa uwaziri mkuu pia aburuzwe mahakamani. Sasa huyu Nasari alipoibua upya suala la Lowasa na Richmond ndio Mwakembe kasema ikiwa Nasari au mbunge yeyote atapeleka hoja bungeni ili kashfa ijadiliwe upya basi yeye Mwakyembe atatoa ripoti upya na bunge litoe uamuzi upya. Ila Mwakembe anaamini Lowasa hatapona itakuwa aibu na adhabu squared. Tusubiri mwenye moyo wa kishujaa apeleke hoja bungeni
 
Huwezi kuamini kwamba huyu bwana miezi michache iliyopita alikuwa waziri wa sheria na katiba,mwanasheria mkuu wa serikali na DPP walikuwa chini yake,alikuwa ana uwezo wa kuagiza kesi ipelekwe mahakamani

Anasema ana ushahidi na mashahidi anao!!
 
Back
Top Bottom