Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,067
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amewataka vijana kutumia muda wao kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu badala ya kupoteza muda wao mwingi katika mitandao ya kijamii kwa kuwa kusoma vitabu ndiyo msingi mzuri wa elimu.
Alitoa kauli hiyo juzi jijini Dar es Salaam wakati alipozindua Kitabu cha “Colour of Life” kilichoandikwa na Mwandishi Ritha Tarimo, ambako katika hotuba yake alisisitiza suala la vijana kujenga utamaduni wa kupenda kusoma vitabu ili kukuza elimu yao.
Dk Mwakyembe alieleza kuwa baadhi ya vijana siku hizi wamekuwa wakitumia muda wao mwingi katika mitandao ya kijamii badala ya kujisomea, hivyo amewashauri wajifunze kutoka kwa mwandishi wa kitabu hicho ili waje kuwa waandishi hodari wa kutegemewa na Taifa.