Euphransia
JF-Expert Member
- Jan 26, 2017
- 937
- 778
Wadau juzi wakati Bw.Mwakyembe anaapishwa aliwaambia waandishi wa habari kuwa ripoti ya tume ya kuchunguza sakata la kuvamia clouds FM lililofanywa Na Mkuu wa Mkoa wa DSM Bw.Makonda haijakamilika Kwa sababu Bw.Makonda hajapewa nafasi ya kujieleza mbele ya Tume. Napenda kumkumbusha Bw.Mwakyembe wakati anaongoza tume ya Richmond aliiwasilisha Ripoti bila kumhoji Mh.Lowassa, mpaka wakati Mh.Lowassa anatangaza kujiuzulu alihoji.Bw.Mwakyembe Mungu anakumbuka sana matendo ya kila mja wake Kwa Makonda ripoti haijakamilika ila Kwa Mh.Lowassa bila kumhoji uliiwasilisha .