Mwakyembe tufahamishe kwanini DStv haipewi ruhusa kuonesha chaneli za ndani?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,797
71,217
Tukiwauliza DStv kwa nini hawaweki channel za habari za kitaifa kama ITV, Star Tv na Channel ten wanatujibu kuwa hawajapewa kibali toka mamlaka husika TCRA chini ya Wizara ya Habari kurusha.

Vipo vituo kama TV E na Clouds ambavyo vipo DStv lakini hivyo vituo ni vya burudani sio kwa ajili ya hard news za uhakika.

Tumuombe Waziri Mwakyembe aingilie kati suala hilo maana familia kumiliki ving'amuzi viwili au vitatu eti kwa ajili ya kupata channel za ndani ni mambo yaliyopitwa na wakati.

Mbona wenzetu Kenya wameshavuka huko? Uwezo wa kupata habari moja toka vyanzo vingi inasaidia kupanua uwezo wa kiakili wa RAIA wafuatiliaji.

Waziri Mwakyembe ingilia hili
 
Tumepigwa life ban kila kona.

Ukitaka kuangalia taarifa za habari basi uwe na king'amuzi cha ndani either startimes, azam n.k.


Ukitaka kuangalia mechi za kimataifa basi uwe na dstv.

Ndio maana mwisho wa siku wagombea wa upinzani wanaenguliwa kibabe, maaaana.........


 
Mzee wa digrii 4 hawezi kuyajua hayo?
Kweli hakuna uhusiano kati ya elimu na akili.
Msio na elimu mmetuchosha humu. Kama hamkusoma msiwalaumu waliosoma, bali walaumuni wazazi wenu kwa kutowapeleka shule wakaishia kunywa Chimpumu au mjilaumu wenyewe kwa kuwa vilaza shuleni!
 
Msio na elimu mmetuchosha humu. Kama hamkusoma msiwalaumu waliosoma, bali walaumuni wazazi wenu kwa kutowapeleka shule wakaishia kunywa Chimpumu au mjilaumu wenyewe kwa kuwa vilaza shuleni!
Nje ya mada mkuu , kama kuwa na digrii nne katamka mwenyewe mwakyembe , tatizo nn ?
 
Kwa kweli mh Mwakyembe mambo mengi hafuatilii katika wizara yake yeye ni mtu wa kwenda kwenye matukio tu na si utendaji
Kwa mfano hili jambo ni LA muhimu sana, lakini kwa vile Watanzania hawana tabia ya kushinikiza mambo basi linabaki kunyamaziwa.
Lakini wasikie Rais Magufuli anauliza eti Chanel zingine hazionekani kwenye ving'amuzi? Kesho yake kila mkataba unaingiwa. Mwakyembe aonyeshe tofauti ya hizo "degree nne" basi!
 
Naombeni mniache Mimi na degree zangu..tafaadhari tuheshimiane kila mmoja amlaumu baba yake/ mlezi au mhisani wake kwa kutotimiza waajibu wake katika kukusomesha.

Actually mi nko vizuri na sitaki kushauriwa na nyie msio na akili.
 
Back
Top Bottom