Mwakyembe: Nimemng'oa bosi ATCL kwa ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe: Nimemng'oa bosi ATCL kwa ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by baraka moze, Jun 8, 2012.

 1. b

  baraka moze Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ASEMA WANAOUNUNG'UNIKA WAKO HURU KUJIONDOA

  Fidelis Butahe | Mwananchi | 7 June, 2012

  SIKU nne baada ya kung'olewa aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ameamua kuanika tuhuma za ufisadi zinazodaiwa kufanywa na kigogo huyo.

  Miongoni mwa tuhuma hizo ni kuingia mkataba wa kununua ndege bila kumhusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) na kununua sare 15 za watumishi wa ndege kwa dola 50,000 za Marekani.

  Juni 5, Dk Mwakyembe alitengua uteuzi wa Chizi na kumteua rubani wa muda mrefu, Kapteni Lusajo Lazaro kukaimu nafasi hiyo, akisema uteuzi ulikiuka Sheria za Utumishi wa Umma.

  Mbali na kutengua uteuzi huo, pia alitangaza kuwasimamisha kazi vigogo wengine wanne wa shirika hilo, hatua ambayo ilianza kuibua malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi kwamba hatua hiyo ilitokana na majungu na ukabila.

  Waliosimamishwa kazi na Dk Mwakyembe ni Kaimu Mkurungenzi wa Uhandisi, Jonh Ringo, Mwanasheria ,Amini Mziray, Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Justus Bashara na Josephat Kagirwa ambaye alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Biashara.

  Jana, waziri huyo wa uchukuzi aliamua kufafanua tuhuma moja hadi nyingine zinazomhusu kigogo huyo na wenzake na kusema, mbali ya tuhuma za Chizi, wakurugenzi wawili wa shirika hilo walikwenda kushonesha sare 15 za wahudumu wa ndege nchini China kwa gharama ya dola 50,000 za Marekani (karibu Sh80 milioni).

  Akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo katika Uwanja wa Ndege wa zamani (Terminal One) jijini Dar es Salaam, Dk Mwakyembe alisema kutokana na hali hiyo, ameagiza kujazwa kwa nafasi zilizo wazi na kuwaonya watakaozichukua, kuhakikisha wanachapa kazi ili ATCL ipige hatua na kama wakishindwa watakuwa wamejiondoa wenyewe.

  Dk Mwakyembe alitoa miezi mitatu kwa shirika hilo kuanza kujiendesha kwa faida, ikiwa ni pamoja na kupata fedha za kuwalipa wafanyakazi wake.

  "Kwa kasi niliyoanza nayo watu kama Chizi ni lazima wakae pembeni, ni mtaalam katika masuala haya, lakini tatizo lake hakuwa muwazi," alisema Dk Mwakyembe.Chizi hakupatikana jana kuzungumzia tuhuma hizo, wakati wote Mwananchi ilipompigia simu yake ya kiganjani, ilikuwa imezimwa.

  Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, alitumia Saa 1:17 kuzungumza na wafanyakazi hao na kufafanua kwamba Serikali imechoka kutoa fedha za kuliendesha shirika hilo, akihoji iweje mashirika mengine ya ndege yaweze kusimama yenyewe, lakini ATCL iishindwe.

  "Tunaipenda ATCL iendelee na tunachukua hatua za kila aina ila tukiona tunashindwa tutaachana nalo ili, fedha zinazotumika hivi sasa zipelekwe kufanyia mambo mengine ya maendeleo," alisema Dk Mwakyembe.

  Tuhuma
  Akichambua tuhuma moja hadi nyingine za ukiukwaji wa sheria na taratibu, Dk Mwakyembe alianza kwa kutolea mfano mkataba tata baina ya shirika hilo na Air Bus ambao umeifanya nchi kudaiwa Sh69 bilioni na kusisitiza kuwa, kutokana na hali hiyo Serikali haikuwa tayari kufumbia macho mambo mengine ya ovyo yaendelea katika shirika hilo.

  Alisema wafanyakazi wote wa ATCL ambao wananung'unika baada ya kutengua uteuzi wa Chizi wako huru kuondoka katika shirika hilo, huku akionya atawatimua wengi watakaofanya mambo kinyume.

  "Nilipoteuliwa kuwa waziri wa uchukuzi siku chache baadaye nilisikia ATCL wanaleta ndege mpya, nilimwita Katibu Mkuu wa wizara anipe ufafanuzi wa jambo hilo, lakini, akaniambia hafahamu lolote," alisema Dk Mwakyembe.

  Aliongeza, "Ndege hiyo ilikodishwa na kutua nchini kwa mara ya kwanza mwezi uliopita kutokana na iliyokuwapo kuanguka mkoani Kigoma. Ndege hiyo aina ya Boeing 737-500 imekodishwa kutoka Kampuni ya Aero Vista ya Dubai."

  Dk Mwakyembe kwa sauti ya ukali alisema, "Niliamua kuwaita wakurugenzi wa ATCL ofisini kwangu saa 3 asubuhi, lakini wakaja saa nne na nusu, pamoja na hayo walinieleza kuwa jambo hilo liko safi na limeshafika kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali."

  Alisema baada ya siku moja, alipata taarifa kutoka ofisi ya AG ikieleza kwamba hawana mkataba huo.

  "Nikaona jambo zito kidogo, nikaamua kukutana na wale wawekezaji ambao walinionyesha mkataba ule ambao ulipitishwa bila wizara kujua, jambo hilo nililihoji pia…, nawambia ukweli mkataba huu niliuona upande wa pili sio kwa viongozi wa shirika," alisema Dk Mwakyembe.

  Alisema hivi sasa mchakato wa kuchunguza mikataba hiyo umeshaanza na kusisitiza kuwa, hiyo ndio ilikuwa moja ya sababu ya kumng'oa Chizi.

  Dk Mwakyembe alisema, "nchi haiwezi kuendelea kwa kukiukwa kwa sheria za ununuzi na ajira. Hata Kapteni Lazaro naye ameponea chupu chupu maana kabla ya kuwang'oa wakurugenzi tulipitia mafaili yao."

  "Msitegemee kubebwa ndugu zangu, nawaomba mchape kazi, mishahara yenu sio mizuri, lakini mkiweza kusimama mtakuwa na uwezo wa kujipangia hata mishahara," alisema Dk Mwakyembe.

  Alisema kwa kutambua mchango wa ATCL, Serikali imepata Sh4.9 bilioni kwa ajili ya matengenezo ya ndege ya shirika hilo na kuwataka kuzitumia kwa ufanisi fedha za shirika hilo."Hivi sasa inatakiwa kila baada ya miezi mitatu tunakutana na kuzungumza," alisema Dk Mwakyembe.

  Kapteni Lazaro aahidi ushirikiano
  Kwa upande wake, Kapteni Lazaro aliahidi kuyazingatia yote yaliyozungumzwa na waziri huyo, huku akiomba shirika hilo kuongezewa muda zaidi kwa kuwa miezi mitatu ni michache ili liweze kujitegemea.


  Kupanda/kushuka ATCL
  ATCL ni kampuni iliyoanzishwa baada ya Shirika la Ndege la Tanzania ATC kuingia ubia na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) mnamo mwaka 2002.

  ATCl ni moja ya mashirika ya ndege yaliyoonyesha kukua kwa kasi miaka ya 1980 na 1990, lakini lilianza kuyumba kutokana na uendeshaji mbovu na hali ikawa mbaya zaidi baada ya kuingia ubia na SAA.

  Serikali iliingia mkataba wa ubia na SAA mwaka 2002 kwa matumaini kwamba itakua na kuwa moja ya mashirika makubwa ya ndege Afrika, lakini hali ikawa kinyume chake.

  Kwenye mkataba huo, Serikali ikibakia na hisa 49 huku SAA ikiwa nazo 51, ambazo zilimfanya mbia huyo kuwa na nguvu ya kuamua mambo mengi.

  Serikali ilivunja mkataba na SAA Septemba 2006, baada ya kubaini kuwa ATCL inazidi kudidimia kiuchumi huku madeni yakiwa yanaongezeka kadri muda ulivyokuwa unaenda.
   
 2. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Mh Mwakyembe,

  Habari za leo,najua unanifahamu vizuri sana,pole na kazi na Hongera kwa Mambo mazito unayofanya. Kaka sio kwamba napingana na wewe kuhusu kumsimaisha kazi yule Chizi bali nataka kupata Ufafanuzi wa kauli yako ya Kwanza kuwa "uteuzi wake haukuzingatia Sheria na Kanuni"'

  Kwa kuwa wewe ni mwanasheria Mwandamizi mie sikubisha,ila baada ya kuonekana Media na watu wengi hawakukubaliana na Utenguzi wa wa huyo Chizi wewe ukaja tena na kuwa kuna Madudu ikiwemo ubadhilifu na Mkataba Mbovu wa ukodishwaji wa ndege Boeing 737-500 inayoruka.

  Kaka sio kwa kuwa Natokea Tanga ukadhani nimechukia wewe kupata nafasi hii kwa vile Mgosi mwenzangu(mwenye NUNDU) kapigwa Chini(La Hasha) Ninachotaka kujua kwa nini wakati unatengua uteuzi wake hukuteleza haya na umekuja kuyasema Mwisho?

  Je, kama tuhuma hizo za ubadhilifu ni kweli kwa nini iishie hapo kwenye kutengua uteuzi? Nini kazi ya CAG DPP,Takukuru na Mahakama? Kwa nini asifunguliwe mashtaka? Au ndo Kulindana kwa kuwa wote mna kadi za CCM mfukoni?

  Kama kweli huyu Chizi ni mbadhilifu basi ni vyema apelekwe mbele ya Sheria ili ile dhana ya ukabila ifutike.

  Nakutakia siku njema kaka Mwakyembe,tunakumiss pale kwa Mzee Kisamo kwenye nyama za Foil.

  Ni Mie Mgosi wa JF(mgeni wenu)
   
 3. M

  MORIA JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kila siku tumekuwa tukilaumu TAKUKURU,DPP,CAG, na Mahakama kuwa ni vichaka va kusafisha watu...tunahitaji uanaume wa namna hii sasa, acha dhana ya ukabila....ujasiri wa namna hii aliukosa JK dhidi ya wana Richmond, angewamwaga hadharani (kiume) leo CCM ingekuwa na turufu mbele ya watz...leo mgeni wetu unaamini TAKUKURU ile ya hosea..mmmh!
   
 4. Akagando

  Akagando JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 536
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Tabu kweel kweli
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,082
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 0
  Hivi wewe mgosi, unataka ufafanuliwe kipi zaidi? naona unazunguka zunguka, sijui unanijuwa nakujuwa, kadi za ccm mfukoni! inahusu nini yote hiyo?

  Kaachishwa kazi kwa kuwa sheria za ajira hazikufuatwa, sasa nani hakufuata hilo jingine. Nyie mtu akifanya kosa asipofanya kosa. Nendeni basi mkagombee ubunge mchaguliwe kuwa Mawaziri. Au fanyeni kitu kionekane hata Rais akuchaguwe kwa kuwa kaona ulichokifanya. Nyama za foil zinauhusiano upi na ATC?
   
 6. M

  MtotoWaMandela Member

  #6
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata kwenye siasa MUNGU yumu anasema usiseme uongo ni dhambi kama mwakyembe anasema kweli kuhusu hujuma za Mr Chizi,MUNGU ambariki sana,lakini km anasema mambo ambayo hayapo tunamuachia MUNGU aliyesema Usimshuhudie jirani yako uongo
   
 7. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,727
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Namkubali huyo jamaa (Mwakyembe), tatizo chama aliko siyo! Kuhusu maamuzi yake nadhani tuvute muda ukweli utaonekana, siyo busara kubeza.
   
 8. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,505
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Huna maneno mengine tofauti na haya?
  The unseen is illustrated by the seen.
   
 9. Akagando

  Akagando JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 536
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  inaonekana njisi gani ulivyo kodiwa kuweka avatar zisivyo na maana kwako.nawe umekosa avatar ya kuweka mpaka hiyo ya kidini kwa upande wako uendi hata kanisani.
   
 10. b

  baraka moze Member

  #10
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  wewe unataka ufafanuliwe kivipi?
   
 11. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #11
  Jun 9, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Ungeungana na vilazaa wa Claudz kuhoji hayo ungekuwa unatumia akili zako vyema sana.Huitaji kuwa na PhD kama Mwakyembe kujua madudu aliyoyafanya CHIZI.
   
 12. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,203
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tatizo hapa ni ushabiki,tuangalie hoja iliyoko mbele,sasa basi kama sheria hazikufutwa aliyepindisha sheria makusudi au bila kujua wajibu wake naye awekwe wazi naye aungane na bwana Chizi.Hapa ni think tank na si gossiping chamber.
   
Loading...